M4C kutua Iringa mjini kesho

Martoism

Member
May 31, 2012
36
21
Ni saa chache zimebaki kabla ya wananchi wa manispaa ya Iringa mjini na viunga yake kukutana na makamanda, wabunge na viongozi wa kitaifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA katika mkutano wa hadhara utakaofanyika uwanja wa mwembetogwa baada ya maandamano ya takribani km 2.

Katika mkutano huo viongozi wataongelea na kujadili maswala mbalimbali yanayo husu mustakabali wa maisha ya wananchi. Aidha pamoja na mambo mengine ziara hiyo ina lengo la kuimarisha na kupanga imara safu za viongozi kuanzia ngazi ya matawi,vitongoji ,mitaa, vijiji, kata, wilaya, majimbo, mikoa, kanda hadi Taifa ikiwa ni maandalizi ya mipango kabambe ya kuchukua dola 2015.

Ni muhimu kufahamu kuwa Iringa mjini ni mojawapo kati ya majimbo Tanzania bara yalichukuliwa kwa kile kinachaitwa "Nguvu ya Umma" dhidi ya nguvu ya dola, makatazo au maelekezo na amri walizokuwa wanapewa Wakurugenzi kutokutangaza matokeo iwapo wapinzani wangeibuka kidedea kama majimbo ya Nyamagana, Arusha mjini, Ubungo, kawe n.k.

Ni muhimu pia kufahamu kuwa Dr. Slaa zaidi ya mara 2 alizuiwa kufanya mikutano katika uwanja wa mwembetogwa kwa kufyatuliwa mabomu na risasi za moto. Ni imani yangu kuwa "Justice shall always prevail" karibuni Iringa wakombozi wetu.
 
Wasije wakawafyatulia risasi na mabomu ya machozi kama wanavyofanya Moro sasahivi! Otherwise, kila la heri.
 
Nafikiri nguvu kubwa wekeni kwa mama makinda ametuendea mabaya mengi waambieni wanajimbo wake
 
kamanda wa polisi mkoa wa Iringa usifanye kama aliyofanya jirani yako wa Mji kasoro bahari. CCM haibebeki hata kwa turubai. Nadhani utakuwa aware na hilo!
 
Ni saa chache zimebaki kabla ya wananchi wa manispaa ya Iringa mjini na viunga yake kukutana na makamanda, wabunge na viongozi wa kitaifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA katika mkutano wa hadhara utakaofanyika uwanja wa mwembetogwa baada ya maandamano ya takribani km 2.

Katika mkutano huo viongozi wataongelea na kujadili maswala mbalimbali yanayo husu mustakabali wa maisha ya wananchi. Aidha pamoja na mambo mengine ziara hiyo ina lengo la kuimarisha na kupanga imara safu za viongozi kuanzia ngazi ya matawi,vitongoji ,mitaa, vijiji, kata, wilaya, majimbo, mikoa, kanda hadi Taifa ikiwa ni maandalizi ya mipango kabambe ya kuchukua dola 2015.

Ni muhimu kufahamu kuwa Iringa mjini ni mojawapo kati ya majimbo Tanzania bara yalichukuliwa kwa kile kinachaitwa "Nguvu ya Umma" dhidi ya nguvu ya dola, makatazo au maelekezo na amri walizokuwa wanapewa Wakurugenzi kutokutangaza matokeo iwapo wapinzani wangeibuka kidedea kama majimbo ya Nyamagana, Arusha mjini, Ubungo, kawe n.k.

Ni muhimu pia kufahamu kuwa Dr. Slaa zaidi ya mara 2 alizuiwa kufanya mikutano katika uwanja wa mwembetogwa kwa kufyatuliwa mabomu na risasi za moto. Ni imani yangu kuwa "Justice shall always prevail" karibuni Iringa wakombozi wetu.

makamanda karibuni sana Iringa.Hata kama Njombe sasa ni mkoa mpya.Tungependa hata jeshi likafanya kazi ya ukombozi ktk jimbo linaloongozwa na bibi kiroboto.Huyu anatakiwa kushikiliwa pua hadi kieleweke kwani tukiachia kidogo tu kataamka na kutaka kugombea tena licha ya kutangaza kutokugombea.
 
Bi Kiroboto hawezi tena akisema afanye hivyo aibu ya mwaka itamkuta! Ukombozi waja kwenye Mkoa wetu mpya! M4C karibuni Iringa yetu
 
Wasije wakawafyatulia risasi na mabomu ya machozi kama wanavyofanya Moro sasahivi! Otherwise, kila la heri.

wakiua ndiyo wana haribu kabisa, wewe uko Arusha je baada ya kuua imesaidia kupunguza nguvu ya CDM..
 
Mkuu, tatizo la ccm na serikali yake ni ufupi wa akili zao! Huitaji kuwa Sheikh Yahya kutambua kwamba matumizi ya nguvu yanaongeza hasira na chuki kwa wananchi. Inazidi kukisambaratisha na kupukutisha wanachama wao na kukijenga na kuimarisha cdm. Ccm imekufa Arusha kwa sababu hiyo lakini hawajifunzi!? Kweli siku za mwisho mgonjwa atakataa uji na kwikwi zitamwandama!
 
Kama munasema baada ya mauaji ya ARUSHA CDM imezidi kwa na nguvu ARASHA,sawa mukifika na IRINGA muwatume vijana wenu wawanyang'anye silaha POLISI ili damu imwagike na muungwe mkono Muzidi kuwa maarufu.
 
Kama munasema baada ya
mauaji ya ARUSHA CDM imezidi kwa na nguvu ARASHA,sawa mukifika na IRINGA
muwatume vijana wenu wawanyang'anye silaha POLISI ili damu imwagike na
muungwe mkono Muzidi kuwa maarufu.
Akili hazikutoshi. kumbe mpo mnaoamini kuwa Arusha Chadema walitaka kupora silaha? ama kweli ujinga mzigo
 
Back
Top Bottom