M4C Kibaha: Shukrani Isiyo Rasmi kwa Polisi

Highlander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
3,093
Reaction score
1,077
Ndugu wanachadema mnaosoma uzi huu, polisi si wabaya kila siku. Kama yupo mwenye mawazo tofauti naomba aeleze hapa. Leo nimepata taarifa ya kufurahisha sana kutoka kwa Kamanda aliyehudhuria Uzinduzi wa Kanda ya Mashariki Pale Kibaha Juzi, kuhusu nidhamu na heshma kubwa waliyoonesha askari polisi kwa viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo pale Kibaha juzi.

Askari wa usalama barabarani walisimamisha magari yaliyokuwa yakitoka Dar, na yale yaliyokuwa yakitoka Mikoani kuruhusu Viongozi wakuu wa Chama kuingia kwenye eneo la Mkutano pasipo bugdha. Askari walio vaa sare za Jeshi la Polisi walijipanga katika maeneo ya Mkutano kwa nidhamu ya hali ya juu kulinda amani. Hakuna aliyeshika mibunduki ya kutisha wananchi. Katika tukio jingine, Mheshimiwa Mwenyekiti aliongeza dakika 15 juu ya muda uliopangwa na wanausalama kwa ajili ya hotuba yake, lakini hakutokea polisi kumshusha kutoka kwenye jukwaa.

Wanachadema waliozungumza nami wanasema wanayo furaha kubwa sana kuona heshima hii ambayo polisi Mkoa wa Pwani wameonesha kwa Viongozi wa Chama hiki kinachochukua dola 2015. Kwa kuwa ukiwaheshimu ziongozi wakuu wa chama unakuwa umekiheshimu chama, tunadhani RPC Mkoa wa Pwani anastahili pongezi, shukrani na heshima kwa busara hii. Hii ndiyo njia tunayotakiwa kuenda nayo kuanzia hapa.

Kama taarifa hii ina makosa naomba waliokuwepo Kibaha wasahihishe kwa lengo la kukuza na kulinda amani ya nchi yetu. Nimepewa zawadi niitume kwa askari polisi wa Mkoa wa Pwani. Tafadhali pokeeni hizi nyimbo 2 kutoka kwa Watanzania wenzenu.
 
Attachments

huo ndio ukomavu wa kisiasa hongera kwa polisi pwani msikubali kutumiwa
 
Mbona kuna uzi humu wa mhudhuriaji mmoja aliyedai kuwa pikipiki zilizokuwa mkutanoni zilinukuliwa namba zake?.
 
Polisi hawatakiwi kukomaa kisiasa, kwa kuwa hawatakiwi pia kujihusisha na siasa. Mara nyingi polisi huwa wanapata amri kutoka nje ya jeshi hilo, sana sana kutoka kwa wakuu wa wilaya. Hongera mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwa kukomaa kisiasa
 
hata wao hawaipendi CCM kwa kuwa huwa wanaamrishwa tu ndio maana huleta fujo, lakini sitashangaa kusikia huyo RPC kapelekwa Katavi
 
Iwe kweli au uongo hivyo ndiyo inatakiwa kuwa, kwasababu kuna leo na kesho
 
i was ther na nilikuwa jirani na baadhi ya polisi,walikuwa wanasikiliza kwa makini,babu mmoja usalama wa ccm maarufu pale kibaha alikuwa bize na mikaratasi akichukua notes,tulikuwa tunamtupia mimacho kila dakika hadi alikimbia eneo.
hivi dunia ya leo bado haya mausalama ya ccm yanachukua note kwa karatasi!!!
 
..asanteni sana polisi,hiki ni chama tawala hata kama hakijashika dola,wakitoa tamko nchi inasikiliza,hutaki waulize ccm, subiri 2015.
 
Hongera sana Jeshi la Polisi, hongera wakazi wa kibaha kweli mmewathibitishia wananchi kama wakijenga tabia ya utii sheria bila shuruti hakuta tokea madhara yoyote, hapo walitii ndio maana hapakuwa na shuruti
 
..asanteni sana polisi,hiki ni chama tawala hata kama hakijashika dola,wakitoa tamko nchi inasikiliza,hutaki waulize ccm, subiri 2015.

Mkuu Gefu, kauli yako ina ukweli sana. Ninachokiona kutoka kwako lakini pia kutoka kwa Mkuu Ben Saanane na wachangiaji wengine ni kwamba wanachadema wanatuma meseji polisi; kwamba ugomvi na vyombo vya dola unakuwa haupo wanapotumia hekima. Polisi,Usalaama wa Taifa, Jw na taasisi nyingine wajue hili; kwamba wakifanye mema wataambiwa, wataheshimiwa, watapendwa--pengine watapendwa hata kushinda upendo wanaopewa na wavurugaji wa nchi waliopo madarakani!
 
una adithia kama ulikuepo vile by the way i dont see any changes done by policcm there
 
Hapo ndo kuna utata kati ya hizi habari mbili, au huyu aliyeanzisha huu uzi ndo wale mamlupu wa nepi!
 
RPC Tayari kashajihamisha kikazi...Nahisi watampleka makao makuu kwa kazi maalumu...Hii habari si nzuri hata kidogo kwa CCM ...
 
Mbona kuna uzi humu wa mhudhuriaji mmoja aliyedai kuwa pikipiki zilizokuwa mkutanoni zilinukuliwa namba zake?.

Haya mambo yapo ila yanafanyika kwa siri. Polisi wanarekodi mikanda ya mikutano wakiwa wamevaa nguo za kiraia.
 
Tanzania inabidi tutengeneze misingi ya utaifa upya, ambayo itakuwa balanced kwa vyama vyote, iwe tawala au upinzani! Tukiweza kufanya hivyo tutakuwa tumelisaidia taifa letu!
 
Back
Top Bottom