M4C Kibaha: Shukrani Isiyo Rasmi kwa Polisi

M4C Kibaha: Shukrani Isiyo Rasmi kwa Polisi

ndgu yng upo sahihi, tena walisimamisha mpaka mabasi na msafara ukapita, na uwanjan walikuwepo tena wengi ila nao pia waliguswa na hotuba za waheshimiwa. Ndo maana wakawaheshimu. Upo sawa.
 
Serikali inapobadilika jeshi la polisi hujigeuza na kuelekea katika serika mpya, hivyo walivyofanya polisi ni sahihi kabisa, ishu ni kwa wakuu wa wilaya mikoa na baadhi ya idara ambazo zinaendeshwa kisiasa. serikali ikibadilishwa tu wao kimekuala kwao ndy maana wankuwa wakali sana wasije wakavurunda. hy ni kawaida katika system
 
Kamaq ni ukweli basi huyo kamanda wa mkoa, mkuu wa mkoa na wakuuwa wilaya za Mkoa wa pwani nilazimwa wapewe shavu mwaka 2015

Wazo lako ni sahihi sana Mkuu. Nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi Katika Nchi za Nje la Marekani, CIA, ni nifasi ambayo ipo kisiasa sana kwa hiyo wananchi wanapobadili chama kinachoongoza serikali aliyekuwapo katika nafasi hii imekuwa kawaida anabadilishwa; lakini kama nimekumbuka vizuri Obama alimwomba Mkurugezi aliyekuwapo wakati wa Bush abakie pale. Kwa hiyo binafsi nakubaliana na wewe Mkuu. Katika mambo ambayo Chadema wanafanya sasa liwepo na jambo la kuwasoma watumishi waliopo katika Serikali hii inayoongozwa na CCM kwa lengo la kujua pumba ni zipi hapa, na mchele ni upi. Dola inapochukuliwa 2015 mchele ubaki, pumba zoooote Tabata Dampo!
 
Nilichosema kuhusu Polisi kuandika namba za Pikipiki na Magari yote yaliyoshiriki katika mapokezi ya viongozi walikuja Kibaha kwa ajili ya uzinduzi wa M4C Kanda ya Pwani ni kweli tupu. Aidha kundi hilo la Askari hao walikuwa wameongozwa na ASP Rashidi, Kwa jinsi walivyokuwa wanafanya kazi hiyo si rahisi kujulikaana na pia walikuwa wanafukuza kila aliyekaribia eneo hilo. Kibaha One ilifanya mbinu kubwa kuweza kunasa uovu huo.
 
Ukweli ni kwamba wale Polisi niliyoeleza kuwa walikuwa wanachukua namba za pikipiki na magari yaliyoshiriki katika mapokezi ya Viongozi walishiriki katika uzinduzi wa M4C Kanda ya Pwani walifanya kazi hiyo kwa usiri mkubwa na Kiongozi wao walikuwa ASP Rashidi. Muulizeni ASP Rashidi akanushe
 
Nilichosema kuhusu Polisi kuandika namba za Pikipiki na Magari yote yaliyoshiriki katika mapokezi ya viongozi walikuja Kibaha kwa ajili ya uzinduzi wa M4C Kanda ya Pwani ni kweli tupu. Aidha kundi hilo la Askari hao walikuwa wameongozwa na ASP Rashidi, Kwa jinsi walivyokuwa wanafanya kazi hiyo si rahisi kujulikaana na pia walikuwa wanafukuza kila aliyekaribia eneo hilo. Kibaha One ilifanya mbinu kubwa kuweza kunasa uovu huo.

Mkuu Kibaha One, sidhani kama kuna mtu anayekataa kuwapo zoezi hilo. Tatizo linalosumbua watu ni kwamba pengine ungelifanya jitihada ya ziada kidogo tu ili kuipatia taarifa yako maana zaidi.

Lengo la kuchukua hizo namba lilikuwa ni lipi? Tunajua kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali vinashirikiana na kitengo cha ulinzi na usalama cha chama. Pengine Ungefanya kuzungumza na kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Chama, yaani Red Brigade au hata huyo mkuu wa hicho kikosi cha Siri, ASP Rashid, wangeweza kuweka mwanga kwenye hili swali Lengo la kuchukua hizo namba lilikuwa ni lipi? Hii ingesaidia zaidi nadhani. hakuna anayekataa zoezi hilo kufanyika nadhani. Hebu tusaidie sasa kufanya utafiti kwa ASP Rashid. Namba za magari alikuwa anazichukua kwa sababu gani?

Je wanataka kuhujumu wenye magari hayo? Kwa hiyo ule uzi wako si mbaya as such, ila kwa kuwa unaelekea kuwa mdadisi mzuri, hebu fanya udadisi tujue malengo ya kuchukuwa zile namba yalikuwa yepi? Na kama kuna mtu aliweza kupata picha ya askari mmoja akifanya zoezi hilo hebu tumbukiza hiyo picha hapa waandishi wa habari wapate mahali pa kuanzia kwenda kumuuliza RPC hizo namba zilikuwa zinachukuliwa kwa sababu gani. Au nimekosea hapo Mkuu Kibaha One?
 
Mkuu tenende, Kwa taarifa tu ni kwamba mikutano yote muhimu zinakuwepo idara zote za siri kutoka majeshini. Wote wanakuwa na kazi ya kuweka rekodi ya tukio kwa tahadhari yoyote, iwe rahisi kujua tatizo lilianzia wapi: Wanakuwepo Military Intelligence, wanakuwepo UWT, Naye Afande Kanumba anakuwa na watu wake. Na unakuwa hujui huyu katoka wapi. Unaweza ufikiri ni CID kumbe ni military intelligence. Malengo ni mema kabisa wakati wote. Mikutano mikubwa yote wanakuwepo. Kwa kuwa Chadema wanachukua dola 2015 ni vizuri mkaanza kuwazowea hawa watoto wetu. Nia ni njema kabisa kwa kadri ninavyojua. Unao uhuru kunisahihisha lakini, kama kuna kitu sikioni sawasawa.

Sina ugomvi na kazi hii waifanyayo ya kurekodi mikutano. Lakinikwa nini iwe mikutano ya CHADEMA tu?! Kwa nini ya CCM hairekodiwi?!
 
Sina ugomvi na kazi hii waifanyayo ya kurekodi mikutano. Lakinikwa nini iwe mikutano ya CHADEMA tu?! Kwa nini ya CCM hairekodiwi?!

Una uhakika gani kwamba mikutano ya CCM hairekodiwi? Nimeongea hivyo kutokana na uzoefu katika mikutano mikubwa ambayo wanakuwapo wanasiasa wazito kama rais ama Waziri Mkuu. Huwa Waandishi wa habari wanachanganyikana na watu wa ulinzi na usalama unakuwa hujui yupi ndo yupi. Yale marundo ya makamera ambayo huwa unayaona kwenye ile mikutano si wote ni waandishi pale. Hebu kaangalie vizuri kama kweli mikutano ya ccm hairekodiwi. sidhani kama umeliona hili sawasawa Mkuu wangu.
 
Highlander, wewe ni mtetezi wa CCM au usalama wa taifa au polisi?!.. Kitengo hicho unalipwa? KAMA HULIPWI basi nenda kwenye mikutano ya makundi haya mawili. Wanachama utawajua na waaandishi utawajua. Kundi linalobaki ni polisi.

Sijadharau mchango wako, lakini napenda ujue nazungumza kitu ninachokiona na kukisikia kutoka kwa watu wanaotumwa kurekodi. Ipo siku tutafahamiana
na kupeana vielelezo.

We Tenende, mtu wa Kikusya hao polisi wako na ccm, na hao usalama wa taifa watamjulia wapi. Mi najiwekea tu post zangu hapa nisikie watanzania wenzangu wanasema nini.
 
Back
Top Bottom