M23 yatuma salam za uimara wake kwa vikosi vya KDF na FDNB vilivyopelekwa Congo kuthubutu kuwapokonya silaha

Akilihuru

JF-Expert Member
May 20, 2022
1,444
2,833
Za asubuhi wakubwa, weekend inaendeleaje?

Leo nawaletea muendelezo wa kile kinachojiri huko Congo katika oparation ya jeshi la kanda yetu hii ya EAC. Oparation hii mahsusi imebuniwa kwa lengo la kuwapokonya silaha waasi wote waliopo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ila walengwa haswa wa oparation hii ni wale vijana walioshiba mafunzo ya kijeshi, wenye weledi wa kupambana na adui mchana au usiku, angani au ardhini, vijana hawa sio wengine bali ni lile kundi imara la waasi wa M23.

Kabla oparation hiyo haijapangwa, viongozi wa nchi zetu za maziwa makuu walitoa kwanza siku maalum na saa kwa makundi hayo kusalimisha silaha zao wenyewe, kuachia maeneo yao (walioyateka) na kusubiri michakato mingine ya kisheria itakayofanywa kwa waasi hao.

Baada ya kumaliza kutoa tamko hilo la kusalimisha silaha, ndipo viongozi wa nchi hizo wakatuma majeshi yao Congo kwa ajili ya kwenda kuwawajibisha waasi wote watakaokaidi kutii agizo hilo la serikali na nchi za maziwa makuu.

M23 ambalo ndio kundi imara na hatari kwa majeshi yaliokwenda huko, lilikaidi maagizo hayo na kusubiri kuona ni nini kitachofanywa na vikosi hivyo vilivyodai kwamba vinakwenda kusafisha uasi katika nchi hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika.

Juzi M23 imefanya oparation zake inazofanyaga kila siku na kupelekea watu 50 kufariki dunia. Hii ni salam ya dhahiri kwa vikosi hivyo vya Burundi na Kenya vilivyopelekwa huko eti kujaribu kuwapokonya silaha 'wanajeshi' wenzao, kama vile mtu anapojaribu kumpokonya mtoto wake pipi.

Kifupi ishaonesha kuwa M23 ni maji marefu ndio maana kdf na fdnb wanashindwa kuthubutu kuingiza miguu katika maji yao (maeneo yao) wasije wakazama mazima ikawa aibu kwao na kwa nchi zao.

Ushauri wangu ni kuitaka serikali mpya ya Congo iangalie namna bora ya kuongea na kundi hili kwa mara ya mwisho kwa lengo la kuleta amani maeneo hayo. Ikishindikana ndio nguvu kubwa na ya pamoja itumike. Ila kuyategemea majeshi haya ya Burundi na Kenya kuleta amani ni kupoteza muda bure, maana hawana uwezo hata waku deal na mayi mayi achilia mbali vijana hatari wa M23.
 
Wewe acha kusifia watu wanaoua raia. Me nilidhani utasema wameua wanajeshi 50 kumbeunazungumzia kikosi kinachoua Raia.

Hata angekua mwanajeshi mmoja wa M23 akiwa na Machine Gunn anawezakuuahata raia 1000.

Kama upo nao subiri moto mkali unakuja. Jehanam mtaiona mkiwa duniani hapahapa. Siku zinahesabika kufikia ile siku muhimu yenye huzuni kubwa kwa M23 wote na familia zao. Save date
 
Kwa hio unamaanisha kikundi cha PaKa road M23 kinaweza kuzishinda nchi zaidi ya 4 za EAC zinazoenda kukifunza adabu hicho kikundi chenye uroho wa madini yaliyopo kwenye ardhi ya Congo?!
Sasa kama Burundi na Kenya wametuma majeshi yao, lakini majeshi hayo yameshindwa kuingia nao vitani unafikiri ni nani m'babe wa vita hivyo?
 
Kwa hio unamaanisha kikundi cha PaKa road M23 kinaweza kuzishinda nchi zaidi ya 4 za EAC zinazoenda kukifunza adabu hicho kikundi chenye uroho wa madini yaliyopo kwenye ardhi ya Congo?!

Hiki kikundi dawa yake ni ndogo tu. Kumshawishi Tanzania ambaye ana uwezo wa kumtoa, awe na nia na sababu ya kumtoa. Tanzania akikubali kwa dhati kabisa, kwake hilo zoezi ni la majuma machache tu. Ukichukua kila nchi ya EAC kuwemo kwenye kikosi hiki, hilo halitazaa matunda, maana kuna wengine wanatuhumiwa kuwa upande wa maadui.
 
Back
Top Bottom