Salaam tena wakuu.
Baada ya uzi wangu wa jana usiku kufutwa kwa sababu ambazo sikujulishwa, asubuhi hii nimeamka na kuamua kufuatilia tetesi za jana.
Ni kweli kwamba mtu alituhumiwa na kutajwa kama MM2 na kamati kuu ya CHADEMA, ameamua kujitokeza na kuzungumza na wanahabari.
Mkutano huo na wanahabari ambao awali ulikua ufanyike Ubungo Plaza saa nne asubuhi, hivi sasa umehamishwa na utafanyika Travetine Hotel - Magomeni kuanzia saa tano na nusu asubuhi.
Kulingana na chanzo changu cha habari, MM2 asingependa atajwe mapema mapema kwenye mitandao kwa sababu za kiusalama ila ni kweli kwamba atazungumza na Wanahabari leo.
Mada atakazozigusa ni pamoja na ukweli kumhusu yeye, msimamo wake na wa kikundi chake dhidi ya wanaoitwa Wahafidhina na mikakati yake na kikundi chake pamoja na harakati watakazofanya mikoani katika kile wanachokiita demokrasia ya kweli ndani ya CHADEMA.
Nitaendelea kuwaupdate juu ya kinachoendelea.
NB: Mod sio mbaya nikapata taarifa ya sababu ya kufuta uzi wa jana. Thanks in advance.