Lwandamina unasubiri nani akwambie nini?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,309
12,604
Timu ya Azam haipati matokeo ikiwa mikononi mwako pia. Inawezekana tatizo ni wewe, wachezaji, au viongozi na au wote kwa pamoja.

Lakini unasubiri hadi Azam ushuke nayo daraja ndio uondoke au unasubiri kutupiwa virago?

Wote tunafahamu kuwa wachezaji wako wana mgomo baridi kwaajili ya wachezaji wenzao waliokuwa wanadai maslahi kwa niaba Yao pia ambao wamesimamishwa kwa muda usiojulikana. hivyo wana waunga mkono kwa njia hii.

Tazama mpira waliocheza dhidi ya pyramids, walijituma kwa maslahi Yao wenye kama sehemu ya marketing yao wenyewe kwenye soka la Africa na dunia lakini sio kwaajili ya Azam team.

Wachezaji wa Azam ni kama wale wa Manchester united walivyomwangusha Ole. Timka zako bhana ili uwaache wafu wazikane wenyewe. Au unaogopa kupoteza maslahi?
 
Inasemwa Kuna mgomo pale Azam, WACHEZAJI wanashinikiza wenzao waliosimamishwa warudishwe kundini .
 
Hivi wachezaji wa team B ama under 20 si unaruhusiwa kuwachezesha.

Kama kuna watu wana mgomo basi ni kuwaweka pembeni.. wawe wanafanya mazoezi wanarud kulala
 
Kama ni mgomo baridi sawa.

Kuna siku nimeangalia match yao, yaani mpaka nikasema, hata mimi naweza kucheza. Wachezaji ni goigoi hasa yule Nado. Akiguswa kidogo kaanguka, sijui hali chakula?
 
Tuliambiwa azam fc ni matajiri hapo bongo inakuwaje hadi leo watu wanadai mishahara hawajalipwa na adhab wamepewa kisa kudai mishahara?
Bongo bahati mbaya
 
Tuliambiwa azam fc ni matajiri hapo bongo inakuwaje hadi leo watu wanadai mishahara hawajalipwa na adhab wamepewa kisa kudai mishahara?
Bongo bahati mbaya
siyo mashahara..kabla ya kuwatoa wasomali waliahidiwa wakishinda wachezaji wote wtapewa usd 10,000 ilivyotoka viongozi nao wakafosi wawe part ya mgao sasa team kama azam kweli ni ya kugombania milions 23 na wachezaji, hao watatu waligoma wakasimamishwa
 
basi kuna shida mahali tunaaminishwa ni timu tajiri hapa bongo lakn wanalilia pasu pasu
 
Back
Top Bottom