Luteni Yusuph Makamba

Luteni Yusuph Makamba

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
855
Yusuph Makamba, si jina geni. Ni jina ambalo katika siasa za Tanzania huwezi ukaliacha kutokana na umaarufu wake hasa baada ya kuwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam enzi za Rais Jakaya Kikwete.

Mzee Makamba amekuwa maarufu kutokana si tu na utendaji wake, bali hata na uwezo wake wa kushika vifungu vya Biblia kitabu kitakatifu cha Wakkristu na Quran.
Umaarufu wa Mzee huyu ambaye pia aliwahi kuwa Luteni wa Jeshi, unaonekana kwenye baadhi ya nyimbo za bongo fleva. Mwanamuziki Jay Moe aliwahi kutaja jina la Makamba kwenye wimbo wake wa 'cheza kwa step' kadhalika mwanamuziki Joseph Mbilinyi aka SUGU aka Mr. Proud aka Mr. 2 aka Jongwe, naye aliwahi kutaja jina la Makamba kwenye wimbo wake 'Dar--DSM' wimbo aliyomshirikisha Balozi. Kutajwa zaidi kwa Makamba, kunaonesha kuwa, yeye ndiye Mkuu wa Mkoa ambaye ametajwa zaidi kuliko Mkuu wa Mkoa yeyote kuwahi kutokea Tanzania.

Mtu yeyote kutajwa kwenye muziki ama sanaa zingine hasa na vijana ni kiashiria tosha kwamba mtu huyo ni kipenzi cha watu na anakubalika kwenye jamii. Mfano wa mwanasiasa mwingine kutajwa zaidi kwenye sanaa ya muziki kwa Tanzania, ni aliyewahi kuwa Rais wa kwanza na waziri Mkuu, Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Jina la Nyerere, ndilo jina pekee kwa Tanzania kutajwa zaidi kwenye sanaa ya muziki na maandiko ambayo kila siku iendayo kwa Mungu, basi jina lake hutajwa aidha kwenye maandiko au kwenye sauti.

Je, ni mwanasiasa gani unaona amenyimwa haki hiyo ya kutajwa na wasanii hasa wanamuziki kwa sasa?
 
Back
Top Bottom