Luteni Makamba:Kaburi la CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Luteni Makamba:Kaburi la CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, Nov 30, 2010.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Siyo siri, kwa sasa hivi CCM inavuna kile Katibu wake Mkuu alichopanda.
  Luteni Makamba, Katibu Mkuu wa CCM amekifikisha chama katika wakati mgumu pengine kuliko wakati wowote tangu kuzaliwa kwake mwaka 1977.
  Wengi tulio wana CCM tulijiuliza ina kuwaje huyu jamaa wa cheo kidogo jeshini angeweza kuhimili asasi hii kubwa ya kisiasa.
  Lazima tukumbuke kuwa kwanza Luteni ni cheo ambacho ni cha platoon commander, luteni anaongoza watu si zaidi ya 12.
  Makamba kielimu hayuko juu sana , hivyo basi hata kwa uzoefu yeye si strategist, siyo political thinker, wala si administrator wa kutumainiwa.

  Madudu yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi ni ya kutia aibu kwa chama kikongwe kama CCM.
  Siyo siri vile vile kuwa kwa kukosa usomi katika CCM,chama hakina sera wala dira inayoeleweka, hivyo basi chama kinaondokewa kwa wingi na vijana hasa wa rika la chini.
  It is no longer mass party.
  CHADEMA , chama kidogo sana , kimeweza kwa ustadi mkubwa kuamsha hisia za vijana wengi , na kuonekana kama tegemeo la wanyonge.
  Wengi wetu tulivutiwa na slogan ya Ari mya,Nguvu mpya na Kasi mpya.This unfortunately was hot air which did not feature in any plans or strategies.

  Makamba amekumbatia makundi fulani ambayo ni dhahiri hayana mvuto kwa jamii-na kundi hilo ni kundi la mafisadi.
  Sura ya chama inaanza kujigeuza kuwa ni kundi la watu wa aina fulani.Siyo siri kuwa Lowassa, Rostam,Chenge na wengine wa mlengo huo ndio wanaoua sura ya chama katika jamii.
  Siasa huwa haina mahakama, mahakama yake ni wananchi.
  Ni wazi vile vile JK amegutuka, ingawaje hatujui kama amechelewa au la. Matukio ya Uchaguzi mkuu na uteuzi wake wa baraza la mawaziri ni kielelezo tosha juu ya kugutuka huko.
  Ni juu ya mwenyekiti wa CCM kuchukua uamuzi mzito kabla 2015 kukiokoa chama.
  But well, what the heck!!
  Hata Mwalimu alisema CCM si mama yangu!
  But it is sad to see a good party machinnery go to waste.
  Makamba , kaburi la CCM!
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  nenda hoteli yake iliyo morogoro inaitwa Mount Usambara Resort ndio utajua huyu jamaa hana uwezo wa kuendesha mambo properly...
   
 3. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,531
  Trophy Points: 280
  Well said.
   
 4. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Unatukumbusha au kwako ndio wazo jipya? ulikuwa wapi kujua mambo haya mbona ume chelewa sana kujua,lakini kwa vile wewe ni CCM ndio maana Nyani haoni......Hivi ulidhani mmeshindwaje uchaguzi mwaka huu mpaka mkaamua kuwa vibaka na kupora ushindi wa CDM? poleni sana nikuongezee nalingine amba huja jua bado Mwenyekiti wenu amekuwa mwasisi wa udini nchini sijui mtaponea wapi? poleni sana
   
 5. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kwali hiki chama kimebaki kama kichekesho, kama rais haijapita mwezi tangu kuapa kuwa rais, kamteua waziri aliyeruhusu peasa za EPA na meremeta kuibiwa eti mbunge wa kuteuliwa!! hii inatoa picha gani kwa kikwete???

  Bado anatapatapa tu, hamna kitu hapa, bado mshikaji wa makamba, tatizo ni kwamba hakumzawadia uwaziri mtoto wa makamba.
   
 6. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  ukweli uteuzi wa mh yule ni aibu. hata kama wako karibu vipi bado wale wa mama wawili hawakuhitajika. ndo mistake wanayofanya bila kuelewa ama kwa kuelewa na kukaidi. yetu macho na masikio.
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Makamba its time to retire
   
 8. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kaburi la ccm ni aliyemchagua na wanaomuheshimu!!
   
 9. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  ''Lazima tukumbuke kuwa kwanza Luteni ni cheo ambacho ni cha platoon commander, luteni anaongoza watu si zaidi ya 12.'' Umeongea mengi yapo mazuri ambayo yanaonesha picha ya Makamba lakini hapo kwenye cheo cha Luteni anaongoza watu 12 u r wrong usiwapotoshe watu.

  Tafuta wakati uwaulize au fanya uchunguzi kabla ya kutudanganya!
   
 10. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  udini udini udinh udini mwanangu herii herii mtangulie peponi muiache TZ yenye watu poor but happy!
   
 11. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Makamba Ndio picha Halisi ya ccm usimlaumu yeye maana wenyewe wanamwamini
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  U
  Mkuu naona unalitazama tatizo la CCM kiunazi zaidi kuliko kuwa analytical.
  Matatizo uliyoyagusia ni symptoms za tatizo lenyewe.Macho yakigubikwa na unazi, si rahisi kuchambua mambo,au kama blogu inavyosema Great Thinking.
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Lole
  Binafsi sidhani Madudu ya ccm au mtokeo yakutia moyo ya CHADEMA yaliyojitokeza kwenye uchguzi ulioisha yanatokana moja kwa moja na Utendaji mbovu wa Wana CCM walioko CCM

  Matokeo mabovu yaliyotokea ni matunda Utendaji wa kisanii wa wana CCM walioko serikalini. JK ambaye ni mwenyekiti mwenyewe ndiye wa kubeba lawama. Hata Philip mangula angekuwa ni katibu mkuu bado kwa sanaa za JK matokeo yasingekuwa tofauti. CCM ina loose touch na wananchi sababu invyoshughulikia UFISADI.

  JK badala ya kuweka watu makini wa kufukia weakness zake anaweka watu wenye weakness kama zake.

  So to me Makamaba has nothing to do with this years election result. Inawezekana kweli Makamba sio strategist sasa waht abaou JK. what abaout washauir wake aliowaweka karibu.???!!

  Otherwise kama nikikubaliana na kichwa cha habri yako basi naongeza maneno machache
  Re: Luteni Makamba:Kaburi la CCMn na JK ni Jeneza
   
 14. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu naona wewe uelewa wako wa masuala haya mi finyu.
  A Platoon is the smallest military unit led by a commisioned officer,a leutenant.Idadi ya askari katika
  platpon inategemea division ya jeshi na aina ya mashambulizi.
  Lwa vyovyote vile luteni ni cheo cha pili toka mwisho katika majeshi.
  Naamini mkuu hujapitia ingaau JKT kukua mambo haya.
  Kuongeza uelewa wako pitia Wikipedia.
   
 15. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamani na kacheo ka kopro na staff sajenti katakuwa wapi? Au ndo sawa na makuruta????
   
 16. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi mzee ana level gani ya elimu? I know he used to be a primary teacher back 20 years, sasa sijui alijiendeleza kielimu au la?
  Kama kuna mwenye CV ya dingi aiweke jamvini? I think dogo wa Bumbuli could be of assistance.
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  CCM ilipofika sasa hakuna jinsi, ni kubadilika. Baadae itakuwa ngumu kwao kushika dola hata kwa mtutu wa bunduki. Times change! Kwanini CCM haioni sababu ya kuachana na makada wasio na mvuto ili kuendelea kushika dola?????
   
 18. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Bora umeuliza swali Zuri maana kuna vyeo Vingi sana hapo kwenye kufika cheo cha Uluteni sasa bwana Lole ebu tuambie hao wengine wapo wapi?
   
 19. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Makamba mnamuonea, ukweli mnao wenyewe kiazi ni mkubwa wetu wa pango. Poleni sana wana harakati
   
 20. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Sema Baba seeemaaaaaa
   
Loading...