Lusinde: Wabunge wa CHADEMA wananituma niwasemee - Mbowe ni dikteta anawapelekesha

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253


Muheshimiwa Lusinde anadai kuwa Mbowe ni dikteta kwa sababu anawatoa wabunge bungeni kwa kuwaweka kwenye chai.

Ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa wabunge wa upinzani ndo wamemtuma awasemee kuhusu huo udikteta wa mwenyekiti mbowe.

Lusinde anadai Mbowe hana uongozi bora wowote, hayo ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.

Kuhusu kiinua mgongo kukatwa kodi

Muheshimiwa Lusinde anadai amejitoa muhanga katika suala hilo na kwamba anaafiki suala la kukatwa posho, anawahimiza wabunge wakae na serikali pamoja wakubaliane utaratibu gani utumike.

My Take: Je Mh Lusinde amekubali suala la kiinua mgongo kukatwa kodi kishingo upande ili kupunguza presha yetu sisi wananchi?
 


Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde amesema moja ya viongozi madikteta nchini ni mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kwa kuwa anawapelekesha wabunge wa CHADEMA na kuwalazimisha kutoka nje na wabunge hao wamemtuma awasemee bungeni kwa kuwa wao hawawezi kumwambia
 


Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde amesema moja ya viongozi madikteta nchini ni mwenyekiti wa Chadema Freeman Lusinde kwa kuwa anawapelekesha wabunge wa CHADEMA na kuwalazimisha kutoka nje na wabunge hao wamemtuma awasemee bungeni kwa kuwa wao hawawezi kumwambia

Hivi naye lusinde alichaguliwa kuwa mbunge kweli inabidi baadhi ya watanzania tukapime akili zetu kama ziko sawa,kuna pacha wake wa ulanga huyo ndio ana MB1 kichwani
 
HAPA NI KAZI TU. Speed ya Magufuli ni balaa. Hakuna mpinzani hata mmoja anayeiweza, na ndiyo maana utakuta wapinzani hawana hoja ya msingi hata moja.
 
Mbunge wa Kilwa kusini mh.Selemani J.Bungara (bwege) Cuf hajachagia jambo lolote tangu aingie bungeni,Lakini najua atakuja huku kwetu Kilwa kwa majigambo makubwa sana
 
Hahaha.....jamaa atakuwa amewamisi tu wabunge wa upinzani na hasa kurushiana madongo(Vijembe) kwahiyo anaona bunge limepoa alafu hakuna Mbuge wa upinzani wa kuweza kujibizana naye.Akicheki Kulia anamwona ndassa,mbele Dr Tulia,Kushoto Zungu,nyuma anamwona Shonza
 
Huku kukurupuka kwengine! Toka lini Mbunge wa CCM kumpendelea wa upinzani! Kama wameshindwa kujadili bajeti si waseme tu kua wanawahitaji wapinzani bungeni! Hizi njia za mkato hazitowasaidia kitu. Au wanaogopa kutumbuliwa!
 
Inafaa ajitokeze mtaalamu aandike thesis kuhusu umuhomu wa aina mbalambali ya michango ya wabunge kwa kuchambua taarifa za HANSARD!
 
Hivi naye lusinde alichaguliwa kuwa mbunge kweli inabidi baadhi ya watanzania tukapime akili zetu kama ziko sawa,kuna pacha wake wa ulanga huyo ndio ana MB1 kichwani

Hehehe bora huyo, mi namshangaa aliyempeleka Agness Marwa bungeni, ana kama 2KB hivi.
 
Back
Top Bottom