Lusinde ndani ya TB-CCM

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Mbunge wa Mtera mheshimiwa Lusinde Livingstone aka Kudadeki yuko Tb ccm kwenye kipindi cha jambo leo akiwa na Mrema wakijadili ubadhirifu wa fedha za serikali za mitaa.
 
Livingstone Lusinde, yule mbunge wa Mtera mtaalamu wa Matusi yuko Live TBC1 kwenye kipindi cha jambo. Anasema Wabunge inabidi wachukue hatua kuwawajibisha baadhi ya watendaji wa serikali sababu serikali imeshindwa kufanya hivyo. Anasema inawezekana mtandao wa wizi unawahusisha baadhi ya vigogo wa serikali ndio maana serikali inashindwa kuwawajibisha. Anasema safari hii wananchi watarajie kuona bunge likiwashughulikia watumishi wezi!
 
ni vyema akatumia lugha yake ya matusi ndo itakuwa bora ... watoeni watoto wasiangalie luninga
 
Hii ni TV ya Chama cha Magamba (CCM) kwa hiyo haishangazi! Labda ameamua kukitumia chombo chao kuwaomba radhi waTZ kwa matusi aliyoyatoa. Labda waTz watamsamehe lakini kusahau ng'o! Endelea kutujuza anachosema huyu kibajaji (kilichojaa matusi) kwani wengine hatuna access kwa runinga huku shamba.
 
Mmmh nimempigia simu mke wangu nyumbani awatoe watoto sebleni au asiweke TBC mpaka ili kunusuru familia yangu na lugha chafu akimaliza mniambie wanangu warudi sebleni.
 
Jamaa anasema ana uhakika huko serikalini kuna watu wezi, anasisitiza mawaziri wawajibike, anasema muda wwa maneno maneno umekwisha kwa sababu serikali imekua na porojo kwa muda mrefu, sasa lazima kazi ionekane, katoa mfano kwamba katika viongozi, ni yupi ambaye angekua na kampuni binafsi afu ikawa inapata hasara na yeye akakaa kimya?

This is a totally different Lusinde. . . Siamini ninachokiona na kukusikia, kweli siasa mchezo mchafu.

My Take: (hii ni kipande kutoka hotuba ya bwana Livingstone)
mnakuja mnadanganywa hapa eti ooh chadema, sijui ooh nasari ataleta ajira na soko, ajira atazitoa wapi? Watu hawana shukrani anasimama hapa dk slaa anatukana ccm, hawajafanya kitu, hawajafanya kitu, shule alizosoma yeye zimejengwa na baba yake? shule zimejengwa na serikali ya chama cha mapinduzi, watu wanajiita wamesoma chuo kikuu (chuo hicho) kimejengwa na serikali ya chama cha mapinduzi, nionesheni hapa chuo walichojenga CDM. . . hakunaaa!
 
Lusinde amebadilika bana, inaonesha ameishasoma alama za nyakati vizuri. Anasema haiwezekani mtoto amekosa dawati na kukaa chini miaka 7 akitegemea atakutana na dawati sekondari lakini anakuta hali hiyohiyo huku fedha za madawati zinaliwa na wajanja. Pia amewalipua wanaopeana ajira kindugu baba alikuwa kiongozi anataka na mwanye awe kiongozi...

MY TAKE: Huyu jamaa ameanza kujirekebisha, Le Mutuz hata Mtera kuipata itakuwa ngumu kwa kweli
 
Ametamani naye kutoka bungeni eti waziri akisoma upuuzi ccm watoke wamwache waziri huyo bungeni
 
Lusinde kigeugeu! Arumeru alisema si vibaya mbunge kufa akarithiwa na mwanae kwani kuna madaktari ambao wazazi wao ni madaktari nk. Leo analalamika kuwa kazi serikali zinatolewa kwa kubebana, zinatolewa kiundugu na mdio maana hakuna wa kumwajibisha mwenzie! Viongozi wanafanya kazi ya kuwalinda ndugu zao waliowapa kazi! Sasa msimamo halisi wa Lusinde ni upi? Au ndio zile waziri mkuu anazoziita "unfortunate statements?"
 
Mbunge wa Mtera mheshimiwa Lusinde Livingstone aka Kudadeki yuko Tb ccm kwenye kipindi cha jambo leo akiwa na Mrema wakijadili ubadhirifu wa fedha za serikali za mitaa.

Hukuwa na haja ya kumwita mheshimiwa, hana heshima ya kupewa title hiyo......
 
Back
Top Bottom