Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,216
- 113,510
Basi bana....naona hatuelewani hapa. Wikendi njema...
Mwanakiji kiboko,amembadilisha Dua dakika moja tuu mpaka dua katoa thanks bila kujua..keep it up bro lakini hapa bado!
Dua, majaribio yanayofanywa yalifanywa na baadhi ya waandishi waliopinga sera zake za kijamaa. There have been this attempt of dictatorization of Mwalimu!
a. Katika utawala wa Mwalimu kuna watu waliwekwa kizuizini kama watu wanavyowekwa kizuizini sehemu mbalimbali duniani na hawafunguliwi mashtaka. Na niyeye aliyeleta mabadiliko baadaye ya sheria ya kuwaweka watu kizuizini (prevention and detention act). Nchi yetu ilirithi kwa kiasi kikubwa sheria ya kikoloni na kwa muda tulienda nayo hivyo hivyo hasa baada ya kugoma kwa jeshi in 1964 ambapo Mwalimu alitambua kuwa siyo wote weusi ni wazalendo na siyo wote wanaosimama kuapa wana maslahi ya TAifa.
b. Rais Nyerere alitumia uwezo wake wa kisheria, uwezo ambao hata Kikwete leo anao na anaweza kuutumia akitaka. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuonesha kuwa Mwalimu alifanya jambo ambalo halikuwa ndani ya uwezo wake kisheria. Kama kuna wakati ambapo Mwalimu angetaka kuonesha ukiukaji wake wa sheria ni wakati wa kesi ya Uhaini. Leo hii wale wajemaa wangepigwa risasi na kuambiwa ni majambazi.
c. Siwezi kushangaa kuna watu ambao hadi leo hatujapewa maelezo nini kiliwapata. Mwalimu hayupo hai sasa na kama kuna watu wanatakiwa maelezo yao tunao viongozi ambao wanaweza kuruhusu historia yetu iangaliwe kwa karibu na iandikwe sawasawa. Kama Vaticani inaruhusu watu wapitie rekodi ya Papa Pius, nina uhakika kama kuna rekodi ya Mwalimu isiyo sahihi yenye utata inaweza kuchunguzwa.
d. Mzee Geeque, ni watu wangapi waliwekwa vizuizini wakati wa Mwalimu na kwa makosa gani. Tanzania ipo sheria ya Prevention and Detention Act ambayo bado inafanya kazi. Asikudanganye mtu hata Marekani sheria kama hiyo ipo, Uingereza wanayo na serikali nyingi zinazo uwezo huo duniani wa kuweza kumtia mtu kizuizini kwa muda fulani na kumuachia bila kumfikisha mahakamani. Zinatumika sana wakati wa maandamano au vurugu. Miye naomba nitajiwe mtanzania mmoja ambaye alikamatwa akatiwa kizuizini na hakufikishwa mahakamani. Inawezekana wapo lakini haiwezi kuwa kama ulivyosema. Hivi mzee mwenzangu umejuaje watu wengi waliwekwa kizuini bila kufikishwa mahakamani zaidi wakati wa Nyerere kuliko wakati wa marais wengine? Na mzee Geeque, Mwalimu alitumia dola vipi kuwadhibiti waliompinga. Mtei yupo. Babu karudi na kafia TAnzania, Kambona karudi na kafia Tanzania, Fundikira kaishi na kafia TAnzania na orodha goes on and on. Lakini msifanye makosa endapo kuna Mtanzania yeyote anafikiria uhaini ajue kabisa kuwa hakuna demokrasia au utawala bora utakaomuokoa. Hilo ni kosa kubwa katika jamhuri yetu. Wamerekani walishanyonga watu in the fifties kwa makosa ya Uhaini! Hata leo hii ukikutwa na hatia ya Uhaini umekwisha; ndio maana wale ndugu zetu wa Zanzibar waliodaiwa kufanya uhaini Zanzibar waliachiwa na Mahakama!
e. Katika utawala wake wa miaka 25 Mwalimu alitia sahihi hati mbili tu za kuruhusu waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe. Yule aliyemuua Dr. Kleruu na mtu mwingine (sikumbuki moja kwa moja). Wakati wa utawala wa Mwinyi watu walikuwa wanapukutika kama njugu (nilipata nafasi ya kushuhudia akinyongwa mtu pale Butimba) in early 90s. Dikteta au kiongozi mwenye nguvu kama Mwalimu angewapukutisha waliompinga. Naomba mnishawishi wazee wenzangu kuwa Mwalimu alikuwa borderline dictator au ametumia madaraka asiyokuwa nayo.
Najua kuna watu ambao hawajamuelewa Mwalimu na hawataki kumuelewa Mwalimu. Madai mengi yanayotolewa dhidi ya Mwalimu hayana msingi katika ukweli ni fiction. Ndiyo maana alipokufa kuna waandishi wa habari wa Kimataifa waliripoti "The TAnzanian Dictator Died".. halafu wakashangaa mbona watu hawaruki ruki na kushangilia?.. Friends Mwalimu was a human being na alifanya makosa na yeye mwenyewe alikiri makosa (sikiliza hotuba yake ya Mei Mosi 1995) but he was not the terrible man and benevolent dictator some people are trying to potray him. No sir, he was not.
mzee ushawahi kusikia "self imposed exile"... ? Mambo yanaweza kumuendea vibaya akaamua kukimbilia nje ya nchi.. akajiita mkimbizi..
Wale ambao hawakukubaliana na Mwalimu waligonga mwamba kweli kweli...
Hatufahamu kwa undani Mwalimu alitofautiana nini na Kambona. Hatuwezi kuwauliza kwani hawapo tena nasi. Inasemekana tofauti zao zilihusu Azimio la Arusha. Ilikuwa haikubaliki hata kidogo kutofauitiana na Mwalimu kwenye mambo ya msingi.
Tuwe na balance kuhusu Mwalimu. He won some and lost some.
....
But I also feel like there is a need to have an in-depth discussion of where and what he did wrong during his rule. There are a lot of myths and half-truths about him that still dog him to this day and I think it is right about time we get the story straightened out and dispell everything (or try to) that is not true.
Waacheni wafu wapumzike! Tangu aachie madaraka ni miaka 22 na sioni chochote kilichoongezeka cha maana ndio kwanza skendo zinazidi!