Lundenga wewe ni mwenyekiti wa maisha?

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Wadau wa Urembo

Kwanza mi sina ufahanu zaidi juu ya masuala ya urembo pamoja na kamati hii ya Miss Tanzania, tatizo langu ni tangu nianze kusikia urembo nchini hili jina la huyu Mzee Lundenga lipo kila siku, hivi huwa anachaguliwa au ndiyo mwenyekiti wa maisha?

Ukisikia Ludenga basi ujue shughuli ya ma miss imeanza, nihabarisheni nijue kama jamaa ni mdau wa urembo na mwenyekiti wa maisha wa Miss Tanzania.

Pia anayejua juu katiba yao atuhabarishe jinsi wanavyochagua viongozi wao, isije watu wakawa wameshafanya Miss Tanzania mradi wao wa kimaisha.
 
Na hata akifariki, hakuna uchaguzi mpaka atakaporudi tena kama Yesu! Jamaa linang'ang'ania wakati hakuna mafanikio yoyote anayoleta zaidi ya kuchagua mamiss kimbinu mwishowe aibu tu. Naichukia Miss Tz kwa ajili tu ya Lundenga na wahindi wake - wezi wakubwa na vibaka wakutupwa
 
kumlaumu lundenga ni awa na kumlaumu kupe au kirusi... yeye ni parasite hivyo ni host ndiye anayetakiwa kuongeza juhudi za kupambana na parasite huyo... binafsi naona miss tz imepoteza mvuto na sifa

he wil remain there as long as mashindano hayana maana, yakipata maana watakua wengine
 
Nimewahi kusikia hii habari kuwa lundenga kupitia kampuni yake wamepewa haki na nani sijui kuandaa mashindano milele, hata serikali haisemikitu wala kuingilia maana jamaa ana haki zote.
mwenye kujua atujuze
 
Wadau wa Urembo

Kwanza mi sina ufahanu zaidi juu ya masuala ya urembo pamoja na kamati hii ya Miss Tanzania, tatizo langu ni tangu nianze kusikia urembo nchini hili jina la huyu Mzee Lundenga lipo kila siku, hivi huwa anachaguliwa au ndiyo mwenyekiti wa maisha?

Ukisikia Ludenga basi ujue shughuli ya ma miss imeanza, nihabarisheni nijue kama jamaa ni mdau wa urembo na mwenyekiti wa maisha wa Miss Tanzania.

Pia anayejua juu katiba yao atuhabarishe jinsi wanavyochagua viongozi wao, isije watu wakawa wameshafanya Miss Tanzania mradi wao wa kimaisha.

Hoja unayoitoa hapa ni sawasawa na kusema ni lini Regnald mengi atajiuzulu kuendesha ITV ili waiendeshe wengine.Lundenga hakuteuliwa na serikali kuendesh a miss Tanzania ila ni yeye mwenyewe kupitia kampuni yake ya Lino agent aliomba kibali cha kuandaa miss Tanzania kutoka kwa waandaaji wa miss world.Hivyo hawezi kuacha kuandaa labda atake mwenyewe kuacha au miss world wenyewe waamue kumtosa lakini si serikali wala mtu yeyote anaweza kumzuia kuandaa miss Tanzania.
 
Dah! toka nimepata akili ya kujua kuna mambo ya umiss huyu mzee namsikia kama mwenye chair!labda kweli ni wa maisha mpaka Masiha arudi,,,lol
 
I have a feeling anaweza akaenda mbali na kumrithisha mkewe miss aliyemuoa au mtoto wake lets wait and see
 
jana himeona interview yake kwenye Monday Agenda ya Capital TV, kwa kweli ilinikera sana sana maana jinsi anavyojibu maswali, unafahamu kabisa jamaa hajui kitu kuhusu kwanza anachokifanya (Miss TZ) na pili anachokiongea.
Nadhani ameanzisha ili kuadhalilisha dada zetu tu, sio kuwasaidia au kuitangaza TZ yetu na utamduni wake.
 
Hatimiliki ya Miss Tanzania iko kwa lundenga.Labda yeye mwenyewe amuue kuuuza. Ndio maana wengine wamejitahidi kuanzisha mashindano mengine lakini hii Miss inayobeba jina la nchi jamaa ni kampuni yake.
 
Ndio sehemu yake ya kula hapo unadhani atakula wapi pengine zaidi ya hapo

hili ni jambo linahusu jamii moja moja na kuna wizara inayohusika na jambo hili sijui inaliongelea vipi? kampuni moja kujipatia hati miliki ya ma miss ni hatari sana, ni rahisi rushwa kujipenyeza sababu inajulikana next year Mzee Ludenga na kamati anayoitaka yeye na majaji anaowataka yeye ndiyo watakuwa hapo jukwaani kuamua. sasa ukiangalia na huu umri wa hawa watoto, sorry nawaita watoto sababu ndiyo kwanza wanaumaliza utoto utoto (18 -22) wanahitaji uangalizi mkubwa sana, so rushwa za kila aina zinaweza kutumika ili mrembo asonge mbele, au kupanga matokeo kabla ya panel ya mwisho.

Haya ndiyo baadhi ya mambo ambayo tunasema serikali lazima iingile kati, anyway sishangai maana serikali yetu kama mnavyoijua. kula kwa urefu kwa kamba yako

Binafsi huyu mzee hana mvuto atoke waje wengine tuone wanakuja na mikakati ipi.
 
I have a feeling anaweza akaenda mbali na kumrithisha mkewe miss aliyemuoa au mtoto wake lets wait and see

Nchi hii kila mtu anashika ka kitengo kake anapata pa kula sasa nimebakia mimi sijui nishike wapi maskini yarabi..
 
Kama una kipaji cha kuongea anzisha kanisa au msikiti au ingia kwenye siasa!!

Ukishindwa andaa fiesta kama Joseph Kusaga na Ruge au Serebuka ama hata mashindano ya Bongo Star Search!!

Kwa taarifa yako mdogo wa Lundenga alipoona kaka yake (Lundenga) anakula hela za bure za sponsors, gate fees pamoja na license fees kwa ku waandaaji wa mikoa na kanda naye akaamua kuanzisha mashindano yake ya Miss Utalii. Mdogo huyo wa Lundenga anaitwa Mr. Chipungaelo almaarufu kama Mr. Chips!! Huyu mwaka juzi aliandaa mashindano ya Miss tourism world pale Ubungo Plaza na mgeni rasmi alikuwa first lady Salma Kikwete!!
 
hii maada imekaa njema, sasa mimi naomba pia nijuzwe kama watu wa mamlaka ya kodi na mapato TRA huwa wanawatoza kodi hawa jamaa, maana viingilio vya kuanzia laki (100,000/=) ni hela nyingi sana ukiangalia mahudhurio yenyewe, pia hawa jamaa wanaoandaa fiesta vipi mbona huwa hawatangazi mapato yao kama wanavyofanya TFF? pindi michezo au matamasha yanapokuwa yamemalizika?
 
Back
Top Bottom