Lulu: Mimi sina Jini mauti Jamani

Lulu: Mimi sina Jini mauti Jamani

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,213
Reaction score
18,455
MSANII nyota wa filamu, Elizabeth Michael ` Lulu ' amekanusha uvumi kuwa matatizo yanayowatokea wanaume aliowahi kuwa nao yanatokana na yeye kuwa na Jini Mauti anayesababisha hali hiyo kutokea, Amani linakujuza.

Akizungumza na gazeti hili juu ya madai ya wadau mbalimbali kuhusiana na matukio mengi yanayomtokea , muigizaji huyo wa filamu ya Foolish Age , alisema maisha yake ya siku hizi ni ya kusali sana , hivyo anaamini kutokana na maombi yake , hali yake iko vizuri kutokana na Mungu kumpa anachokihitaji .

"Ninasali sana kwa sasa aisee, mara nyingi nafanya hivyo mara tatu kwa siku , ninao uwezo wa kukemea mapepo na yakaondoka , hayawezi kukaa mwilini mwangu , " alisema muigizaji huyo ambaye miaka michache iliyopita , aliondokewa na mpenzi wake , Steven Kanumba aliyeanguka na kufariki mbele yake .

Mtabiri mmoja maarufu jijini Dar es Salaam , Maalim Hassan Yahya Hussein, alisema tatizo kubwa linalomsumbua binti huyo ni jini mauti ambalo baada ya kumpenda, halitaki kuridhia uhusiano wake wa kimapenzi na binadamu.

" Hapa nimshauri tu, achukue hatua ya matibabu haraka iwezekanavyo vinginevyo hali hiyo itaendelea , anatakiwa afanye kafara kwa kuchinja mnyama yoyote ili aondokane na matatizo haya, " alisema .

Chanzo: GlobalPublishers
 
Attachments

  • 1431000283460.jpg
    1431000283460.jpg
    32.4 KB · Views: 3,490
insta yake bado anaiendesha binamu......

huyo mtabiiri akajambe mbele
 
Hhhhhaaaaaaaaaaa hiyo cheni aliyovaa si na husna maulid anayo kwa hiyo wote walipewa za kufananaa zenye madini
 
Hhhhhaaaaaaaaaaa hiyo cheni aliyovaa si na husna maulid anayo kwa hiyo wote walipewa za kufananaa zenye madini

Hata mimi nimejiuliza kuhusu hiyo cheni.
Naona jamaa alikua anahonga tanzanite hatareee.
Ila Husna anayo na pete yake pia.
 
Hata mimi nimejiuliza kuhusu hiyo cheni.
Naona jamaa alikua anahonga tanzanite hatareee.
Ila Husna anayo na pete yake pia.

Ndio hivyo walipewa sare sareee,
 
Hhhhhaaaaaaaaaaa hiyo cheni aliyovaa si na husna maulid anayo kwa hiyo wote walipewa za kufananaa zenye madini

Marehemu alikuwa kiboko,ivi husna na Lulu nani mzuri binamu
 
Hata mimi nimejiuliza kuhusu hiyo cheni.
Naona jamaa alikua anahonga tanzanite hatareee.
Ila Husna anayo na pete yake pia.

Makamanda zangu katika ubora wenu.
 
Ndio hivyo walipewa sare sareee,

Kanumba nae aliwahi kumnunulia Lulu perfume kumbe alimnunulia pia demu mwingine, yan wakipewa vijizawadi wanajiona keki kumbe wenzao wanagawa kama pipi kwa kila mtu
 
kusali mchezoo..

Si aliokokaga kipindi cha kanumba? Na kwaya akawa anaimba kwa zamaradi mmh baadae dunia ikawa tamu akasahau ata nyimbo za dini kutwa akawa anaimba nyimbo za ajabu uko insta, sasa iv tena majanga
 
Si aliokokaga kipindi cha kanumba? Na kwaya akawa anaimba kwa zamaradi mmh baadae dunia ikawa tamu akasahau ata nyimbo za dini kutwa akawa anaimba nyimbo za ajabu uko insta, sasa iv tena majanga

Wa kusali atakua yeyee (masanja's voice

malaya tu yuko sokoni
na nyie w anaume wapenda maarufu mtakuf a sana tuu
 
Back
Top Bottom