Lukuvi DOWANS ni "petty issue".......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi DOWANS ni "petty issue"..........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 29, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,895
  Likes Received: 416,603
  Trophy Points: 280
  ‘CCM kinapitia wakati mgumu’
  Saturday, 29 January 2011 08:33

  Elias Msuya na Fredy Azzah

  KIKIWA kinatimiza miaka 34 tangu kuzaliwa kwake Februari 5, 1977, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelezewa kuwa, ingawa kimeendelea kushinda nafasi ya urais nchini, kinakabiliwa na wakati mgumu.

  Wakizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, wabunge wa CCM walisema chama hicho hakiwezi kufa kwa sasa, lakini kinapitia tu wakati mgumu kama ilivyo kwa vyama vingine duniani.

  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, alisema kwa kipindi cha miaka 34 ambacho CCM imekuwa madarakani, kimefanikiwa kufikia malengo yake hasa kwa kushinda chaguzi zote.


  “Chama chochote kile duniani, malengo yake ni kushika dola. Kwa kipindi chote CCM tumefanikiwa kushika dola. Hata kwenye michezo, kama timu inashuka daraja mwenye timu huivunja,” alisema Lukuvi.

  “Chama cha siasa ni taasisi endelevu, sio kwamba tumeongoza kwa maziwa na asali. Tunapitia kwenye milima, misitu na vichaka.

  Ni jukumu letu kujitambua ili tuendelee kushika dola,” alisema. Kuhusu suala la Dowans ambalo limeonekana kukigawa chama hicho kabla ya wabunge wake kukutana na kuweka msimamo wa pamoja, Lukuvi alisema hilo haliwezi kukigawa chama.“Chama hakiwezi kugawanyika kwa ‘petty issues’ (mambo madogo madogo).

  Chama kupitia mwenyekiti wetu alishasema jambo hilo sio kubwa. Ni uhuru wa maoni tu, kama ni mawaziri kupingana watakuwa wamevunja kanuni zao, sio chama,” alisema.

  Naye Mbunge wa Uzini, Muhammed Seif Khatib, alisema sio kwamba CCM imepoteza mwelekeo, bali kinakwenda kulingana wakati ulivyo.

  “Sioni kama chama kimepoteza mwelekeo, kinakwenda kulingana na wakati, dunia imebadilika, mahitaji yameongezeka, vionjo vimeongezeka kwa hiyo chama kinakumbana na mazingira ya wakati huu,” alisema. Alikitetea chama hicho kuwa, hakiwezi kuleta pepo duniani na kwamba, matatizo yapo duniani kote sio Tanzania pekee.

  Kuhusu suala la Dowans, Khatibu alisema kilichotokea ni uhuru wa maoni sio kugawanyika kwa chama. Naye Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Stella Manyanya, alisema kwa kipindi cha miaka 34, chama hicho kimefanya mambo mengi mazuri ambayo yameifikisha nchi hapa ilipo, na bado kina uwezo wa kuongoza miaka mingi ijayo.

  Hata hivyo, Manyanya alisema changamoto anayaoiona ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi, ni suala la mawasiliano.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,895
  Likes Received: 416,603
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Ni jukumu letu kujitambua ili tuendelee kushika dola," alisema. Kuhusu suala la Dowans ambalo limeonekana kukigawa chama hicho kabla ya wabunge wake kukutana na kuweka msimamo wa pamoja, Lukuvi alisema hilo haliwezi kukigawa chama."Chama hakiwezi kugawanyika kwa ‘petty issues' (mambo madogo madogo). 
  Yaani huyu Lukuvi kwa kuita DOWANS ni suala dogo...............................inanithibitishia ya kuwa amelewa madaraka.................Haiwezekani bilioni 94 zikawa "petty issue".................................the man must be living in "wonderland"....................
   
 3. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  mgawanyiko CCM upo na haukwepeki..... it is a time bomb.... hata mwalimu nyerere alishauona na alishauri sisiem imegeke ili iwe na vyama viwili....enzi za G 55..... mrema akapewa dili akakurupuka halafu ikashindikana..... sasa imebakia muda mfupi tu utaniambia
   
 4. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  "Dowan ni petty issue" I like that one. Si Lukuvi kama ana haya mabillioni atulipie basi kama ni petty issue??
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Siku hizi Lukuvu Ticha wa primary anabonga English.

  Suala la Mabillioni ya fedha kuilipa Dowans analiita "Petty Issue "

  Yale yale ya Vijisenti!!!

  Lukuvi anaujasiri wa kuita suala la Dowans Petty Issue??

  Kweli CCM wamelewa Fedha za wizi na madaraka
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Matatizo yapo Duniani ni kweli lakini sio mgawo wa umeme usiokuwa na mwisho,wanafunzi kukaa chini wakati waziri anatembelea gari la milioni 150,mishahara kiduchu na hailipwi kwa wakati,barabara mbovu na nyingi zinajengwa chini ya kiwango,vituo vya afya dawa hamna..,wamelewa madaraka kiasi kwamba wanashindwa kuona ukweli kwamba wamefeli kwa kiasi gani...!
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Hiyo yenye nyekundu inawezekana ni kauli ya kijinga kabisa. Kushinda uchaguzi halafu kiwe nini? Yaani chama kikae tu kula na kuiba pesa za watanzania na sio kufanya kazi kuifanya Tanzania iwe nzuri zaidi? ushindi maana yake nini kwa CCM? NI bora kama watu hawawezi kuongea wakae kimya, kuliko kuongea pumba!!
   
 8. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  alibaba...Rostam Aziz

  and

  forty thieves....William Lukuvi.., Nazir Karamagi....
   
 9. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du km Petty Issue walipe basi! Dowans hizo 94bn watakiona cha moto kinachompata Mubarak huko Misri au Tunis, Tunisia Baraza lote halitakiwi
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Hivi hizi kauli za wana CCM ni dharau kwa Watanzania ama
  Chenge = Visent
  Kombani= nilkuwa napima Upepo
  Warema = Hayo ni mawazo/maneno yangu binafsi
  Lukuvi= Petty Issue
  Mary = Askofu wavue majoho

  ni balaa kabisa
   
Loading...