Luku mlimani city kuanzia elfu kumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Luku mlimani city kuanzia elfu kumi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sikiolakufa, Apr 29, 2011.

 1. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu mbona kila nikienda mlimani city kununua umeme nikiwa na shilingi zangu elf nne wananiambia wanauza kuanzia elf 10 hii ni sawa? Kwa nini tanesco inatubagua sisi wananchi wa kipato cha chini? Au hayo ni majivuno ya hao wauzaji wa luku hapo kuna dada mmoja anaitwa hapiness mrema yeye hana matatizo ila yule mwingine mweusi sijui mhaya....kaaazi kweli kweli
   
 2. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Anajua hutapata unit. Hiyo elfu nne ni makato tu. Sasa akichukua atakupa nini?
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  hahaha,hata vocha za jiti tatu hakuna pale.hakuna utalii,wanalipa kodi banaa.njoo huku kwetu,luku ya buku kwa raha zako
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Nini mlimani city? Nilipokuwa Arusha wananchi walitangaziwa kabisa kuwa hakuna LUKU chini ya 10,000
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Umeme wa buku 4 utapata units ngapi?

  By the way, umejuaje majina ya wauza LUKU?

  Halafu, kama unazo buku nne unaenda Mlimani City kutafuta nini? Kwa nini usiende Mwananyamala Komakoma kununua LUKU? Maana ndiyo "size yako"!
   
 6. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jamani acheni kumuonea..hiyo buku nne sio hela ndogo, basi wangeweka mabango kabisa kutuambia ni watu wa aina gani wanatakiwa kuingia pale, mambo yanayohusiana na basic needs and other social services bei inatakiwa iwe sawa kwa wote! tatizo ukweli tunaukimbia na kuona ni kawaida
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  khaaaa!
   
 8. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Da, asante kwa kunijuza maana nipo njian naelekea huko m/city na Tsh.2000/- zangu.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  sasa asiambiwe?anaenda kuongeza foleni tu!shoprite hapaingiliki siku hizi manake foleni imejaa kila mtalii kabeba mkate au chocolate moja.samahani kama nimekukwaza,ila sinza na mwanayamala hakuna soo.mi mwisho wa mwezi ndo natia jeuri mlimani city!
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
   
 10. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyinyi ndio mtaimaliza nchi hii na ukabila.Acha ufinyu wa mawazo.Pata uhakika kwanza ndipo uje na shutuma za kikabila kama hizo manake umeshaanza na sijui......,ina maana huna uhakika wewe.
   
 11. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu asanteni kwa maoni yenu, mimi ni mkazi wa sinza nilinunua nyumba mwaka 2000 kwa hiyo mimi ni mkazi wa sinza A kitalu number 238 karibu kabisa na Mlimani city....kulingana na kipato changu umeme wa elf nne huwa napata unit 16 ambazo huwa zinakaa siku mbili tatu maana natumia taa radio na tv tu....sasa huyo anayeniambia niende mwananyamala nikafanye nini wakati mimi ni mkazi halali wa sinza.....kwa nini tanesco waweke kiwango cha chini cha kununua umeme sh 2000 wakati wakijua hayo ni makato? na huyo anayeuliza mimi nilijuaje majina ya wauzaji hivi hajui kusoma kila ukinunua umeme jina la mtu aliyekuuzia linakuwa chini pale ya karatasi ile....au ananunua umeme kwa Mpesa nini? mimi nilileta hii hoja kwa makusudi maana watu wengi wananyanyaswa na wahudumu wasio na maadili ya kazi....mnajifanya mna uchungu na nchi hii kumbe mnaangalia mambo ya siasa tu wala hamuangalii mwananchi wa kawaida anavyo nyanyasika kwenye nchi yake.......mnakuwa kama EL...bwana
   
 12. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 407
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mimi nakaushauri ujiunge na hizi huduma za M-pesa, Zap na siku hizi Tigo pesa, hata elfu mbili unanunua, hupotezi muda wala hukereki
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,592
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Pia ATM za Baadhi ya mabenki kiwango cha chni ni 10,000/= kwanini hili? au nalo ni makato?
   
 14. x

  xman Senior Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani kuhusu luku hapo mlimani city wamemwonea tu kwa kumwambia hawauzi chini ya 10000, Tanesco hawana makosa yoyote maana wao hawajaset kiwango cha chini,kiwango cha chini kinakuwa determined na makato ambayo yanaendana na hiyo huduma e.g tax,service charge n.k,so muuzaji usika ndio anaamua aanze kuuza kuanzia kiasi gani, ni sawa na mtu anavyoamua kuuza vocha za sh. 5000 tu na kwenda juu. alafu wewe kwani sinza nzima lazima ununue lmimani city tu
   
Loading...