Luhwavi, Membe na Lukuvi, mnayopanga Gizani ili Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM yawekwa Hadharani

Lizaboni unajiamini sana. Ukiona panya anamchokoza paka,shimo liko nyuma yake. Hayo uliyopost yalishasemwa na mzee wa Kanisa la Ufufuo,Baba Askofu Gwajima,akaishia kutafutwa na wazee wa kazi/kuhojiwa,walikesha kwenye makazi yake,wewe unajiamini nini? Membe ni kachero mwandamizi, hiyo shughuli hakuna kustaafu. Nasubiri miezi 3 kama ID hii Lizaboni itakuwepo.
Dah! Humjui Lizaboni wewe
 
Walioshindwa hawataki kuamini kuwa wameshindwa. Kuna watu wanajiona kuwa wana hati miliki ndani ya ccm

Ndio maana wanataka wapigiwe kura ya ndio tu, watu wakitaka kupiga ya hapana wanatoka povu, kwani kuna ubaya gani hao akina lukuvi kumobilize makada wapige kura ya hapana?! nawe kama unaona anafaa hamasisha wajumbe wapige ndiyo kuliko kuja hapa kuanza kuwachafua wenye mawazo kinzani na nyie wazee wa ndiyooo.
 
Huyu Lizaboni kacharuka sana wiki mbili tatu hizi anaweweseka sana ni kama mtu mwenye presha anaehofia kukosa kitu flani hivi
 
Huyu Lizaboni kacharuka sana wiki mbili tatu hizi anaweweseka sana ni kama mtu mwenye presha anaehofia kukosa kitu flani hivi
Siku zote nipo hivi Mkuu. Labda wewe ni mgeni hapa JF
 
Umeandika hoja nyepesi zilizojaa majungu matupu ! Sema umenifurahisha kwa vile umelenga kuvuruga ccm ama kwa kulipwa au kwa kujitolea .
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimeapa kusema kweli na nitasema kweli daima kwani hii ndio nguzo kuu ya kupambana na maovu yote nchini. Sitasema uongo na daima sitafumbia macho maovu yote yanayotendeka chamani bila kujali yanatendwa na nani.

Mtakumbuka ni hivi juzi tu nimeumbua mkakati wa chini kwa chini unaoratibiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhwavi wa kutaka kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM. Niliahidi kuwa nitaendelea kuwaumbua wale wote wanaoshirikiana na Luhwavi na ambao wana mikakati isiyo ya ushirika lakini dhamira yao ni kuona Magufuli hawi Mwenyekiti wa CCM iwe mwaka 2016 ama 2017. Nimerudi tena kama nilivyowaahidi na sasa ni zamu ya Benard Membe na Wiliam Lukuvi kuumbuka.

A. BENARD MEMBE
Mtakumbuka kuwa kwenye mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, Benard Membe na Edward Lowasa ni makada wawili ambao walitengeneza kambi mbili hasimu. Makada hao wawili kila mmoja alijiona kuwa yeye ndiye mrithi pekee wa Dr Jakaya Kikwete kwenye nafasi ya Urais. Hata hivyo, kwa mapenzi ya Mungu, wote hawakuwa. Lowasa alikatwa mapema kabla hata ya kufika kwenye Tano Bora. Membe alifanikiwa kuingia Tano Bora lakini akashika mkia kwenye mchujo wa kwenda kwenye Tatu Bora ambapo Dr John Pombe Magufuli aliibuka mshindi na ndiye Rais wetu.

Hata hivyo, Lowasa aliamua kutimka chamani na kwenda kugombea CHADEMA ambako aliangukia pua kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015. Hivyo nguvu ya Lowasa ikazikwa rasmi ndani ya CCM. Benard Membe aliamua kubaki chamani kwa matarajio kuwa atapewa nafasi ya uteuzi ikiwemo nafasi ya Waziri Mkuu ambayo angeipata kama angekuwa Mbunge wa Jimbo lakini alishauriwa asigombee ubunge kwa ahadi kuwa angepatiwa nafasi nyingine. Haikuwa hivyo. Membe ana manung'uniko na yupo Bechi asijue hatma ya maisha yake kisiasa.

Kutokana na hali hiyo, Membe ameibuka kuwa na chuki na Rais Magufuli na amekuwa akiratibu na kushiriki mikakati ya chini kwa chini ili Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM akishirikiana kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu Bara Rajab Luhwavi. Kwa nini Membe anafanya hivyo? Nitawaeleza.

1. Chuki na hasira ya kuukosa Urais. Baada ya Lowasa kubwagwa hata kabla ya kuingia kwenye Tano Bora, Membe akajiona ni Rais anayesubiri kuapishwa. Kubwagwa kwa Lowasa kulimfanya Membe ajione ni mshindi. Hata hivyo, kitendo cha mwanasiasa huyo kushindwa kuingia hata kwenye Tatu Bora kulimfanya ahisi kuwa amehujumiwa. Hasira zake alizielekeza kwa Benjamin Mkapa ambaye anasema kuwa ndiye aliyemwaga sumu ili asichaguliwe. Hivyo, Membe akawa na chuki na Mkapa na Rais Magufuli.

2. Kukosa nafasi ya Uteuzi. Membe alijiona kuwa anazo sifa za kiongozi mkubwa wa serikali ya Rais Magufuli. Hivyo kitendo cha Serikali hii kumuacha hata kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hakika anaona kuwa ni dharau kubwa kwake.

3. Serikali ya Awamu ya Tano kushindwa kumsimamia kwenye nafasi za Uongozi wa Jumuiya ya Madola na AU. Membe anadai kuwa kwa uzoefu wake na kufahamika kwake, angefaa kugombea nafasi zilizojitokeza kwenye Jumuiya ya Madola na Umoja wa Afrika kama Serikali yake ingemtia moyo na kuahidi kumpa ushirikiano. Hata hivyo, anaona kuwa Serikali hii haina msaada kwake na anamshutumu Rais kuwa huenda anammaliza kisiasa ili ifikapo mwaka 2020 asiwe na mpinzani ndani ya chama.

4. Kuimarisha Mtandao. Membe anashirikiana na Luhwavi ili kutengeneza mtandao wa uongozi ndani ya chama. Taarifa zilizopo ni kwamba wanataka Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti hadi 2017 na Katibu Mkuu awe Luhwavi ili asaidie kutengeneza mtandao ambao utajenga safu ya uongozi kuanzia ngazi ya taifa hadi kwenye matawi kwenye uchaguzi wa chama utakaofanyika mwaka 2017. Ama ikiwa watashindwa kukwamisha Magufuli asiwe Mwenyekiti hapo Julai 23, watafanya hivyo mwaka 2017 ambapo chama kitafanya uchaguzi katika ngazi zote. Ajenda kuu ni kuhakikisha kuwa nguvu ya Membe inarejea ambayo itamsaidia kumuangusha Rais Magufuli kwenye mchujo wa Mgombea Urais wa CCM, uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo amepanga kugombea.

B. WILLIAM LUKUVI
Huyu naye ana ndoto za kuwa Mwenyekiti wa CCM. Labda nikuulize Lukuvi, je Uenyekiti wa CCM Utauweza? Je wewe ni Presidential Material? Taarifa zilizopo ni kwamba Lukuvi anavizia nafasi ya Uenyekiti wa CCM. Kwa sasa anapima upepo na hasa anaangalia nini kitatokea Julai 23. Kwamba, ikiwa kundi la Wapinzani wa Magufuli litaelekea kushinda, anaamini kuwa anaweza kugombea na kushinda mwaka 2017 kwa vile anaamini kuwa yeyote atakayeshinda nje ya Magufuli Julai 23, atatengeneza ombwe la uongozi ambalo litahitajika kuzibwa mwaka 2017. Lukuvi anaona ni vigumu kwa sasa kumzuia Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti ila anaamini kuwa watafanikiwa kufanya hivyo mwaka 2017. Hivyo mkakati wa Lukuvi ni kwa ajili ya 2017 na si mwaka huu.

Swali la kujiuliza, je mikakati yote hii ni kwa faida ya nani? Kwani hakuna maisha nje ya siasa? Je wanafikiri ni rahisi kumuangusha Rais Magufuli sasa ilhali walishindwa hivyo mwaka 2015? Hakika huku ni kutapatapa. Siasa za mtandao zimeshazikwa Rasmi mwaka 2015 na wana CCM hatupo tayari kuona mitandao inarejea chamani

Wale wote ambao bado hamuamini kuwa Magufuli ndio Rais, mnapaswa kuamini hivyo sasa na ndiye Mwenyekiti wetu wa CCM.
Sorry kama ntakuwa sjaelewa hoja yako vizuri. Mm nadhani kama ni kweli hao wanamkwamisha pombe asichukue uenyekiti , hawakosei wanatumia haki yao kuwa na mtazamo tofauti, kwani nini maana ya demokrasia? wao wanaona hafai basi kura ndo iamue nani awe mwenyekiti . Ndo maana ya democracy
 
Sindano imekuingia. Hiyo ndio tiba yako
Nina mashaka kama una uelewa wa kutosha manake ungekuwa smart enough ungeshagundua kwamba wala sina time na viroja unavyoandika ndo maana vyote navipotezea lakini kwa akili zako wewe unadhani eti unapiga sindano!!

In short unaboa; hizo paranoia zako zilikuwepo hata uchaguzi wa CCM wa 2012 lakini wenye akili zao walijua hapakuwepo na mtu wa kufanya JK asiwe Mwenyekiti na mengine yote wenye akili zao walishajua was just ELECTION fever!

Na hii ya kesho kutwa; narudia, hakuna hujuma zozote dhidi ya JPM ingawaje ni kweli pia wapo wana-CCM wasiotaka JPM apewe chama! Majority ya hawa sio kwamba wana chuki na JPM bali wapo more concerned na chama chenyewe! Hawa wanaamini leadership style ya JPM akiipeleka kwenye chama basi inaweza kuathiri chama!!

Ngoja niseme jambo moja; kwaheri! Wacha niendelee kula bia hapa wakati wewe ukiendelea kupiga kelele zisizo na tija!!! Na msingi wa kelele zako ni MAJUNGU, FITINA NA UCHONGANISHI! Mtoto wa kiume kuishi kwa majungu na fitina haipendezi! Maelezo yako mengi yanajengwa zaidi na hisia!

Ulianza kumfitinisha Rajab Luhwav, ukaja kwa Ally Hapi hadi kufikia kufungua thread inayoashiria kwamba Ally Hapi ndie Egnecious hapa JamiiForums! Kama sio fitina hizi tuite nini? Unaposema Mteule wa Rais anashiriki kumuhujumu Rais unatarajia nini?!

Leo umekuja kumfitinisha Lukuvi na Membe!! Bora huyo Membe manake michezo kama hii keshaizoea! Kesho utasema January Makamba anashiriki kumuhujumu Rais na mtondogoo utadai Mwigulu Nchemba, huku mwenyewe ukijitia eti huwezi kufumbia macho maovu! Mbona hatukuoni ukikemea maovu yanayofanywa na watendaji wa chama chako?

JPM ana Team kubwa sana ya kugundua what's going on kwahiyo haya yako ni makelele tu yasiyo na msaada wowote kwa JPM! Wewe huna ubavu wa kufahamu intel ambayo JPM mwenyewe hana labda kama intel yenyewe ni majungu!! Hutu tuhabari habari twa kuokoteza okoteza kwenye tubaraza twa Lumumba means nothing to JPM but just making noises to JF Members!

KARIBU TUONGEZE DAMU!!!!
 
wasiompenda raisi wetu wawe makini maana kundi la malaika waleteo mabaya wasijekuwa juu ya maisha yao. zaburi 78:49:(
 
Nimesoma mpaka hapo uliposema Membe alitegemea kupewa uwaziri mkuu nikagundua wewe ni mnafiki na muongo wa kutupwa na huenda hata katiba ya nchi huijui. Waziri mkuu ni lazima awe mbunge wa kuchaguliwa jimboni sasa Membe angewezaje kutegemea ateuliwe kuwa waziri mkuu wakati hakugombea ubunge? Baada ya kuona uzushi huu hata sikuendelea kusoma zaidi. Wadanganye wasiojua katiba
Well said , huyu jamaa sometimes anaandika vitu ambavyo ni very poor na havina connections na inaonyesha hata uwezo wake wa kufikiri ni mdogo kabisaaa
 
Nina mashaka kama una uelewa wa kutosha manake ungekuwa smart enough ungeshagundua kwamba wala sina time na viroja unavyoandika ndo maana vyote navipotezea lakini kwa akili zako wewe unadhani eti unapiga sindano!! Hebu wasome walionielewa: In short unaboa; hizo paranoia zako zilikuwepo hata uchaguzi wa CCM wa 2012 lakini wenye akili zao walijua hapakuwepo na mtu wa kufanya JK asiwe Mwenyekiti na mengine yote wenye akili zao walishajua was just ELECTION fever!

Na hii ya kesho kutwa; narudia, hakuna hujuma zozote dhidi ya JPM ingawaje ni kweli pia wapo wana-CCM wasiotaka JPM apewe chama! Majority ya hawa sio kwamba wana chuki na JPM bali wapo more concerned na chama chenyewe! Hawa wanaamini leadership style ya JPM akiipeleka kwenye chama basi inaweza kuathiri chama!!

Ngoja niseme jambo moja; kwaheri! Wacha niendelee kula bia hapa wakati wewe ukiendelea kupiga kelele zisizo na tija!!! Na msingi wa kelele zako ni majungu na uchonganishi! Ulianza kumchonganisha Rajab Luhwav, ukaja Ally Hapi; leo Lukuvi na Membe; kesho utasema January Makamba, mtondogoo utasema Mwigulu Nchemba, huku mwenyewe ukijitia eti huwezi kufumbia macho maovu! Mbona hatukuoni ukikemea maovu yanayofanywa na watendaji wa chama chako? JPM ana Team kubwa sana ya kugundua what's going on kwahiyo haya yako ni makelele tu yasiyo na msaada wowote kwa JPM! Wewe huna ubavu wa kufahamu intel ambayo JPM mwenyewe hana labda kama intel yenyewe ni majungu!! Hutu tuhabari habari twa kuokoteza okoteza kwenye tubaraza twa Lumumba means nothing to him but just making noises to JF Members!

KARIBU TUONGEZE DAMU!!!!
Mkuu nimeingiaje kwenye mgogoro wenu me sihusiki
 
Mkuu Lizaboni , hawa wote unaowataja naona unawaonea bure tu kama unakwepa kumtaja/kuhusisha jitihada zao na mwenyekiti wa sasa. Sioni ni kwa vipi hao unaowataja kwa pamoja au mmoja mmoja wanaweza hata kufikiria tu kuwa wanao uwezo wa kuzuia JPM kupewa uenyekiti. Alishindwa kufurukuta Mh Lowassa, pamoja na support na resources zote alizokuwa nazo, itakuwa hao ambao hata hawajai kiganjani? Kama CCM imeweza "kushinda" kwa kishindo uchaguzi wa Zanzibar, wanawezaje kushindwa kuhakikisha Mh Rais naye "anashinda" kwa kishindo uenyekiti?

Kuna mawili tu....ama JPM mwenyewe hautaki huo uenyekiti au Mwenyekiti aliyepo hana nia ya dhati ya kuachia madaraka!
 
Kama kweli kuna watu wanatumia nguvu raisi asiwe mwenyekiti lazima kuna la mgambo likilia kuna jambo.

Sote tunajua nchi yetu aijazubaa kabisa kwenye ulinzi na usalama wa mipaka yake na vyama vya siasa vimejaa cells za usalama. Binafsi raisi asipopewa uenyekiti naona ni message tosha kuna concerns na utawala wake au urafiki wake na raisi Kagame.

Ngoja tuone mwisho wake
 
Back
Top Bottom