Luhwavi, Membe na Lukuvi, mnayopanga Gizani ili Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM yawekwa Hadharani

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimeapa kusema kweli na nitasema kweli daima kwani hii ndio nguzo kuu ya kupambana na maovu yote nchini. Sitasema uongo na daima sitafumbia macho maovu yote yanayotendeka chamani bila kujali yanatendwa na nani.

Mtakumbuka ni hivi juzi tu nimeumbua mkakati wa chini kwa chini unaoratibiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhwavi wa kutaka kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM. Niliahidi kuwa nitaendelea kuwaumbua wale wote wanaoshirikiana na Luhwavi na ambao wana mikakati isiyo ya ushirika lakini dhamira yao ni kuona Magufuli hawi Mwenyekiti wa CCM iwe mwaka 2016 ama 2017. Nimerudi tena kama nilivyowaahidi na sasa ni zamu ya Benard Membe na Wiliam Lukuvi kuumbuka.

A. BENARD MEMBE
Mtakumbuka kuwa kwenye mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, Benard Membe na Edward Lowasa ni makada wawili ambao walitengeneza kambi mbili hasimu. Makada hao wawili kila mmoja alijiona kuwa yeye ndiye mrithi pekee wa Dr Jakaya Kikwete kwenye nafasi ya Urais. Hata hivyo, kwa mapenzi ya Mungu, wote hawakuwa. Lowasa alikatwa mapema kabla hata ya kufika kwenye Tano Bora. Membe alifanikiwa kuingia Tano Bora lakini akashika mkia kwenye mchujo wa kwenda kwenye Tatu Bora ambapo Dr John Pombe Magufuli aliibuka mshindi na ndiye Rais wetu.

Hata hivyo, Lowasa aliamua kutimka chamani na kwenda kugombea CHADEMA ambako aliangukia pua kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015. Hivyo nguvu ya Lowasa ikazikwa rasmi ndani ya CCM. Benard Membe aliamua kubaki chamani kwa matarajio kuwa atapewa nafasi ya uteuzi ikiwemo nafasi ya Waziri Mkuu ambayo angeipata kama angekuwa Mbunge wa Jimbo lakini alishauriwa asigombee ubunge kwa ahadi kuwa angepatiwa nafasi nyingine. Haikuwa hivyo. Membe ana manung'uniko na yupo Bechi asijue hatma ya maisha yake kisiasa.

Kutokana na hali hiyo, Membe ameibuka kuwa na chuki na Rais Magufuli na amekuwa akiratibu na kushiriki mikakati ya chini kwa chini ili Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM akishirikiana kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu Bara Rajab Luhwavi. Kwa nini Membe anafanya hivyo? Nitawaeleza.

1. Chuki na hasira ya kuukosa Urais. Baada ya Lowasa kubwagwa hata kabla ya kuingia kwenye Tano Bora, Membe akajiona ni Rais anayesubiri kuapishwa. Kubwagwa kwa Lowasa kulimfanya Membe ajione ni mshindi. Hata hivyo, kitendo cha mwanasiasa huyo kushindwa kuingia hata kwenye Tatu Bora kulimfanya ahisi kuwa amehujumiwa. Hasira zake alizielekeza kwa Benjamin Mkapa ambaye anasema kuwa ndiye aliyemwaga sumu ili asichaguliwe. Hivyo, Membe akawa na chuki na Mkapa na Rais Magufuli.

2. Kukosa nafasi ya Uteuzi. Membe alijiona kuwa anazo sifa za kiongozi mkubwa wa serikali ya Rais Magufuli. Hivyo kitendo cha Serikali hii kumuacha hata kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hakika anaona kuwa ni dharau kubwa kwake.

3. Serikali ya Awamu ya Tano kushindwa kumsimamia kwenye nafasi za Uongozi wa Jumuiya ya Madola na AU. Membe anadai kuwa kwa uzoefu wake na kufahamika kwake, angefaa kugombea nafasi zilizojitokeza kwenye Jumuiya ya Madola na Umoja wa Afrika kama Serikali yake ingemtia moyo na kuahidi kumpa ushirikiano. Hata hivyo, anaona kuwa Serikali hii haina msaada kwake na anamshutumu Rais kuwa huenda anammaliza kisiasa ili ifikapo mwaka 2020 asiwe na mpinzani ndani ya chama.

4. Kuimarisha Mtandao. Membe anashirikiana na Luhwavi ili kutengeneza mtandao wa uongozi ndani ya chama. Taarifa zilizopo ni kwamba wanataka Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti hadi 2017 na Katibu Mkuu awe Luhwavi ili asaidie kutengeneza mtandao ambao utajenga safu ya uongozi kuanzia ngazi ya taifa hadi kwenye matawi kwenye uchaguzi wa chama utakaofanyika mwaka 2017. Ama ikiwa watashindwa kukwamisha Magufuli asiwe Mwenyekiti hapo Julai 23, watafanya hivyo mwaka 2017 ambapo chama kitafanya uchaguzi katika ngazi zote. Ajenda kuu ni kuhakikisha kuwa nguvu ya Membe inarejea ambayo itamsaidia kumuangusha Rais Magufuli kwenye mchujo wa Mgombea Urais wa CCM, uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo amepanga kugombea.

B. WILLIAM LUKUVI
Huyu naye ana ndoto za kuwa Mwenyekiti wa CCM. Labda nikuulize Lukuvi, je Uenyekiti wa CCM Utauweza? Je wewe ni Presidential Material? Taarifa zilizopo ni kwamba Lukuvi anavizia nafasi ya Uenyekiti wa CCM. Kwa sasa anapima upepo na hasa anaangalia nini kitatokea Julai 23. Kwamba, ikiwa kundi la Wapinzani wa Magufuli litaelekea kushinda, anaamini kuwa anaweza kugombea na kushinda mwaka 2017 kwa vile anaamini kuwa yeyote atakayeshinda nje ya Magufuli Julai 23, atatengeneza ombwe la uongozi ambalo litahitajika kuzibwa mwaka 2017. Lukuvi anaona ni vigumu kwa sasa kumzuia Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti ila anaamini kuwa watafanikiwa kufanya hivyo mwaka 2017. Hivyo mkakati wa Lukuvi ni kwa ajili ya 2017 na si mwaka huu.

Swali la kujiuliza, je mikakati yote hii ni kwa faida ya nani? Kwani hakuna maisha nje ya siasa? Je wanafikiri ni rahisi kumuangusha Rais Magufuli sasa ilhali walishindwa hivyo mwaka 2015? Hakika huku ni kutapatapa. Siasa za mtandao zimeshazikwa Rasmi mwaka 2015 na wana CCM hatupo tayari kuona mitandao inarejea chamani

Wale wote ambao bado hamuamini kuwa Magufuli ndio Rais, mnapaswa kuamini hivyo sasa na ndiye Mwenyekiti wetu wa CCM.
 
jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,756
2,000
....kwanini jamaa huko CCM wanamuogopa Magufuli?, wana dhambi gani haswa inayowafanya wahangaike mchana na usiku kumzuia asiwe mwenyekiti?, halafu jamaa ndio alikuwa anautaka urais, wakati mwingine watz tumshukuru Mungu tu!

Lakini Magufuli nae ajiulize, kwanini kuna nguvu kubwa sana huko chamani ya kumpinga?, hii sio kwasababu baadhi ya maamuzi anayochukua yanaonekana ya kukurupuka, kwamba he isn't ready and fit enough to remain a president or be a chairman!, by the way anavyosema "angejua asingechukua form ya kugombea urais", inaonesha jamaa anawapa wapinzani wake ndani ya chama nafasi ya kushindana nae kwa kuonesha udhaifu!
 
Addict

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
702
500
Acha kuhangaika na majungu weweeeee
Chama chenu kina katiba yake...Acha katiba ifuatwe....wewe unadhani ni peke yako ambaye mawazo yako ni sahihi

Kwani magufuli akipingwa ni kosa gani katika demokrasia
Naona watu wamekudekezaaaaa na unajiona much know sasa
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
Acha kuhangaika na majungu weweeeee

Chama chenu kina katiba yake...Acha katiba ifuatwe....wewe unadhani ni peke yako ambaye mawazo yako ni sahihi

Kwani magufuli akipingwa ni kosa gani katika demokrasia

Naona watu wamekudekezaaaaa na unajiona much know sasa
Magufuli ndiye Rais wetu na ndiye Mwenyekiti wetu ajaye wa CCM. Mpende msipende ndivyo itakavyokuwa
 
jnhiggins

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
1,622
2,000
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimeapa kusema kweli na nitasema kweli daima kwani hii ndio nguzo kuu ya kupambana na maovu yote nchini. Sitasema uongo na daima sitafumbia macho maovu yote yanayotendeka chamani bila kujali yanatendwa na nani.

Mtakumbuka ni hivi juzi tu nimeumbua mkakati wa chini kwa chini unaoratibiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhwavi wa kutaka kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM. Niliahidi kuwa nitaendelea kuwaumbua wale wote wanaoshirikiana na Luhwavi na ambao wana mikakati isiyo ya ushirika lakini dhamira yao ni kuona Magufuli hawi Mwenyekiti wa CCM iwe mwaka 2016 ama 2017. Nimerudi tena kama nilivyowaahidi na sasa ni zamu ya Benard Membe na Wiliam Lukuvi kuumbuka.

A. BENARD MEMBE
Mtakumbuka kuwa kwenye mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, Benard Membe na Edward Lowasa ni makada wawili ambao walitengeneza kambi mbili hasimu. Makada hao wawili kila mmoja alijiona kuwa yeye ndiye mrithi pekee wa Dr Jakaya Kikwete kwenye nafasi ya Urais. Hata hivyo, kwa mapenzi ya Mungu, wote hawakuwa. Lowasa alikatwa mapema kabla hata ya kufika kwenye Tano Bora. Membe alifanikiwa kuingia Tano Bora lakini akashika mkia kwenye mchujo wa kwenda kwenye Tatu Bora ambapo Dr John Pombe Magufuli aliibuka mshindi na ndiye Rais wetu.

Hata hivyo, Lowasa aliamua kutimka chamani na kwenda kugombea CHADEMA ambako aliangukia pua kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015. Hivyo nguvu ya Lowasa ikazikwa rasmi ndani ya CCM. Benard Membe aliamua kubaki chamani kwa matarajio kuwa atapewa nafasi ya uteuzi ikiwemo nafasi ya Waziri Mkuu. Haikuwa hivyo. Membe ana manung'uniko na yupo Bechi asijue hatma ya maisha yake kisiasa.

Kutokana na hali hiyo, Membe ameibuka kuwa na chuki na Rais Magufuli na amekuwa akiratibu na kushiriki mikakati ya chini kwa chini ili Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM akishirikiana kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu Bara Rajab Luhwavi. Kwa nini Membe anafanya hivyo? Nitawaeleza.

1. Chuki na hasira ya kuukosa Urais. Baada ya Lowasa kubwagwa hata kabla ya kuingia kwenye Tano Bora, Membe akajiona ni Rais anayesubiri kuapishwa. Kubwagwa kwa Lowasa kulimfanya Membe ajione ni mshindi. Hata hivyo, kitendo cha mwanasiasa huyo kushindwa kuingia hata kwenye Tatu Bora kulimfanya ahisi kuwa amehujumiwa. Hasira zake alizielekeza kwa Benjamin Mkapa ambaye anasema kuwa ndiye aliyemwaga sumu ili asichaguliwe. Hivyo, Membe akawa na chuki na Mkapa na Rais Magufuli.

2. Kukosa nafasi ya Uteuzi. Membe alijiona kuwa anazo sifa za kiongozi mkubwa wa serikali ya Rais Magufuli. Hivyo kitendo cha Serikali hii kumuacha hata kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hakika anaona kuwa ni dharau kubwa kwake.

3. Serikali ya Awamu ya Tano kushindwa kumsimamia kwenye nafasi za Uongozi wa Jumuiya ya Madola na AU. Membe anadai kuwa kwa uzoefu wake na kufahamika kwake, angefaa kugombea nafasi zilizojitokeza kwenye Jumuiya ya Madola na Umoja wa Afrika kama Serikali yake ingemtia moyo na kuahidi kumpa ushirikiano. Hata hivyo, anaona kuwa Serikali hii haina msaada kwake na anamshutumu Rais kuwa huenda anammaliza kisiasa ili ifikapo mwaka 2020 asiwe na mpinzani ndani ya chama.

4. Kuimarisha Mtandao. Membe anashirikiana na Luhwavi ili kutengeneza mtandao wa uongozi ndani ya chama. Taarifa zilizopo ni kwamba wanataka Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti hadi 2017 na Katibu Mkuu awe Luhwavi ili asaidie kutengeneza mtandao ambao utajenga safu ya uongozi kuanzia ngazi ya taifa hadi kwenye matawi kwenye uchaguzi wa chama utakaofanyika mwaka 2017. Ama ikiwa watashindwa kukwamisha Magufuli asiwe Mwenyekiti hapo Julai 23, watafanya hivyo mwaka 2017 ambapo chama kitafanya uchaguzi katika ngazi zote. Ajenda kuu ni kuhakikisha kuwa nguvu ya Membe inarejea ambayo itamsaidia kumuangusha Rais Magufuli kwenye mchujo wa Mgombea Urais wa CCM, uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo amepanga kugombea.

B. WILLIAM LUKUVI
Huyu naye ana ndoto za kuwa Mwenyekiti wa CCM. Labda nikuulize Lukuvi, je Uenyekiti wa CCM Utauweza? Je wewe ni Presidential Material? Taarifa zilizopo ni kwamba Lukuvi anavizia nafasi ya Uenyekiti wa CCM. Kwa sasa anapima upepo na hasa anaangalia nini kitatokea Julai 23. Kwamba, ikiwa kundi la Wapinzani wa Magufuli litaelekea kushinda, anaamini kuwa anaweza kugombea na kushinda mwaka 2017 kwa vile anaamini kuwa yeyote atakayeshinda nje ya Magufuli Julai 23, atatengeneza ombwe la uongozi ambalo litahitajika kuzibwa mwaka 2017. Lukuvi anaona ni vigumu kwa sasa kumzuia Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti ila anaamini kuwa watafanikiwa kufanya hivyo mwaka 2017. Hivyo mkakati wa Lukuvi ni kwa ajili ya 2017 na si mwaka huu.

Swali la kujiuliza, je mikakati yote hii ni kwa faida ya nani? Kwani hakuna maisha nje ya siasa? Je wanafikiri ni rahisi kumuangusha Rais Magufuli sasa ilhali walishindwa hivyo mwaka 2015? Hakika huku ni kutapatapa. Siasa za mtandao zimeshazikwa Rasmi mwaka 2015 na wana CCM hatupo tayari kuona mitandao inarejea chamani

Wale wote ambao bado hamuamini kuwa Magufuli ndio Rais, mnapaswa kuamini hivyo sasa na ndiye Mwenyekiti wetu wa CCM.
Nimesoma mpaka hapo uliposema Membe alitegemea kupewa uwaziri mkuu nikagundua wewe ni mnafiki na muongo wa kutupwa na huenda hata katiba ya nchi huijui. Waziri mkuu ni lazima awe mbunge wa kuchaguliwa jimboni sasa Membe angewezaje kutegemea ateuliwe kuwa waziri mkuu wakati hakugombea ubunge? Baada ya kuona uzushi huu hata sikuendelea kusoma zaidi. Wadanganye wasiojua katiba
 
NAHINGA

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
1,019
1,500
Kama kweli, CCM mnajinasibu kufuata democrasia kwenye chama chenu basi acheni iwe hivyo na sio kuanza mikwara na kuwachafua wenzenu.Kuna tatizo gani Magufuli akipingwa?!! sio ndio democrasia hiyo au ww kwako democrasaia ni kusema Fulani awe mwenyekii ina ikawa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom