Luhanjo kamsafisha David Jairo hana tuhuma yoyote ya Rushwa

Arafat, we utakua ni mwanasheria unaejaribu kueleza mambo ya kihasibu!, hujui na hujui kama hujui! (usiniambie sema we unaejua kwani nakusihi subiri siku 10 za CAG utajua tu!)
 
Kasafishwa kutoka katika tuhuma ya rushwa kuja kwenye finance audit ambayo ni ukaguzi wa accounts na kuangalia kama kuna kosa la kinidhamu alilolifanya, kama ikiwa hizo fedha alizo kusanya zitaonyeshwa vyema katika vitabu au kama ikiwa wanajuwa jinsi walivyozikusanya na kuwa hazionyeshi kasoro yoyote katika vitabu vya hizo taasisi basi hana kosa tena.
Huu ukaguzi sio "normal routine" kwa CAG bali ni specific kwa ajili ya tuhuma za kifisadi zilizotolewa Bungeni kwa hiyo CAG hawezi ku-declare inocense ya Jairo kabla ya kuanza ukaguzi wa hesabu! Kama CAG ataonekana kufuatilia tu "correctness of figures" basi hakuna haja ya kufanya ukaguzi! Tunataka tupate lengo hasa la kuchukua fedha nyingi kiasi hicho (TSh 1bn/-) ikitiliwa maanani kwamba kuna tuhuma za rushwa zilizotolewa kabla ya tukio la "Barua ya Shellukindo!" Suala jingine ni, Je, matumizi ya fedha hizo yalitokana na Bajeti ya Wizara? Kama hayakuwepo, Je, kulikuwa na authorization yoyote ya fund reallocation? Nionavyo mimi endapo CAG atakodolea tu makaratasi PCCB nao waendelee na uchanguzi wa tuhuma dhidi ya rushwa ili kubaini kama kuna hongo yoyote iliyotembea kwa wabunge au kama kuna vifungu vyovyote vya Sheria vilivyovunjwa!
 
"...Jairo ambaye yuko chini yake, analazimika kwenda likizo kuanzia juzi ili kupisha uchunguzi wa awali ambao unalenga kubaini iwapo ametenda kosa la kinidhamu kwa mujibu wa sheria zinazoongoza Utumishi wa Mmma.(Philemon Luhanjo kwa mujibu wa nukuu ya Gazeti la Mwananchni)

Kwa mijibu wa hii kauli ya Luhanjo uchunguzi unaofanyika hauna haja na ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa sababu makosa aliyofanya Jairo yameshapindishwa na si ya rushwa tena na hamna uchunguzi wowote wa rushwa dhidi yake, hivyo kamsafisha na tuhuma za rushwa, wanachofanya sasa ni kumpaka mafuta tu!

Kwa mujibu wa Sheria Na.6 ya 2001 (Public Finance Act) hakuna kosa watakalo mkumba nalo Katibu Mkuu wa Wizara maana yeye ndio Accounting officer wa Wizara na fedha yote ya serikali katika wizara husika ipo chini yake, yeye ndiye mwenye VOTE ya ku-control fedha hizo na matumizi yake hivyo matumizi yeyoye atakayofanya ili mradi yawe na lisiti halali ni sahihi na haki; swali lililo baki hapo na wanalotaka kuja nalo ni kama hayo matumizi si halali au la! Ni kazi rahisi sana, kuwa na lisiti za soda na hotel walizolipa zenye gharama sawa na matumizi yaliyofanyika sidhani kama inawashinda hawa watu ambao hawana hata chembe ya aibu katika nyuso zao.

View attachment 34348
Wanacho angalia watu wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu ni kile kinachoitwa "General accepted accounting practice" yaani kama matumizi yaliyofanyika yakitunzwa vyema ki-hasibu na gharama zake ni bei halali ya soko huo ndio utakao kuwa mwisho wao, swali kwanini hawaku institute uchunguzi wa tuhuma ya rushwa? badala yake Luhanjo anaenda mbali hadi kusema kosa la kinidhamu! Kusema kosa la kinidhamu tayari ni kumsafisa na makosa ya kijinai ambayo ni fraud na corruption.

Ushauri wangu kwa serikali, badala ya kupoteza fedha zaidi kumpaka mafuta Jairo, rais atangaze kuwa Jairo hana kosa na kuwa anampangia kazi nyinge maana haina jinsi yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na Majeshi yote bado yana mtii na kumpigia Mizinga hasiwe na shaka apunguze matumizi yasiyo lazima katika uchunguzi ambao tayari wameshau elekeza katika dimbwi, awe wazi na atangaze maamuzi yake juu ya Jairo, Pia Pinda kwa mujibu wa maelezo yake bunge alisema Jairo ni wakufukuza tu, ila anamsubiri rais sasa asimamie maneno yake ajiuzulu kama kweli hana unafki katika maneno yake na matendo yake akae pembeni maana ukitofautiana mtazamo na mawazo kiasi cha kuoneka kama hivi ni bora kupisha hili husiwe sehemu ya usafi au uchafu huo unao upinga.

katiba ya tanzania inamapungufu makubwa , luhanjo anaongea kwa mamlaka makubwa kuliko waziri mkuu, wakati waziri mkuu ndio msimamizi mkuu wa serikali, raisi akisafiri na makamu wa raisi,waziri mkuu ndio anaendesha nchi kama sijakosea sasa hapo kuna mkanganyiko mkubwa wa madaraka
 
Mkuu unachanganya mambo, PM ana madaraka yake ya uendeshaji nchi anapokaimu shughuli za Mkuu wa nchi na hayana utata ingawa kuna mapungufu kwenye Katiba. Madaraka ya CS kwa Watumishi wa Umma hayana utata, suala ni PM na baadhi ya Wanasisa kujiona wana madaraka kwenye kila kitu jambo ambalo si kweli. Kuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali hakumaanishi kuwa na Uwezo wa kuwachukulia hatua Watumishi wa Umma bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wao.
 
Wana JF,

Ipo Siku Mtu ataamka zake na kwenda pale karibu na Lango la IKULU na akaanza wapasua watu vichwa la AK 47 then akaaacha majibu kama yule Jamaa wa Norway.

Maana viongozi wetu wao wemisha jiona wao wako Huru kutufanyia wajuavyo kila sheri ni nzuri kwa viongozi ila kwa walala hoi hakuna sheria nzuri hata siku mmoja. Sasa kwanini usiwafanye watu waka kusubilia nje ya lango la IKULU. Yaani viongozi wetu natumaini wana fikiria kwa Tumbo na siteka kwa Bongo za kichwani, Maana wao ndio watakao tuhepushia machafuko au kutuletea machafuko
 
Nazijuwa sheria za kazi kuliko unavyofikiria wewe, tupe sehemu inayokata kumchunga za tuhuma za rushwa!
Arafat una haraka sana Mkuu,Jairo hajasafishwa kwa Rushwa na sina hakika ya kuwepo kwa tuhuma za Rushwa dhidi yake (labda utoe ushahidi wa yote mawili).Ukisoma barua yake na hata ya mtangulizi wake utabaini kwamba walikuwa wanatekeleza utaratibu ambao nathubutu kusema kuwa upo kwa Wizara nyingi wa kuchangia gharama za bajeti na hapo ndipo tunaelezwa kuwa kuna kupanda kwa posho ambazo zinawahusisha wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge/Wizara. Suala hili lina pande mbili, kwa sehemu ya kwanza Tujiulize hapa kama ni halali kuchangia gharama hizo au wanafanya double payments? Je, fedha hizo zilifanya kazi gani? Ni jukumu la nani kufanya malipo hayo? Je, kuna ukiukwaji wowote wa Sheria katika jambo hilo? Majibu mazuri ya maswali hayo yatapatikana baada ya uchunguzi wa CAG.Sehemu ya pili itaanzia pale CAG atakapotoa ripoti yake na kuonesha kwamba malipo yalifanyika mara mbili kwa kazi moja ya kamati/safari za viongozi wa Wizara. Hapo ndipo TAKUKURU watakapoanza kazi yao na watakuwa na orodha ya beneficiaries wote.Tuwe na subira.
 
Kuna kanuni na taratibu za utumishi wa umma,kwanini hazitumiki kumuwajiisha kama zimevunjwa?, huo uchunguzi ni wanini? au ndio ku-buy time kama ilivyo kawaida ili baadaye iishe kimyakimya? sheria msumeno kwa nini haukati mbele na nyuma..???
 
Kasafishwa kutoka katika tuhuma ya rushwa kuja kwenye finance audit ambayo ni ukaguzi wa accounts na kuangalia kama kuna kosa la kinidhamu alilolifanya, kama ikiwa hizo fedha alizo kusanya zitaonyeshwa vyema katika vitabu au kama ikiwa wanajuwa jinsi walivyozikusanya na kuwa hazionyeshi kasoro yoyote katika vitabu vya hizo taasisi basi hana kosa tena.
Hivi ni lazima kila mtuhumiwa akutwe na kosa/hatia?
 
Kuna kanuni na taratibu za utumishi wa umma,kwanini hazitumiki kumuwajiisha kama zimevunjwa?, huo uchunguzi ni wanini? au ndio ku-buy time kama ilivyo kawaida ili baadaye iishe kimyakimya? sheria msumeno kwa nini haukati mbele na nyuma..???
Atawajibishwa ikithibitika kuwa amezivunja.
 
David Jairo hatenganishiki na JK, fuatilieni kidogo tu mtaona. Na hata ugumu wa kuchukua hatua haukutokana na JK kuwa safarini, umetokana hasa na hatua yenyewe inayopaswa kuchukuliwa na ni nani mwenye uthubutu huo, huku wachukuaji wenyewe wa hatua wakiwa wanalijua vema tendo alilofanya Jairo kuwa ni common practice humo katika mawizara. Kwa hiyo kombe litafunikwa, mwanaharamu akishapita litafunuliwa na maisha yataendelea.
 
hayo ndio wenyewe bwana, Magamba Limited hawawezi mwadabisha mwenzake, hata hivyo naye aliyeteuliwa kumkagua hatujui kama aweza kumweka hatiani ikigundulika maana lipoti kibao amezilalia
 
Tusubiri kazi ya CAG kwanza.
Kama taratibu za utoaji wa fedha haukufuatwa, basi game itahamia upande wa pili, zilitumikaje na nani alipata mgao/posho na kwa sababu gani?
Aliyetoa na kupokea rushwa. . . . Part 3 ya game ianze.
 
Huu ukaguzi sio "normal routine" kwa CAG bali ni specific kwa ajili ya tuhuma za kifisadi zilizotolewa Bungeni kwa hiyo CAG hawezi ku-declare inocense ya Jairo kabla ya kuanza ukaguzi wa hesabu! Kama CAG ataonekana kufuatilia tu "correctness of figures" basi hakuna haja ya kufanya ukaguzi! Tunataka tupate lengo hasa la kuchukua fedha nyingi kiasi hicho (TSh 1bn/-) ikitiliwa maanani kwamba kuna tuhuma za rushwa zilizotolewa kabla ya tukio la "Barua ya Shellukindo!" Suala jingine ni, Je, matumizi ya fedha hizo yalitokana na Bajeti ya Wizara? Kama hayakuwepo, Je, kulikuwa na authorization yoyote ya fund reallocation? Nionavyo mimi endapo CAG atakodolea tu makaratasi PCCB nao waendelee na uchanguzi wa tuhuma dhidi ya rushwa ili kubaini kama kuna hongo yoyote iliyotembea kwa wabunge au kama kuna vifungu vyovyote vya Sheria vilivyovunjwa!

Nani mwenye mamlaka ya ku-authorise reallocation ya funds katika Wizara kama si Jairo!
 
Mkuu unachanganya mambo, PM ana madaraka yake ya uendeshaji nchi anapokaimu shughuli za Mkuu wa nchi na hayana utata ingawa kuna mapungufu kwenye Katiba. Madaraka ya CS kwa Watumishi wa Umma hayana utata, suala ni PM na baadhi ya Wanasisa kujiona wana madaraka kwenye kila kitu jambo ambalo si kweli. Kuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali hakumaanishi kuwa na Uwezo wa kuwachukulia hatua Watumishi wa Umma bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wao.

Wewe ni mgumu kuelewa sijui kwanini, unachojaribu kusema ndicho walicho kifanya wakina Luhanjo, kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa Umma Luhanjo ni Mamlaka ya Nidhamu lakini nidhamu inayoongelewa hapo si makosa ya kijinai mbona huelewi.

Mtu akisha fanya makosa ya Kijina hapaswi tena kushughulikiwa na mamlaka ya kinidhamu dogo anashughulikiwa na vyombo vya dola kwa mujibu wa makosa husika. Unataka kusema wewe ukiuwa mtu Luhanjo atazua husikamatwe na kukupa Likizo ya siku kumi na kukuchunguza kama una makosa ya kinidhamu?

Kwa taarifa yako ukisha sikia makosa ya kinidhamu basi tayari kasafishwa kama hujui na hapo ndipo husipo pa elewa.
 
Arafat una haraka sana Mkuu,Jairo hajasafishwa kwa Rushwa na sina hakika ya kuwepo kwa tuhuma za Rushwa dhidi yake (labda utoe ushahidi wa yote mawili).Ukisoma barua yake na hata ya mtangulizi wake utabaini kwamba walikuwa wanatekeleza utaratibu ambao nathubutu kusema kuwa upo kwa Wizara nyingi wa kuchangia gharama za bajeti na hapo ndipo tunaelezwa kuwa kuna kupanda kwa posho ambazo zinawahusisha wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bunge/Wizara. Suala hili lina pande mbili, kwa sehemu ya kwanza Tujiulize hapa kama ni halali kuchangia gharama hizo au wanafanya double payments? Je, fedha hizo zilifanya kazi gani? Ni jukumu la nani kufanya malipo hayo? Je, kuna ukiukwaji wowote wa Sheria katika jambo hilo? Majibu mazuri ya maswali hayo yatapatikana baada ya uchunguzi wa CAG.Sehemu ya pili itaanzia pale CAG atakapotoa ripoti yake na kuonesha kwamba malipo yalifanyika mara mbili kwa kazi moja ya kamati/safari za viongozi wa Wizara. Hapo ndipo TAKUKURU watakapoanza kazi yao na watakuwa na orodha ya beneficiaries wote.Tuwe na subira.

Unabisha nini sasa hapo? Kama hana tuhuma za Rushwa kwanini unataka ushahidi wa kusafishwa nazo.
 
Kuna kanuni na taratibu za utumishi wa umma,kwanini hazitumiki kumuwajiisha kama zimevunjwa?, huo uchunguzi ni wanini? au ndio ku-buy time kama ilivyo kawaida ili baadaye iishe kimyakimya? sheria msumeno kwa nini haukati mbele na nyuma..???

Hapo ndipo kwenye hoja yangu Mkuu nashukuru sana, wanachotaka kusema ni kuwa mamlaka yake ya nidhamu inamchunguka kama kuna kosa kafanya ambayo ni bayana ni kama kavunja kanuni za Utumishi wa Umma wala si kama katoa Rushwa, hapo ndipo watu wanaposhindwa kupaelewa.
 
Hivi ni lazima kila mtuhumiwa akutwe na kosa/hatia?[/QUOTE

Swala la hatia ni la Mahakamani, hapa tunaongelea swala la Uchunguzi kwanini kosa lisi chunguzwe kama kosa la kutoa rushwa? na wabunge wachunguzwe kwa kupokea hiyo rushwa?
 
Tusubiri kazi ya CAG kwanza.
Kama taratibu za utoaji wa fedha haukufuatwa, basi game itahamia upande wa pili, zilitumikaje na nani alipata mgao/posho na kwa sababu gani?
Aliyetoa na kupokea rushwa. . . . Part 3 ya game ianze.

Na kama taratibu za kutowa fedha zilifuatwa nini kitakacho fuata?
 
Back
Top Bottom