Luhaga Mpina unasema January Makamba anastahili kuwepo gerezani, wewe unastahili kuwepo bungeni?

Apr 24, 2011
29
542
Luhaga Mpina leo amenukuliwa na vyombo vya habari anasema January Makamba ni mhujumu uchumi anayepaswa kuwa gerezani siyo Ofisi ya wizara ya nishati. Binafsi sina tatizo na hilo alilosema. Lakini Luhaga Mpina wewe hupaswi kuwa mbunge wa Kisesa. Hukuchaguliwa uchaguzi wa 2020, mgombea wa CHADEMA, Francis Kishabi alitangazwa mshindi usiku, asubuhi ukatangazwa mshindi wewe. UJAMBAZI!

Nhundu Francis kishabi, aligombea udiwani kata Mwandoya, Jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu, Simiyu na pia aligombea ubunge jimbo la kisesa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisesa kwa tiketi ya CHADEMA, viti vyote viwili alishinda.. Matokeo ya udiwani yalibandikwa kabisa Francis Kishabi mshindi baadae kidogo yakachanwa kwa madai matokeo ya udiwani na ubunge yote yanatolewa Mwanhuzi

Kesho yake kilichofuata..

Hata udiwani aliokuwa ametangazwa kwamba ameshinda wakasema kashindwa, ubunge kapokwa akapewa Luhaga Mpina, Magufuli akampa uwaziri wa Mifugo na Uvuvi (alitueleza sababu akisema aliamua kuchagua mtu kichaa-kichaa kama yeye amsaidie). Yote haya yanafanyika kwenye mkoa ambao RC ni mtakatifu Anthony Mtaka.. Hakuweza kuruhusu demokrasia kushamiri

Kilichofuata!

Nhundu Francis Kishabi alikuwa anakabiliwa na shauri la Arson 1/2018 lenye mashtaka matano (5) ndani yake likiwepo shtaka la kuchoma kituo cha polisi Mwandoya, katika jimbo la Kisesa, Meatu, Simiyu, akihusishwa na wapiga kura wake wapatao 24. kati ya mwaka 2015—2020 Francis Kishabi alikuwa diwani wa kata ya Mwandoya (Chadema) pia Mwenyekiti wa Chadema Meatu.

Shauri hilo liliendeshwa kwa miaka mitatu, Mwishoni kabisa wa shauri hilo, hakimu aliyeanza na shauri hilo tangu mwanzo, akapandishwa cheo na kuhamishwa mkoa mwingine kikazi na jalada likapokelewa hakimu mwingine (mgeni) aliyepokea mwishoni wakati wa kufunga utetezi kwa Upande wa mashtaka.

February 2021 Francis Kishabi akahukumiwa miaka 3 gerezani pamoja na wenzake. Kishabi alikata Rufaa. Na 30/7/2021 Mahakama kuu kanda ya Shinyanga ikamuachia huru NHUNDU FRANCIS KISHABI na wenzake wanne waliokuwa wamehukumiwa miaka 3 gerezani, Feb 2021 kwa tuhuma za kuchoma moto Kituo cha polisi Mwandoya-Simiyu.. 2015/2020 Kishabi alikuwa diwani kata ya Mwandoya, pia mwenyekiti wa Chadema-Meatu, mgombea ubunge Kisesa 2020.

Luhaga Mpina sasa ni mbunge wa jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu, mkoa wa Simiyu, leo amenukuliwa anasema January Makamba anastahili kuwa gerezani kwa Makosa ya uhujumu uchumi (Binafsi sina tatizo na hilo), lakini swali langu ni, Je, Luhaga Mpina anastahili kuwa bungeni? Alishinda ubunge? Nani alimchagua? Misimamizi wa uchaguzi, Meatu Fabian Manoza alipora uchaguzi kwa niaba ya CCM.

#MMM, Martin Maranja Masese

20220406_172255.jpg
 
Unamlaumu Mpina kwani alijitangaza mwenyewe?

Wewe nae umeanza kuwa zuzu sasa. Baada ya kesi Mahakamani umeanza kupoteza mwelekeo.
Mda so mrefu utapotea kabisa.

Tunajadili swala la kitaifa kuhusu mfumuko wa bei wewe unaanza leta ngonjera zako as if zinaleta ugali kwa mama yako.
 
Sasa Mpina kama ana ushahidi auweke hadharani au aupeleke kunakohusika sio kutupigia kelele....siasa za kinafiki hatupaswi kuziendekeza, kama ana ushahidi auweke hadharani bila kupepesa macho, AU ATUAMBIE AMEPELEKA USHAHIDI TAKUKURU AU KWA WAHUSIKA WAMEKAA KIMYA HAWAKUCHUKUA HATUA.

Mimi leo ninaweza kuwaambia namdai TRUMP na PUTIN hela $300000...muanze kuwashutumu sasa wamenidhulumu.

Ninachoona hii nchi sasa hivi kuna struggle of power, kuna mparuano ambao unaleta siasa chafu zakijinga jinga...
 
Unamlaumu Mpina kwani alijitangaza mwenyewe?

Wewe nae umeanza kuwa zuzu sasa. Baada ya kesi Mahakamani umeanza kupoteza mwelekeo.
Mda so mrefu utapotea kabisa.

Tunajadili swala la kitaifa kuhusu mfumuko wa bei wewe unaanza leta ngonjera zako as if zinaleta ugali kwa mama yako.
January naye alijichagua uwaziri mwenyewe?
 
Luhaga Mpina leo amenukuliwa na vyombo vya habari anasema January Makamba ni mhujumu uchumi anayepaswa kuwa gerezani siyo Ofisi ya wizara ya nishati. Binafsi sina tatizo na hilo alilosema. Lakini Luhaga Mpina wewe hupaswi kuwa mbunge wa Kisesa...
Mbona matokeo hayakuoingwa mahakamani.Ramli chonganishi, hebu muache mwakilishi wetu bhana apige kazi.Hapa KAZI TU
 
Luhaga Mpina leo amenukuliwa na vyombo vya habari anasema January Makamba ni mhujumu uchumi anayepaswa kuwa gerezani siyo Ofisi ya wizara ya nishati. Binafsi sina tatizo na hilo alilosema. Lakini Luhaga Mpina wewe hupaswi kuwa mbunge wa Kisesa...
Kuganga mnamsagia kunguni.

Ukiwa mchafu usichokoze watu.

Mpina ataipata🤣🤣
 
Back
Top Bottom