figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,654
- 59,077
Salaam Wakuu,
Hapa chini ni barua ya aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO, ndugu Luhaga Mpina kwenda kwa Onorius Njole Katibu wa tume ya Samia.
=======
Luhaga Joelson Mpina
30 Januari, 2026
NDG. ONORIUS .J.NJOLE
KATIBU WA TUME,
TUME YA KUCHUNGUZA MATUKIO WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA OKTOBA 2025
S.L.P 471 DAR ES SALAAM
YAH: WITO WA KUKUTANA NA TUME YA RAIS YA KUCHUNGUZA MATUKIO YA WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2025
Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu.
2. Nakiri kupokea barua yako yenye Kumb.NaaSAE.351/527/01 ya tarehe 21 Januari, 2026 ikinitaka kufika kukutana Tume tarehe 31 Januari 2026 kuanzia saa 8: mchana hadi saa 9:00 alasiri katika Ukumbi wa Manyara Benki Kuu- Dar es Salaam.
3. Utakumbuka kuwa Mnamo tarehe 18 Novemba 2025 Chama changu cha ACT Wazalendo kilitoa Taarifa kwa Umma kuwa kinapinga na kinakataa kabisa Tume iliyotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuchunguza matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025 na siku zilizofuata.
4. Chama cha ACT Wazalendo kiliweka wazi kwamba hakitashiriki kwa namna yoyote ile katika uchunguzi utakaofanywa na Tume hii. Hatutatoa ushahidi wala kutoa ushirikiano wowote kwani tunatambua kuwa ni chombo kisicho huru na kitakachotegemea maagizo ya Serikalia
5. Na hata nilipozungumza na vyombo vya habari tarehe 6 Disemba 2025 ambapo niliunga mkono msimamo wa Chama kuwa Tume hiyo siyo huru na imeundwa bila kuzingatia kanuni na taratibu za usuluhishi wa migogoro (Conflict Resolution Strategies and Guidelines)
5. Hivyo basi kwa Heshima kubwa nakujulisha kuwa sitaweza kuhudhuria wito huo kwa ajili ya majadiliano.
Pamoja na barua hii nimeambatisha nakala ya Tamko Ia Chama cha ACT Wazalendo.
Ninakushuruku kwa ushirikiano.
Luhaga Joel Mpina