Lugola awatangazia vita wanaomkejeli Rais Magufuli mitandaoni

Lugola acha watu waseme,usiwatishe,maana lipo kwenye katiba badilini katiba kama mnataka hivyo zaidi ya hapo kelele za kumsema rais vibaya au vizuri zitakuwepo tu hata afanye mazuri kiasi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio kweli.Huyu wa sasa ndo anaongoza kwa kusemwa..
mpaka wateule wake wanapaniki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi huyu watu wanasema chini chini tofauti na Jakaya hakukuwa na sheria za mitandao, hafu ona hata matokeo ya uchaguzi asilimia zake so public opinion lazima zitofautiane mno.

Hao wateule ni vile wanatumia nguvu kutaka kusifiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ipo kwenye taharuki. Kila mwenye dhamana ya kupiga mkwara basi anaitumia vyema nafasi yake.

Nyerere aliwahi kuandika kitabu kiitwacho

"Uongozi wetu na hatma ya Tanzania"


Nadhani hata Magufuli mwenyewe sometimes anawashangaa. Yaani hapa duniani unataka kila mtu amsifie mtu aliyekupa ulaji? Huyu Lugola amwambie ateue watu wote tuwe mawaziri kama yeye, ndipo sote tutafiha hekima zetu tutaanza kumsifia kila wakati.
 
Kama hizi "Routine Challenges and Jabs" ndizo zinamsumbua rais hadi anawatuma akina Lugola kutisha watu basi afadhali asichukue tena fomu kutetea kiti make anaweza akapata "Myocardia Infarction" ya bure kabisa.

Hizi "Jabs" zipo tu duniani kote huwezi kuzikwepa so long as you're there as a leader, hazikwepeki vinginevyo ni kuacha tu urais na kufanya shughuli zako binafsi ambazo ni less stressful. That's the only solution but intimidation and threats, won't do.
 
Kama hizi "Routine Challenges and Jabs" ndizo zinamsumbua rais hadi anawatuma akina Lugola kutisha watu basi afadhali asichukue tena fomu kutetea kiti make anaweza akapata "Myocardia Infarction" ya bure kabisa.

Hizi "Jabs" zipo tu duniani kote huwezi kuzikwepa so long as you're there as a leader, hazikwepeki vinginevyo ni kuacha tu urais na kufanya shughuli zako binafsi ambazo ni less stressful. That's the only solution but intimidation and threats, won't do.
Hakuna mwanamume mwoga wa hoja kama jiwe. Ni mwoga, ni mwoga kupindukia. Kutokana woga wake wa hoja ndio maana alipiga marufuku mijumuiko ya kisiasa (upande wa upinzani) mara tu alipoingia madarakani. Na ndio maana anatumia nguvu nyingi ya kidola kudhoofisha upinzani ikiwa ni pamoja na projekti maalumu na maarufu ya 'kununua' wabunge na madiwani njaa wa kambi ya upinzani. Hawezi kuhimili nguvu ya hoja.
 
Mimi ninashauri yaainishwe maneno ya kejeli na matusi ni yepi maana kunawatu watakamatwa ilihali hawakuwa na lengo la kutukana bali wamekosa tafsiri ya matusi kejeli au uchochezi
 
'...Sio kwamba siambiwi yanayosemwa, sio kwamba sisikii, Au sio kwamba sina Cha kujibu.... naamua Kuwa kimya kwa Kuwa sioni faida ya kujibu jibu Kila kitu...'-Rais wa Nne wa Tanzania 2005-2015 Jakaya Kikwete
Mkuu post yako hii imepata "likes" za kutosha yaan kama zote Kwa leo.
Hongera kwa kutukumbusha
 
Mh lugola ,vip wanaowakejeli wagonjwa kuwa wanazulula🤣🤣🤣🤣 Nao udili nao Maana wamezidi😁wamesahau kuwa nao wanaumwa wanavitabu vyao vya MATIBABU India😁😁😁
 
Back
Top Bottom