Lugola aagiza Polisi kuwakamata wapinzani ‘wanaomtukana’ Rais kupitia mikutano ya ndani. Asisitiza mikutano ya siasa ya hadhara marufuku

Kuzuia shughuli za siasa ni faida kwa upinzani na ni hasara kwa ccm.Faida Mbili kwa upinzani, kwanza ccm inashindwa kujua nguvu za wapinzani wanabaki na mawazo hauna nguvu hivo ccm inalala ikijua imemaliza Kazi upinzani Uko moyoni mwa watz wote walioumizwa na awamu hii,PILI Ccm haiwezi jua hoja na ajenda za upinzani ni zipi ili iweze kujipanga kuzijibu ikifika wakati kipenga kimelia upinzani wana nafasi kubwa sana ya kutema nyongo na kuporomosha makombora ya mashambulizi mazito kwa ccm ambapo ccm haiwezi kupata mda wa kujibu hoja wakati wa kujinadi maana hoja zinakuwa nyingi kuliko uwezo wa ccm kujibu,tofauti na kama ingeruhusiwa mikutano watu wangekuwa washazichoka hoja na zisingekuwa na nguvu wakati wa kampeni
Waache waendelee kujichimbia kaburi
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewaagiza Makamanda wa Polisi nchini washirikiane na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuchunguza na kuwakamata wapinzani wanaomtukana Rais pamoja na Serikali kwa ujumla kupitia vikao vyao vya ndani vya siasa.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mjini Kilosa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kilosa Town, Wilayani humo, jana, Lugola amesema ana taarifa kuna baadhi ya wapinzani ambao wanafanya vikao vyao vya ndani huku wakitukana, kubeza pamoja na kuwachonganisha wananchi na Serikali yao ambayo inaongozwa na Rais Dkt John Magufuli.

Kutokana na wapinzani hao kuvunja agizo lililowekwa, amewaagiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wilaya nchini kuwachunguza viongozi wa siasa kwa kina kupitia vikao vyao, na watakaowabaini wanavunja utaraibu huo wawakamate haraka iwezekanavyo.

Lugola ameendelea kusisitiza kwa kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya siasa ya hadhara mpaka hapo kampeni zitakapoanza rasmi kwa uchaguzi ujao.

“Mimi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sitakubaliana na kiongozi wa chama chochote kuvunja agizo tulilolitoa nchi nzima kwa kutokuruhusu kufanyika mikutano ya hadhara ya siasa, na pia kupitia mikutano ya ndani ambayo inafanyika, ambapo baadhi ya wanasiasa wahuni wanamtukana Mheshimiwa Rais ambaye ndio kiongozi mkuu wa nchi, mimi sitakubaliana na hilo,” alisema Lugola.

Lugola amewataka wapinzani kuwa wasikivu kwa kufuata sheria za nchi na pia kutambua kuwa, Rais wa nchi hii ambaye kipenzi cha wananchi anapewa heshima yake kwa kuiletea maendeleo nchi.

Lugola alisema Rais Magufuli ni kiongozi ambaye kwa muda mfupi ameiletea mabadiliko makubwa nchi, na pia mipango mikubwa ya maendeleo inakuja katika uongozi wake.

Lugola alifanya mikutano miwili ya hadhara wilayani Kilosa, ambapo mkutano mmoja ulifanyika mjini Kilosa na mwingine ulifanyika Tarafa ya Kimamba wilayani humo, ambapo alizungumza na wananchi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi wilayani humo kupitia kutoa nafasi kwa wananchi kutoa kero zao.

Aidha, Lugola aliwataka polisi nchini kuwa makini kwa kutenda haki wakati wanaletewa kesi za ardhi zenye jinai hasa katika Mkoa wa Morogoro ambao unakabiliwa na migogoro ya aina hiyo.

“Nimepata malalamiko ya baadhi ya polisi hapa Kilosa kutokutenda haki katika ukamataji wa watuhumiwa, polisi amepewa taarifa ya mtuhumiwa lakini hamkamati, sasa polisi ambaye ametajwa hapa mkutanoni hakumkamata mtuhumiwa huku uthibitisho ukionyesha kabisa mtuhumiwa amekosa na anapaswa kuwepo kituoni, naagiza polisi huyo akamatwe awekwe mahabusu,” alisema Lugola

Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa za wahamiaji haramu katika mkoa huo ili Uhamiaji iweze kuwakamata na kuwafungulia kesi wahamiaji hao kutokana mataifa mbalimbali wanaoingia nchini bila kufuata taratibu za nchi.

“Wakazi wa Kilosa, endeleeni kuchapa kazi, moto wa Magufuli mnauona, sasa hakuna uonevu, hakuna kauli ‘unanijua mimi nani’, nchi imetulia, maendeleo ya kasi mnayaona, huyu Magufuli hakika ameletwa na Mungu,” alisema Lugola.

Lugola amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani humo akitembelea Wilaya za Morogoro, Mvomero na Kilosa, akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.

Lugola mwaka jana mara alipoteuliwa kuiongoza Wizara hiyo, alitoa maagizo mbalimbali kwa Makamanda wa Polisi Mikoa nchini ambayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe
Lugola anatatua migogoro ya ardhi kama nani ?
 
Lugola mbona unamitafutia ban hapa JF wewe tumbotumbo?
Hayo maagizo kampe mchepuko wako!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtuhumiwa wa rushwa aliyefutiwa mashtaka kisiasa badala ya kusafishwa mahakamani! Mtu wa aina hii anakuawaje waziri? Hakuna watu safi zaidi? Au ndiye atakuwa mtiifu zaidi? Au ndiyo ccm mpya isiyokuwa na maadili ya uongozi? Usemi kuwa mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa kwa usinzi huku kwetu hauna maana!.
 
Mmeipitisha hiyo sheria mpya baada ya katazo..? Kumbuka katiba imesema hivyo, na ikaja kutengenezewa sheria ya vyama vya siasa ambako humo shughuli za vyama vya siasa zimeruhusiwa.. Hilo katazo ni haramu.. Hata mkija na utetezi gani, halibadili uharamu wake.. Ndo tunaposema udikteta huo..

Halafu mbona katazo hili haramu ni kwa upinzani tuu..? Mbona Bashiru & Polepole wanazunguka na kufanya mikutano..? Ndo udikteta huo..

Wabunge wote wafanyie shughuli zao katika majimbo waliyochaguliwa. Hata hilo ni baya jamani? Mbunge wa Iringa anataka akafanyie siasa zake Mwembeyanga pale kwa vile anaishi Mikocheni. Si utapeli huo?

Pia naona unataja katiba jumla jumla lakini ni dhahiri hata hujaisoma. Hebu lete hivyo vipengele tuvichambue uone kama havijakusuta. Acha kuimbishwa mambo kikasuku.

Halafu Bashiru na Polepole sio viongozi wa majimbo. Wao kwa ujumla wanakagua utekelezaji wa ilani ya chama ambacho ikifika 2020 mtakibana majukwaani. Na hii ndiyo kazi yao.

Tatizo la Upinzani hasa Chadema wana Katibu Mkuu togwa (kapooza) hana mikakati kama alivyokuwa Dkt. Slaa.

Siasa za kihuni na kilaghai zimepitwa na wakati. Badilikeni.
 
Waoga katika ubora
tapatalk_jpeg_1550950906922.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
fuc** Lugola unatumika sana dingi kumbuka ulipotoka..
rais sio mungu na mungu sio rais malaya wewe..
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewaagiza Makamanda wa Polisi nchini washirikiane na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuchunguza na kuwakamata wapinzani wanaomtukana Rais pamoja na Serikali kwa ujumla kupitia vikao vyao vya ndani vya siasa.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mjini Kilosa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kilosa Town, Wilayani humo, jana, Lugola amesema ana taarifa kuna baadhi ya wapinzani ambao wanafanya vikao vyao vya ndani huku wakitukana, kubeza pamoja na kuwachonganisha wananchi na Serikali yao ambayo inaongozwa na Rais Dkt John Magufuli.

Kutokana na wapinzani hao kuvunja agizo lililowekwa, amewaagiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wilaya nchini kuwachunguza viongozi wa siasa kwa kina kupitia vikao vyao, na watakaowabaini wanavunja utaraibu huo wawakamate haraka iwezekanavyo.

Lugola ameendelea kusisitiza kwa kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya siasa ya hadhara mpaka hapo kampeni zitakapoanza rasmi kwa uchaguzi ujao.

“Mimi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sitakubaliana na kiongozi wa chama chochote kuvunja agizo tulilolitoa nchi nzima kwa kutokuruhusu kufanyika mikutano ya hadhara ya siasa, na pia kupitia mikutano ya ndani ambayo inafanyika, ambapo baadhi ya wanasiasa wahuni wanamtukana Mheshimiwa Rais ambaye ndio kiongozi mkuu wa nchi, mimi sitakubaliana na hilo,” alisema Lugola.

Lugola amewataka wapinzani kuwa wasikivu kwa kufuata sheria za nchi na pia kutambua kuwa, Rais wa nchi hii ambaye kipenzi cha wananchi anapewa heshima yake kwa kuiletea maendeleo nchi.

Lugola alisema Rais Magufuli ni kiongozi ambaye kwa muda mfupi ameiletea mabadiliko makubwa nchi, na pia mipango mikubwa ya maendeleo inakuja katika uongozi wake.

Lugola alifanya mikutano miwili ya hadhara wilayani Kilosa, ambapo mkutano mmoja ulifanyika mjini Kilosa na mwingine ulifanyika Tarafa ya Kimamba wilayani humo, ambapo alizungumza na wananchi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi wilayani humo kupitia kutoa nafasi kwa wananchi kutoa kero zao.

Aidha, Lugola aliwataka polisi nchini kuwa makini kwa kutenda haki wakati wanaletewa kesi za ardhi zenye jinai hasa katika Mkoa wa Morogoro ambao unakabiliwa na migogoro ya aina hiyo.

“Nimepata malalamiko ya baadhi ya polisi hapa Kilosa kutokutenda haki katika ukamataji wa watuhumiwa, polisi amepewa taarifa ya mtuhumiwa lakini hamkamati, sasa polisi ambaye ametajwa hapa mkutanoni hakumkamata mtuhumiwa huku uthibitisho ukionyesha kabisa mtuhumiwa amekosa na anapaswa kuwepo kituoni, naagiza polisi huyo akamatwe awekwe mahabusu,” alisema Lugola

Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa za wahamiaji haramu katika mkoa huo ili Uhamiaji iweze kuwakamata na kuwafungulia kesi wahamiaji hao kutokana mataifa mbalimbali wanaoingia nchini bila kufuata taratibu za nchi.

“Wakazi wa Kilosa, endeleeni kuchapa kazi, moto wa Magufuli mnauona, sasa hakuna uonevu, hakuna kauli ‘unanijua mimi nani’, nchi imetulia, maendeleo ya kasi mnayaona, huyu Magufuli hakika ameletwa na Mungu,” alisema Lugola.

Lugola amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani humo akitembelea Wilaya za Morogoro, Mvomero na Kilosa, akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.

Lugola mwaka jana mara alipoteuliwa kuiongoza Wizara hiyo, alitoa maagizo mbalimbali kwa Makamanda wa Polisi Mikoa nchini ambayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe
Naona kabisa Rais akiwarudisha Hawa wahuni sababu amebadili uelekeo. Ameshaonja utamu wa madaraka, the only way ni kurudisha watu vichaa.

Namuona Lugola, Bashite, Mpina na wa aina hiyo wakirudishwa kumhalalishia mama uhuni wao. Hawa ni mabingwa wa kujitoa akili, wananchi mnabaki kuwalaumi wao na mnaona Rais ni malaika kumbe yeye ndio amewatuma.

Usiniambie kwamba mtu kama Sabaya alikuwa taarifa zake hazipo Ikulu. Sitaki kuamini hilo na ndio maana alisifiwa na Magufuli pamoja na Bashite.

Nakumbuka ule msemo wa Kamanda mstaafu wa Dodoma, RPC Muroto alisema "atawapiga kipigo Cha mbwa mwizi"

Kuna yule mwingine alisema "sadism is inevitable when the system is alarming". Hawa watu wakipewa green light kufanya waliyofanya.

No wonder wakifanya ukatili, jamaa alikuwa anawasifia sana. He knew ameuza lawama kwao na shukrani yake ilikuwa kuwaprotect na kuwaacha madarakani wakiwa na powers kubwa sana kushinda hata immediate bosses wao.

Huyu mama anajua anachofanya, ni mhuni tu kama wahuni wengine.
 
Back
Top Bottom