Lugha zetu za asili Tanzania na Herufi za kizungu.

Lakini still wana herufi zao kutokana na lugha yao, mfano kabla hakijaja kiswahili lugha za kibantu wao walikua na herufi gani za lugha zao??
Hilo swali ulilouliza ndilo ambalo pia mleta mada ameuliza.

Mfano kabla ya kuja kwa hao wazungu na waarabu waliotuletea aina za uandishi, sisi tulikuwa na nini?

Au tuliishia katika uchoraji na uchongaji tu kama ile michoro ya Amboni Tanga na pia sauti za mawasiliano tu bila uandishi wa herufi zetu?
 
Oooh shukran sana kwa kunielewesha bro,
ila siamini kama tulikua hatuna uandishi wetu, ninachoona tuwaulize wazee wa zamani kama bado wapo.
 
Haina shida mkuu.
Nilitaka afafanue labda kuna kitu anamaanisha ambacho mimi sikijui ili nijifunze.
Si unajua tena elimu haina mwisho mkuu.
Baada ya Yesu Kristo kufufuka Dunia ilianza kuhesabu mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu...na kwa minajili hiyo leo ni mwaka wa 2017.

Ila kabla ya hapo tayari ilishapita miaka mingine mingi baada tu ya kuumbwa Adam.
 
Ila pia kumbuka kuwa Watu weusi wenye asili ya kibantu (wenye pua kubwa na lips pana) ndio wanaoongoza kwa kusubiri kutafuniwa kiila kitu.

Hawana asili ya Ubunifu (Innovation), Ugunduzi (Discovery) wala Uvamizi kwa nia ya utawala / ushikaji dola (Conguering).

Ni kama watu hawa waliumbwa ili kutawaliwa na kuwatumikia Wazungu, Waarabu, Wahindi na hata Wachina...na mpaka leo ni Watumwa kwa races hizo na ushahidi upo wazi.
Nakuelewa maana yako. Lakini nilidhani hiyo ilikuwa enzi zile za mababu wa mababu, inawezekana hadi leo na utitiri wa watafiti tulionao hilo likawa bado nitatizo letu wabantu?! Na kama ndivyo, inamaanisha hata kuchora chora kwenye mawe hatukuwahi au babu zetu hawakuchora mawasiliano yao au wagunduzi hawa kuyaelewa?!
Basi tukiri sisi hatuwezi kugundua,je wale athropoligist wanaweza kutafuta haya ma herufi ya mawasiliano ya makabila yetu kama yamewahi kuwepo?! Mimi hata tukifanyiwa utafiti na wanaojua kama lugha zetu zitapata herufi nitafurahi sana. Tusaidie kama wapo anthropologist wa lugha unaowafahamu wanaweza kuwa na data za kuanzia utafiti wa hili mkuu.
 
Oooh shukran sana kwa kunielewesha bro,
ila siamini kama tulikua hatuna uandishi wetu, ninachoona tuwaulize wazee wa zamani kama bado wapo.
Kama kungekuwa na aina ya uandishi, leo hii ungekuwepo kule Cameroon kabla ya kifaransa.

Asili ya Wabantu ni Cameroon.

Wale wachache wasio wabantu kama waethiopia na wamisri wa zamani wana aina yao ya uandishi na Lugha yao complete kama kiaramaic.

Wamasai sio wabantu ni nilotes na wana uhusiano mkubwa na waethiopia, wamasai halisi wana gestures inayotambulisha namba zooote kuanzia enzi na enzi.

Huoni Wabantu wanatafuniwa kiiila kitu, hata herufi rasmi ya kilugha hakijawahi kugunduliwa na kabila lolote lenye asili ya kibantu.
 
Nakuelewa maana yako. Lakini nilidhani hiyo ilikuwa enzi zile za mababu wa mababu, inawezekana hadi leo na utitiri wa watafiti tulionao hilo likawa bado nitatizo letu wabantu?! Na kama ndivyo, inamaanisha hata kuchora chora kwenye mawe hatukuwahi au babu zetu hawakuchora mawasiliano yao au wagunduzi hawa kuyaelewa?!
Basi tukiri sisi hatuwezi kugundua,je wale athropoligist wanaweza kutafuta haya ma herufi ya mawasiliano ya makabila yetu kama yamewahi kuwepo?! Mimi hata tukifanyiwa utafiti na wanaojua kama lugha zetu zitapata herufi nitafurahi sana. Tusaidie kama wapo anthropologist wa lugha unaowafahamu wanaweza kuwa na data za kuanzia utafiti wa hili mkuu.
Nafikiri hayajawahi kuwepo, zaidi ya michoro, michongo na lugha ya mawasiliano.

Kwanza kumbuka uandishi huo ni source au element mojawapo ya formal education.

Uliwahi kusikia kuwa Wabantu walikuwa na Formal education kabla hatujaletewa na Wakoloni?

Wakati hao wakoloni wakiandika kwa kutumia wino na bawa la kuku katika ofisi zao enzi hizo sisi tulikuwa tunachora wanyama kwenye mapango kwa kutumia damu.

Huoni tofauti hiyo?
 
'Time'
Ndiyo inayolea relevance ya jambo fulani.
Unamaanisha nyakati hizi hatuwezi kugundua au kutengeneza kitu chetu?! Najua itakuwa ngumu lakini ugumu sio kushindwa.Wataalam wanaweza kuweka mawazo yao pamoja wakafanya hii kitu, inaweza isitumike leo lakini wanaweza kuwa na kumbukumbu za data za kuanzia na wengine wakamaluzia. Nasikia hata wale ma genius kuna fomular zao zingine hazijawa practical. Zipo na zinakubalika theoretically but not practically yet. Nasi tunaweza kwa misingi hiyo.
 
Nafikiri hayajawahi kuwepo, zaidi ya michoro, michongo na lugha ya mawasiliano.

Kwanza kumbuka uandishi huo ni source au element mojawapo ya formal education.

Uliwahi kusikia kuwa Wabantu walikuwa na Formal education kabla hatujaletewa na Wakoloni?

Wakati hao wakoloni wakiandika kwa kutumia wino na bawa la kuku katika ofisi zao enzi hizo sisi tulikuwa tunachora wanyama kwenye mapango kwa kutumia damu.

Huoni tofauti hiyo?
Naona tofauti. Lakini nimewahi sikia simuluzi kwamba wakati wakoloni wanaanza kuja hao babu zetu walipigana nao,na katika harakati hizo nasikia babu zetu walikuwa wakiwasiliana kwa alama kama code zao za mawasiliano ambazo wazungu hawakuzijua. Sasa hizo code zilikuwa na maumbo gani na hayo maumbo yalimaanisha nini?! Mimi nadhani tukianzia hapo tunaweza tuka kuta hizo herufi au wewe bado hushawishiki?! Labda hatukuwa na formal education lakini tuliwasiliana. Unaamini tusinge tawaliwa na wakoloni tunge kuwa tunaongea bila kuandika mpaka leo?!
 
Tatizo hizo codes hazikuandikwa. Wahindi walitawaliwa lakini waliweza baadaye kutumia herufi zao katika maandishi ya lugha zao. Sisi bado tulikuwa hatuna maandishi.
 
Habari zenu wana bodi.
Huwa najiuliza maswali lakini sipati majibu lakini leo naomba nanyi mnisaidie.
Tanzania tuna makabila mengi na haya makabila yanaongea lugha tofauti. Lakini pia tunaongea kiswahili. Swali langu ni hili ilikuwaje tuweze kuongea lugha tofauti lakini tukashindwa kuwa au kuweza kuandika hizi lugha zetu kwa HERUFI zetu?! Yani makabila yote tulijua kuongea lakini hakuna hata kabila moja liliweza kuwa na herufi za maandishi yake?! Angalia Ethiopia wana herufi zao,wahindi wana herufi zao,wachina wana herufi zao, warusi wana herufi zao,sweden wana herufi zao waingereza wana herufi zao. Sisi Tanzania tulishindwa au tulitegemea ugunduzi wa wazungu kutuwekea vitu vyetu kwenye kumbukumbu na kwakuwa hawakuziweka kumbukumbu inamaana hatukuwa na herufi zetu kweli?!
Je, tunaweza kutengeneza herufi zetu leo au ugunduzi uliishafungwa?! Ikiwa tunaweza kugundua leo, je kumeshawahi kufanyika utafiti wa kuanza kutengeneza herufi zetu au ugunduzi ni wa kiteknelogia tu lakini sio maandishi(herufi)?!. Kwa wataalam wa tafiti za lugha kumewahi au wamewahi kuona herufi zozote za kuwakilisha maandishi ya kabila lolote Tanzania?! Je kuna wataalam wale wanaoitwa ma anthropologist wa lugha?! Je wamewahi kutafiti herufi za kuwakilisha mawasiliano ya kimaandishi ya lugha yoyote ya makabila yetu Tanzania?!
Kwa BAKITA kiswahili tunaweza kukiundia herufi zetu mbali ya hizi A to Z?! Je kuna juhudi hizo au mnakuza lugha tu herufi zina mamlaka yake?!
Ni mjadala wa wote kwa yeyote anayejua chochote kuhusiana na hili. Karibuni kwa mjadala.
Fanya utafiti ubuni herufi zako na ikiwezekana anza na kabila lako, utapata u-professor kiulaini.
 
Mi naamini kulikuwa na michoro iliyokuwa inamaanisha kitu flani. Ama kwenye magome au mapango. Labda tafsiri yake haikupatikana au zilipotea kwasababu za vita na kuhama hama bila mpangilio au vita. Maana hadi leo huwa naona history au geographical channel wakisema kuna alama au michoro kwenye zile pyramid hakuna anayefahamu zilimaanisha nini, licha ya kuwa researched intensively still hakuna ajuaye.
Sisi tulidharaulika na hakuna aliyeamini hata sasa kutuamini tunafahamu jambo lolote interesting. Story zetu hatuna hata hatuziandiki, leo tunasoma historia zao na vitabu vyao sio vyetu,waandishi wao hadithi zao, kwa mantiki hiyo ni rahisi kupoteza maliasili zetu in terms of kumbukumzap,
Najua lugha za leo umuhimu nasi ni mawasiliano lakini uchumi pia umeathiri. Kila mtu anataka kujifunza kiingereza, kifaransa,kijerumani au kichina ili aweze kufanya biashara au kupata kazi kwenye maeneo yanayoongea lugha hizo.
Still siamini eti hadi leo tungekuwa tunaongea tu bila kuandika, na ninaamini babu zetu waliandika kwa michoro, sema hata babu zetu hawakuwa na namna nzuri kuzitunza. Na ziliweza kupotea haraka baada ya kuletewa hizi elimu za kiarabu na kiingereza. Historian anthropologist waligundua mafuvu, nyayo, mifupa na masalia mengine, naamini herufi zilikuwepo labda hazikuwa na mkalimani au zilikosa maana hivyo hata hazikutunzwa kabisa.
Still naomba mwenye kufahamu tujuzane.
 
Fanya utafiti ubuni herufi zako na ikiwezekana anza na kabila lako, utapata u-professor kiulaini.
Hahaha, u professor naupenda, lakini nikubali mimi sio mtaalam wa mambo ya kale sio mtaalam wa lugha hivyo siyo mtu sahihi kwa hilo.
Wenye taaluma yao hii inaweza kuwa chachu kuanza kufukua data au kukusanya wakaja na bonge la thesis na wakalijaza nyama na kulitetea tukapata kitu chetu. Hamu yangu ni kupata herufi zetu najua kutengeneza sauti na matumizi inaweza kuwa ngumu kwa leo, lakini kuwe na kumbukumbu hata kwenye makaratasi.
Nimewahi kuona program moja sijui ni discovery channel mtu anaongea lugha iliyopotea na yuko peke yake dunia nzima, lugha inajulikana jina lakini wazungumzaji kabaki mmoja na ni mzee sana.
Ni moja ya makabila ya kale huko kwa red indian marekani. Lakini documentary ipo.
Hata hapa watu hawajifunzi native language zao hivyo kupunguza idadi za watumuaji kwadababu hasa za kiuchumi. Maana kufahamu kikurya au kinyakyusa leo hakuna faida zaidi ya kuongea. Uchumi umekuwa determinant factor kubwa, mtu atakuuliza kwanini nijifunze kihaya?!
Kwa mwendo huo tutabaki na majina ya makabila lugha zitapotea. Hatuziandiki na hatuzitunzi.
 
Kama kungekuwa na aina ya uandishi, leo hii ungekuwepo kule Cameroon kabla ya kifaransa.

Asili ya Wabantu ni Cameroon.

Wale wachache wasio wabantu kama waethiopia na wamisri wa zamani wana aina yao ya uandishi na Lugha yao complete kama kiaramaic.

Wamasai sio wabantu ni nilotes na wana uhusiano mkubwa na waethiopia, wamasai halisi wana gestures inayotambulisha namba zooote kuanzia enzi na enzi.

Huoni Wabantu wanatafuniwa kiiila kitu, hata herufi rasmi ya kilugha hakijawahi kugunduliwa na kabila lolote lenye asili ya kibantu.
Mkuu naweza kuwa nimetoka nje ya mada. Hili la wabantu kuanzia kameroon nami limenipa tashwishi ya kufahamu. Ulimaanisha wabantu wote tuli originate hapo kameroon?! Kivipi?! Inamaana bara zima hili hapo kale halikuwa linakaliwa na watu?! Vipi kuhusu wale anthropologist wanaodai fuvu zee kuliko yote afrika liligunduliwa huko oldivai gorge, kwanini haikuwa huko kameroon?! Ufafanuzi kidogo mkuu, huu ubantu wetu na watafiti wanaweza kuwa wanalisha matumbo yao kwa kuandika uongo, na kwakuwa hakuna ushahidi wa kuwapinga tukawa tunaeleweshwa ndivyo sivyo. Msaada kwenye tuta ukipata muda mkuu. Shukrani
 
Kwani una uhakika fuvu la mtu wa kwanza lilikuwa la Mbantu?

Asili ya wabantu ni katika milima ya cameroon mkuu. Huku kwingine walikuwepo waethiopia miaka miingi na walishaendelea kabla hata ya hao Wabantu na ni kulingana na vyanzo vingi vya taarifa na habari.

Ukija kwa upande wa Afrika ya kaskazini nchi zake kama Libya ilikuwepo tangu enzi za utawala wa Roma na warumi ndio waliilocate na kuipa jina Libya.

Kule Egypt ndio kabisaa walishakuwa mbali mno.

Nchi pekee ya watu weusi iliyokuwa na historia nzuri katika karne ya 13 huko ni Mali wakati wa Mansa Mussa na sundiata Keita lakini pia hao walitajirishwa na waarabu katika biashara na hata katika system ya uongozi.
 
Habari zenu wana bodi.
Huwa najiuliza maswali lakini sipati majibu lakini leo naomba nanyi mnisaidie.
Tanzania tuna makabila mengi na haya makabila yanaongea lugha tofauti. Lakini pia tunaongea kiswahili. Swali langu ni hili ilikuwaje tuweze kuongea lugha tofauti lakini tukashindwa kuwa au kuweza kuandika hizi lugha zetu kwa HERUFI zetu?! Yani makabila yote tulijua kuongea lakini hakuna hata kabila moja liliweza kuwa na herufi za maandishi yake?! Angalia Ethiopia wana herufi zao,wahindi wana herufi zao,wachina wana herufi zao, warusi wana herufi zao,sweden wana herufi zao waingereza wana herufi zao. Sisi Tanzania tulishindwa au tulitegemea ugunduzi wa wazungu kutuwekea vitu vyetu kwenye kumbukumbu na kwakuwa hawakuziweka kumbukumbu inamaana hatukuwa na herufi zetu kweli?!
Je, tunaweza kutengeneza herufi zetu leo au ugunduzi uliishafungwa?! Ikiwa tunaweza kugundua leo, je kumeshawahi kufanyika utafiti wa kuanza kutengeneza herufi zetu au ugunduzi ni wa kiteknelogia tu lakini sio maandishi(herufi)?!. Kwa wataalam wa tafiti za lugha kumewahi au wamewahi kuona herufi zozote za kuwakilisha maandishi ya kabila lolote Tanzania?! Je kuna wataalam wale wanaoitwa ma anthropologist wa lugha?! Je wamewahi kutafiti herufi za kuwakilisha mawasiliano ya kimaandishi ya lugha yoyote ya makabila yetu Tanzania?!
Kwa BAKITA kiswahili tunaweza kukiundia herufi zetu mbali ya hizi A to Z?! Je kuna juhudi hizo au mnakuza lugha tu herufi zina mamlaka yake?!
Ni mjadala wa wote kwa yeyote anayejua chochote kuhusiana na hili. Karibuni kwa mjadala.
Mafwi Munda maswali yako ni mazuri sana na yenye kuamsha ari ya kujifunza zaidi.
Lakini kabla sijaenda mbele naomba nikurekebishe kidogo kuwa si kila lugha duniani ina maandishi yake ni lugha chache sana hata hicho kiingereza ulichokitaja herufi hizo c zake ni herufi za lugha zingine(imerithi) sina hakika sana lkn nahsi ni kutoka lugha ya kilatini au zenye asili ya kilatini km vile kihispania n.k

Ugunduzi wa maandishi ktk jamii nyingi uliendana na ukuaji wa ustaarabu wa jamii hizo za kale (ancient World civilization) hata hivyo vita na ubabe wa kuporana miliki na madaraka ulisababisha baadhi ya jamii kupoteza historia na utamaduni wao.

Zipo baadhi ya jamii zilihifadhi historia yao kwa michoro(sawa na kusema maandishi) hata hivyo alama hizo zilipotea kutokana na sababu nilizotaja hapo awali na zilizobakia zilishindwa kuelezeka/kutafsirika kwa sababu ama za ukosefu wa ujuzi miongoni mwa watafiti hao au sababu za kibaguzi(bias)

Ikumbukwe kuwa historia ya mtu mweusi imeandikwa na mtu mweupe ambaye kwa miaka mingi amejitahidi kuonesha kuwa mtu mweusi hana historia wala ustaarabu wowote ule.

Lakini hatujachelewa yawezekana wazo lako likaingia mikononi mwa wasomi wetu.

Mkazamoyo.
 
Back
Top Bottom