Mafwi Munda
JF-Expert Member
- Nov 30, 2017
- 1,750
- 1,599
- Thread starter
- #41
Asante mkuu kwa marekebisho, na maelezo yako. Nia yangu nikujifunza hivyo napokea maelezo yako mkuu.Mafwi Munda maswali yako ni mazuri sana na yenye kuamsha ari ya kujifunza zaidi.
Lakini kabla sijaenda mbele naomba nikurekebishe kidogo kuwa si kila lugha duniani ina maandishi yake ni lugha chache sana hata hicho kiingereza ulichokitaja herufi hizo c zake ni herufi za lugha zingine(imerithi) sina hakika sana lkn nahsi ni kutoka lugha ya kilatini au zenye asili ya kilatini km vile kihispania n.k
Ugunduzi wa maandishi ktk jamii nyingi uliendana na ukuaji wa ustaarabu wa jamii hizo za kale (ancient World civilization) hata hivyo vita na ubabe wa kuporana miliki na madaraka ulisababisha baadhi ya jamii kupoteza historia na utamaduni wao.
Zipo baadhi ya jamii zilihifadhi historia yao kwa michoro(sawa na kusema maandishi) hata hivyo alama hizo zilipotea kutokana na sababu nilizotaja hapo awali na zilizobakia zilishindwa kuelezeka/kutafsirika kwa sababu ama za ukosefu wa ujuzi miongoni mwa watafiti hao au sababu za kibaguzi(bias)
Ikumbukwe kuwa historia ya mtu mweusi imeandikwa na mtu mweupe ambaye kwa miaka mingi amejitahidi kuonesha kuwa mtu mweusi hana historia wala ustaarabu wowote ule.
Lakini hatujachelewa yawezekana wazo lako likaingia mikononi mwa wasomi wetu.
Mkazamoyo.