Lugha za upendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lugha za upendo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 5, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  [h=3]Lugha za upendo[/h]

  Wakati mwingine ukikosa kuguswa unapata "skin hunger"[​IMG] MGUSO (physical touch)
  Kukumbatia, kubusu, kushikana mikono na sex (ktk ndoa) ni njia ya mawasiliano ya hisia za upendo au kupendwa.
  Watafiti wengi hasa wa maendeleo ya watoto wamethibitisha kwamba kukumbatia, kumbusu na kumshika mtoto kunampa afya njema kihisia.
  Kuguswa ni kitu muhimu sana katika mawasiliano ya ndoa hasa linapokuja suala la mahaba, kwa kushikana mikono, kubusu, kukumbatiana na kutekenyana kule kunakonyegesha huleta raha sana kwa mke na mume.

  Inawezekana mume wako au mke wako kwake kupendwa ni kukumbatiwa au kupata busu kabla hujaondoka asubuhi na unapokutana naye tena baada ya shughuli za kujenga familia au kutembea mmeshikana naye mikono, pia inawezekana kwako ni jambo gumu na unaona kama ushamba fulani hivi au ulimbukeni.
  Jambo la msingi fahamu kwamba kila mmoja wetu ana aina ya kujisikia anapendwa na ni kitu kidogo lakini kinaweza kufanya ndoa au mahusiano yako kuwa matamu au machungu.

  Unaweza kutumia muda mwingi kumpikia chakula kitamu, au kununulia mizawadi ya gharama, hata hivyo kama mwenzi wako kupendwa ni kupokea mguso wa kimwili bado zawadi zako hazitamkuna vizuri kama ungempa mguso wa kimwili.
  Ktk milango ya mitano fahamu, kugusa ndiyo peke yake kunahusisha mwili mzima ingawa kuna sehemu zingine zikiguswa ni balaa zaidi na zinahusisha watu walio katika ndoa tu.
  Kuona tunatumia macho, kunusa tunatumia pua, kusikia tunatumia masikio, kuonja tunatumia ulimi lakini kugusa ni mwili mzima.

  Sex ni physical touch, ndiyo maana kuna wanawake au wanaume bila kumpa sex anaona bado humpendi hata kama utamnunulia gari au kumpeleka vacation North pole hata hivyo hapa tunazungumzia sex ndani ya ndoa na si vinginevyo.
  Mwili ni kwa ajili ya kuguswa,
  Unaonaje mtu akigoma kukusalimia mikononi?
  Naamini utatambua kwamba kuna mushkeli.Inawezekana mume wako au mke wako kupata mguso wa mwili ni lugha yake ya msingi kuonesha unampenda na anategemea utamgusa mwili wake kila siku kwa kutekenya nywele zake, au kutembea umemshika mkono au kumpa busu na kumkumbatia kila unapoondoka home asubuhi au unaporudi na pia kumpa romance ya uhakika kabla ya sex mkiwa faragha,

  KUSAIDIANA KAZI
  Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe na yeye ni kitu kimoja.

  Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.

  Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

  Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako kazi hasa mwenzi ambaye kwake kupendwa ni kusaidiana kazi.

  MANENO YA SIFA
  (Kusifia, kutia moyo na kushukuru)
  Je ni mara ngapi umesema Asante au kumsifia spouse wako kwa jinsi alivyofaanya kitu ambacho kilionekana kizuri?
  Na je kawaida unapomsifia au ku-appreciate vitu anafanya huwa anajisikiaje?
  Hayo maswali ni ya msingi sana mtu kujiuliza hasa kama unataka kujua mwenzi wako kwake maneno matamu ndiyo KUPENDWA.

  Maneno mazuri au yanayotia moyo au yanayomsifia ambayo ni matamu husababisha mambo yafuatayo kwa mwenzi wakoHuleta upamoja na ukaribu zaidi (intimacy)Huleta uponyaji kwenye majeraha ya hisia zake kama kuna maumivu moyoni mwake (healing) na kumfarijiMwenzi hujisikia kulindwa zaidi na anajisikia yupo katika mikono salama.

  Fahamu kwamba wewe ndiye mtu muhimu kuliko mtu yeyote duniani kwake, hivyo maneno unayoongea either yanamjenga au yanambomoa na si kubomoa tu bali na kumuumiza na unampa wakati mgumu.
  Lengo la upendo si kulalamika kwa kile ambacho hupati
  bali ni kufanya kile ambacho kitamsaidia yule unayempenda,
  yule umechagua uishi naye hadi kifo kitakapowatenganisha.

  Mojawapo la hitaji kuu la ndani la mwanadamu ni kuwa appreciated na kile mtu anafanya.
  Je umewahi kuwa na boss mkali na mwenye maneno ovyo na mtu wa amri?
  Huwa unajisikiaje?
  Fikiria unaishi na mke au mume wa aina hiyo.

  Nami mwenzi wangu yupo kwenye hili kundi, kwake kumpenda ni pamoja na kumpa appreciation ya yale anafanya hadi jinsi anavyovaa, mwanzo wa ndoa ilikuwa ngumu kujua ila nilishangaa ananiambia mbona wenzako wananiambia nimependeza na wewe husemi chochote?
  Kwa kutojua nilikuwa namjibu “ndiyo maana nilikuoa ni kweli unampendeza na hilo najua.

  Hata hivyo sasa nimejifunza kusema asante na kumshukuru na kumpa sifa kwa kila anachovaa hata akivaa akapendeza nakuwa mtu wa kwanza kumwambia bibie leo umependeza na unawake.

  Tutaendelea!
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  [h=3]Lugha za Upendo[/h]

  Love is the most powerful weapon for good in the world.[​IMG] Wakati mwenzi (Spouse) wako anajisikia kuridhishwa kimapenzi (emotionally na romantically) hujisikia salama kihisia na hujiona ulimwengu unampa vyote na matokeo yake hujitoa zaidi kuhakikisha anajiweka katika kiwango cha juu kwako kuimarisha upendo na mahusiano kwa ujumla.

  Na anapojisikia kutoridhishwa kabisa kimapenzi, hujisikia mweupe, empty na kama vile anatumika au unamtumia tu kufanikisha na kutimiza hitaji lako la mapenzi.

  Moja ya tatizo kubwa katika kuonesha upendo (love) tumeshindwa kufahamu kwamba mke na mume huongea lugha tofauti za upendo.
  Kila mmoja huwa na namna tofauti jinsi anavyojisikia unampenda kwa mfano mwingine ukimpa zawadi yoyote hujisikia unampenda na ukimsifia anaona ni maneno matupu na mwingine ukimsifia basi hujiona raha na hujisikia unamthamini na kumpenda.

  Kuonesha upendo kuna lugha kama zilivyo lugha za mawasiliano na utamu wa lugha ni pale unapoifahamu kwa kuisikia na kwa kuiongea, pia utamu wa upendo katika ndoa au mahusiano ni pale unapofahamu lugha ya upendo kati yako na mpenzi wako.

  Itakuwa vigumu sana kwa anayejua kibena kuanza kuongea na anayejua kimasai na wote wakawa wanadhani inawezekana.
  Kumbuka Babeli haikujengwa ikaisha kwani baaada ya lugha kuharibiwa kila kitu kilisambaratika.

  Kimsingi ili kuelewana na mpenzi wako kuna lugha za msingi tano ambazo kati ya hizo moja wapo inaweza kuwa ni maalumu kwa ajili ya mpenzi wako na kuifahamu au kuzifahamu lugha zake basi unaweza kujenga mahusiano imara.

  Hata hivyo mahusiano bora huanza kwanza na Hofu ya Mungu (Christ in you)
  Lugha tano muhimu ambazo mara nyingi wapendanao hutumia ni:
  1. Kuwa na muda na mwenzi wako (Quality time)
  2. Kupeana zawadi (Receiving gifts)
  3. Kusaidia kazi (Acts of services)
  4. Kumpa maneno ya kumsifia, kumtia moyo kwa kile anafanya (words of Affirmation)
  5. Mguso wa kimwili (physical touch)

  KUWA NA MUDA NA MWENZI WAKO
  (Quality time)
  Msingi wa kuwa na muda na mwenzi wako ni upamoja (togetherness) pamoja na kuwa kimawazo, kimwili na kiakili.
  Kukaa na kuangalia TV pamoja si kuwa na muda na mwenzi wako kwani hapo mnaipa TV qulity time.
  Kuwa na muda na mwenzi wako ni kukaa pamoja na kumpa attention yote, anaongea na wewe unamsikiliza tena ninyi wawili tu. Ni kutembea pamoja yaani mmeamua kwenda kutembea kwa ajili ya kwenda kutembea wewe na yeye tu si kwa sababu mnaenda kanisani au mnaenda kazini.

  Kupeana muda wa pamoja ni kama vile kwenda kula pamoja (outing) ninyi wawili na mkifika hapo kwenye hoteli mnaongea kwa kuangaliana ninyi.

  Kama mpenzi wako yupo kwenye hili kundi yaani kwake kupendwa ni kuwa pamoja basi ni dhahiri ukifanya haya mara kwa mara anatajisikia raha sana na atajisikia unampenda sana.

  Hata hivyo kama mpenzi wako kwake lugha ya upendo ni zawadi ataanza kulalamika why unakuwa na mimi tu muda wote hata zawadi huniletei?
  Maana kwake kupokea zawadi ndo kuonesha unampenda na si kufuatana kila mahali.

  KUPEANA ZAWADI
  (Receiving gifts)
  Zawadi ni kitu chochote unachoweza kukishika kwa mikono na kinakupa hisia kwamba aliyenipa zawadi alikuwa ananifikiria na ananipenda.
  Zawadi huelezea upendo kwamba alikuwa ananiwaza na kuniona mtu wa maana sana kwake.

  Wanandoa wengi hupuuza na kuona kwamba zawadi siyo kitu muhimu ktk mapenzi, pia wapo wengine hudhani zawadi kwa mpenzi hadi kiwe kitu kikubwa kama gari au nyumba, vitu vidogo sana kama pipi, Chocolate au maua ni zawadi za msingi sana na zina maana kubwa sana katika kuimarisha mapenzi katika ndoa.
  Nahisi hata wewe msomaji ulikuwa maarufu sana kutoa zawadi wakati wa uchumba na sasa umeacha, Bisha!

  Zawadi muhimu pia ni wewe kuwepo au kupatikana pale mke wako au mume wako au mpenzi wako anakuhitaji anapokuwa na shida (wapo wakiona shida hukimbia wapenzi), uzoefu inaonesha zawadi hata za kutoa muda wako hukaa ktk kumbukumbu za mhusika kwa miaka mingi bila kusahau na pia huongeza level ya mapenzi kwako.

  Inawezekana mke wako au mumeo ni watu ambao akipewa zawadi basi yeye ndo kupendwa yaani ndo anaguswa zaidi, moyo wake unaamini ukipewa zawadi ndo unapenda.
  Kama mpenzi wako kupewa zawadi ndo lugha yake ya upendo basi ikitokea wewe unampa sifa kwa mambo mazuri anafanya usishangae akikwambia punguza maneno zawadi zipo wapi? Atakwambia anataka matendo si maneno!

   
 3. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Thanks Pdidy..mimi nina-conclude

  Upendo = Vitendo
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Yaaaaaaaaaaani weeeeeeeeeeeee umenena ubunge ungekuwa kubadilishana ningemtoa shibuda nikugaie
   
 5. giningi

  giningi Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  p did,leo utakuwa ulishukiwa na roho mtakatifu kuandika hii thread sio bure,ubarikiwe sana ,namtumia shemejio sasa hivi!
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hilo nalo neno.
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  nashukuru mkuu tuombbeane ila vyema ukaiombea kwanza kusoma wamesoma meng kama mwananchi na dar leo na leo kunaendelea kuwaka moto Mungu ampe ufahamu asomapo hiyo
  ubarikiwe kaka
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  KUSAIDIANA KAZI
  Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe na yeye ni kitu kimoja.

  Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.

  Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

  Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako kazi hasa mwenzi ambaye kwake kupendwa ni kusaidiana kazi.  hili nimeipenda sana sana sana na imenikumbusha wakati wife akijifungua housgirl akala kona
  nikaanza kufua nepi na yale mavi meusi si mnajua tunaanza ga huko ndio tunakuja
  brown mara kijani..nilifua nepi mpaka mkwe akaogopa ..sasa hivi mwanangu kila nikiamka saa 0530 am lazima
  nimvue pampas nimsafishe mamake akiamka kila siku anakutana na mpya aijalishi muda gani tumika pale unapoweza
  ipo siku utatamani na utopata muda wa kufanya hivyo
  Mubarikiwe
   
 9. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Cool....!!!! Nice One...
  Actions Speaks Louder than Words
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  KUSAIDIANA KAZI
  Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe na yeye ni kitu kimoja.

  Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.

  Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

  Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako kazi hasa mwenzi ambaye kwake kupendwa ni kusaidiana kazi.  imenikumbusha sana mbali wakati mwanangu anazaliwa hgirl akla kona ikabidi nianze kuosha nei na yale mananii meusi
  mpaka brown mara green sijui mwishoni ni blue ama..basi nilipiga maji nepi mpaka raha mkwe akawa anataka kusafisha nikwamambia
  mwanangu nimemtafuta mwenyewe nishindwe kuosha nepi zangu weeee
  Kingine mkiamka asbh wazee mapema angalien watoto wenu wavuen pampas kama anatumia bado msafishe atakatake mama akiamka
  anashangaa mtoto safi..m mwanangu mpaka leo akiiwa anawashwa anataka abadilishwe pampas usiku anabingirika mpaka kwa baba anaweka
  miguu yake kwenye mgongo unajua kumekucha ....somo tu jiandae uzazi sio kubadilisha chupa za kilimanjaro
   
 11. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133


  noted with thanks
   
 12. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  ujumbe wako ni mzuri sana, asante sana.
  Mwenye macho ameona, mwenye masikio amesikia na kuyafanyia kazi kama siyo jana,
  basi leo, na kama siyo jana wala leo , basi hata kesho yatafanyiwa kazi.a
   
 13. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  jaman pdidy umenikuna sana leo
   
Loading...