Lucky Dube: Miaka kumi(10) tangu auawe

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
Lucky Dube anatimiza miaka 10 tangu auwawe kwenye eneo la Rosettenville, Johannesburg, Afrika Kusini. Hii ilikuwa tarehe 18/10/2007.

Dube aliyeuwawa akiwa na umri wa miaka 43, alizaliwa sehemu inayojulikana kama Ermelo, Transvaal (kwa sasa Mpumalanga) mwaka 1964, Augusti, 3. Wazazi wake walitengana kabla ya kuzaliwa kwake na aliishi na mama yake ambaye alimpa jina la LUCKY kwa maana ya bahati; hii ni kutokana na mimba kadhaa kuharibika, hivyo kuzaliwa kwa Lucky Dube ilionekana kama ngekewa au bahati.

Pamoja na ndugu zake wawili Thandi na Patrick, Dube alitumia muda wake mwingi wa utotoni akiishi na bibi yake aliyejulikana kwa jina la Sarah wakati mama yake alipokwenda kazini. Mwaka 1999 kwenye moja ya interview yake, Dube alimuelezea bibi yake kama 'kipenzi chake kikubwa' ambaye alifanya kazi kubwa ya kumlea, na kumkuza Dube.

Kuanza Muziki

Katika umri wa utotoni, Dube alifanya kazi kama mtunza bustani na kadiri alipokuwa akikua, aligundua kuwa kipato alichokuwa akikipata hakikutosheleza kuilisha familia yake, ndipo Dube alianza shule. Katika mazingira ya shule alijiunga na kikundi cha muziki kilichoitwa The Skyway Band. Alijifunza na kufuata imani ya kirasta akiwa shule, na alipofikisha umri wa miaka 18 Dube alijiunga na kundi la muziki la binamu yake lililojulikana kwa jina la The Love Brothers, ambalo lilipiga muziki wa Kizulu aina ya mbaqanga. Akiwa na kundi hilo, waliweza kuingia mkataba na kampuni ya muziki Gallo Music, kampuni kubwa kabisa huko Afrika Kusini.

Dube, alivutiwa zaidi na muziki wa Jimmy Cliff na Peter Tosh toka Jamaica, na ndipo safari yake ya kuimba muziki wa reggae ilipoanzia. Mwaka 1984, alirekodi album yake ndogo ya reggae iliyokwenda kwa jina la Rastas Never Die, hata hivyo album hiyo haikufanya vizuri sokoni ambapo iliuza nakala 4000 (elfu nne) tu ukilinganisha na mauzo yaliyofanyika kwenye muziki wa mbaqanga ambapo aliuza hadi nakala 30,000 (elfu thelathini). Akiwa mwenye shauku kubwa ya kupiga vita ubaguzi wa rangi (ant-apartheid), kupitia muziki na tungo zake mbalimbali, serikali ya kibaguzi ya wakati huo ilipiga marufuku album yake mwaka 1985 kutokana na mashairi ambayo yalionekana kuikosoa serikali ya kibaguzi. Hakukata tamaa, kwani mwaka huo huo wa 1985 aliendelea kuimba muziki wa reggae na aliweza tena kurekodi album yake iliyoitwa Think About The Children iliyompa mafanikio makubwa kwa kuuza nakala na kufikia hadhi ya mauzo ya platinam na kumpaisha na kuwa moja ya wanamuziki maarufu zaidi huko Afrika Kusini na nje ya Afrika Kusini.

Mafanikio

Dube aliendelea kutoa album za reggae ambapo mwaka 1989 alishinda tuzo ya OKTV kwa album ya Prisoner, tena akashinda tuzo kutokana na album ya Captured Live (iliyotokana na onesho la moja kwa moja). Mwaka uliofuata alitoa album ya House of Exile. Mwaka 1993 album yake ya Victims, iliuza zaidi ya nakala milioni moja duniani kote. Mwaka 1995 alipata mkataba wa kurekodi na Motown moja ya makampuni makubwa kabisa nchini Amerika, ambapo Trinity ndiyo album ya kwanza kurekoodiwa na kampuni hiyo. Dube inaaminika kuwa ndiye mwanamuziki bora zaidi toka Afrika kusini, na miongoni mwa wanamuziki wachache toka bara la Afrika kufanya vizuri katika soko la kimataifa. Pia kutokana na kukubalika hadi nje ya Afrika, moja ya wimbo wake unaojulikana kama Victims, toka album iliyobeba jina hilo VICTIMS, ulifanyiwa marudio (cover) na mwanamuziki wa reggae nchini Jamaika anayeitwa Anthony B.

Mwaka 1996, alitoa album mjumuisho iliyokwenda kwa jina la, Serious Reggae Business, ambayo ilifanya awe muuzaji bora na kutajwa kama mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa wakati wa utoaji wa tuzo za World Music Awards kadhalika kama mwanamuziki bora wa kimataifa kwenye tuzo za Ghana Music Awards. Album zake tatu zilizofuata zilifanya ashinde kwenye tuzo za South African Music Awards. Album yake ya hivi karibuni, Respect, ilisambazwa na kampuni ya Warner Music. Dube amezunguka dunia aki-perform na wanamuziki kama Sinéad O'Connor, Peter Gabriel, Celine Dion, Ziggy Marley na Sting. Mwaka 1991 aliweza kushirki tamasha kubwa zaidi la reggae sunsplash huko Jamaika ambapo aliombwa arudie tena kutokana na umahiri wake na upekee wa aina yake kama mwanamuziki toka barani Afrika.

Kifo chake

Mnamo tarehe 18/10/2007, Lucky Dube aliuwawa jijini Johannesburg kwenye kitongoji cha Rosettenville muda mfupi baada ya kuwashusha watoto wake wawili karibu na nyumba ya ndugu yake. Dube alikuwa akiendesha gari yake ya kifahari aina ya Chrysler 300C, ambayo waporaji walikuwa wakiitaka. Wauaji hao, katika kujitetea, walidai hawakujua na kugundua kuwa aliyekuwa akiendesha gari hiyo alikuwa Lucky Dube bali walijua alikuwa ni Mnigeria. Watu watano walikamatwa kuhusiana na mauaji hayo na walipatikana na hatia hivyo walihukumiwa kifungo cha maisha tarehe 31 Machi 2009. Wengine wawili walifanya jaribio la kutoroka lakini walikamatwa na wote wanatumikia kifungo cha maisha. Mtandao wa mwanamuziki maarufu toka Jamaika, na mfalme wa reggae duniani, hayati Robert Nesta Marley maarufu kama Bob Marley (www.bobmarley.com) pia ulihabarisha dunia juu ya kifo cha Lucky Dube miaka kumi (10) iliyopita, hii inatoka na jinsi alivyoheshimika hata huko Jamaika ambako reggae ndiyo asili yake.

Hadi umauti unamfika, Dube alirekodi album 22, na ni moja ya wanamuziki wenye mafanikio makubwa zaidi toka barani Afrika. Katika uhai wake, pia aliwahi kufanya ziara nchini Tanzania mwaka 1997 na kumtania mtangazaji maarufu sana wa wakati huo wa kituo cha televisheni cha CTN Rahma Azizi kuwa alimpenda na angependa amuoe na kwenda naye Afrika Kusini. Tofauti na wanamuziki wengine wa reggae, Lucky Dube hakuwa mtumiaji wa marijuana au bangi tofauti na uchangamfu wake mkubwa jukwaani, ila kama ilivyo kwa wanamuziki wengine wa reggae hasa wenye imani ya kirasta, Lucky Dube alikuwa mtu mkarimu sana kwa jamii na mtu aliyejishusha licha ya umaarufu wake mkubwa duniani kote na licha ya mafanikio makubwa aliyokuwa nayo.

Lucky Dube atakumbukwa zaidi kwa nyimbo zake kama vile, Together As One, Prisoner, Reggae Strong, Different Colours One People, Remember Me, My Brother My Enemy, Serious Reggae Business, Reggae Strong For Peace, God Bless The Women, Trinity, The Way It Is, Victims, na nyinginezo nyingi.

Makala hii imetafsiriwa na imeandaliwa kwa msaada wa: mtandao wa wikipedia Lucky Dube - Wikipedia
Picha kwa msaada wa mtandao.
RememberingDube.jpg


Murdered reggae legend mourned - CNN.com
 
Nikiambiwa nitaje nyimbo zake bora nashindwa niiweke ipi, na ipi niiache. Yaani kati ya wanamuziki ambao sichoki kuwasikiliza ni Lucky Dube, Celine Dion na Koffi Olomide.
Ngoja kwa kumbukumbu yake, kesho baada ya gospel mbili tatu nitiririke na nyimbo zake siku nzima huyu mwana wa Afrika, rafiki wa Wapenda haki duniani. Mungu ampumzishe The Reggae Icon kwa namna anayoona inampendeza.
 
Huyu msanii anajulikana kweli huko migombani Moshi, yaani unakuta mzee wa kichaga anaomba, aitwe mekuuu, bon tu safaaaaa hadi unashangaa
 
Mkuu ukisoma haya mashairi utagundua kitu

Lucky Dube Lyrics

"Good Things"

There will be a time in your life
When you'll need me the most
But I won't be there
There will be a time in your life
When you won't need me at all
I won't be there
But while I've got the chance
I'm gonna tell you what I know
About this world we're living in
It may seem so beautiful
From where you are
It may look so innocent
In your eyes
But let me tell you
It's not a bed of roses

[Chorus: x3]
Good things come to those
Who got out and made them happen
They don't come to those who wait

I can sit here and teach you
Every trick in the book
But at the end of the day
It is your life

[Chorus: x3]
Good things come to those
Who got out and made them happen
They don't come to those who wait

You don't have to worry
The future is in your hands
[Till fade]
 
Back
Top Bottom