Lowassa una tatizo

Lowassa una tatizo

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,868
Reaction score
5,753
Nimeichukua kama ilivyo.

LOWASSA UNA TATIZO


Na Happiness Katabazi

LEO Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Katika Viwanja Vya Jangwani Dar Es Salaam. Na ukweli kampeni za UKAWA zimefana hongereni sana.

Nimefuatulia kwa makini Uzinduzi huo mwanzo hadi mwisho kupitia Kwenye Televisheni.

Nimewasikiliza wote waliopewa nafasi ya kuzungumza na wamezungumza waliyozungumza hata Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye nimemsikia yote aliyoyasema licha yote aliyoyasema Sumaye siyo mapya.

Lakini wenye akili timamu tunayapuuza yote aliyoyasema Sumaye Leo kwasababu Sumaye ambaye amewahi kugombea urais mara mbili kupitia CCM na hakufanikiwa.

Enzi akiwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu aliwahi kusema "UKITAKA BIASHARA ZAKO ZIKUNYOKEE VIZURI UJIUNGE NA CCM". Hadi sasa Sumaye hajafuta Kauli hii ambayo ilizua mjadala Mkali nchini.

Nirudi Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo.

Mada hiyo nitajadili uamuzi wa Mgombea Urais wa CHADEMA kwa muunganiko wa UKAWA, Edward Lowassa Leo saa 11 jioni alipopanda jukwaani kuanza kuhutubia alisema ameishauriana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Kuwa asisome hotuba yake ya Uzinduzi wa kampeni hiyo kwasababu eti muda umekwenda na Polisi wa Dar Es Salaam, hawampendi kabisa kwahiyo eti wakizidisha muda Polisi hao watapata Sababu.

Kwasababu hiyo eti Mbowe na viongozi wengine wamemshauri asiisome hiyo hotuba ndefu badala yake hiyo hotuba itawekwa Kwenye Website ili wananchi waisome.

Jamani , hivi huyu Lowassa yupo Siriazi kweli ?Lowassa hayupo Siriazi kuutaka urais wa Tanzania.

Leo Ndio ilikuwa siku rasmi ya Lowassa ambaye ni mgombea urais kuja Uwanjani kueleza wananchi atayafanyia nini kupitia Katika kinywa Chake na kuwaomba kura wananchi .

Lakini Lowassa Hilo Leo limemshinda kashindwa kueleza kwa wananchi atayafanyia nini na mipango ya serikali yake akafanikiwa Kuwa rais itakuwa ni ipi kwa Sababu dhahifu kabisa.

Mgombea urais kabisa bila aibu Katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni yako bila aibu na woga unasema eti hutasoma hotuba yako badala yake Utaiweka Kwenye website?

Tumuulize huyu Lowassa ambaye amekuwa akijigamba Kuwa anachukizwa na umaskini na amekuwa akiwa tembelea watu wa Haki ya chini Kwenye masoko .

Sasa Nimuulize hao masikini ambao hawana simu za Smartphone wataweza kuisoma hiyo hotuba yake kupitia website?

Jibu ni Jepesi Watanzania Wengi hawataisoma hiyo hotuba yako kwa Sababu hata hela za kuweka Bando Kwenye simu hawana uhakika wa kuzipata.

Sasa ikitokea wasikupigie kura za Ndio kwasababu umeshindwa kusimama jukwaani kunadi sera zako utakapoingia Ikulu utawafanyia nini utakuja Kulalamika umeibiwa kura?

Maana hata unapotaka Mwanamke kimapenzi lazima usemezane naye ,umwage sera zako ili akakubali au aukataee wewe Leo Lowassa Hilo limekishinda la kututongoza wananchi wenye akili timamu ili tu kuipigie kura kwasababu dhahifu?

Kama Mbowe na viongozi wenzake walijua muda ni Mdogo, kwanini wasinge panga Ratiba ikaanza mapema ili upate muda mrefu wa kusimama jukwaani usome hotuba yako?

Lowassa unataka kutuchezea akili, yaani unataka tukupe urais wakati umeshindwa kusoma hotuba ya ufunguzi wa kampeni zako?

Kama ulishauriana na viongozi wa UKAWA usisome hotuba yako ,sasa kulikuwa na maana gani ya kufanya mkutano huo Leo ?Simngeweka hiyo hotuba Kwenye Mtandao tukajua Moja.

Hilo limekushida,Je ikitokea ufanikiwe urais wa Tanzania, licha naamini huwezi kufanikiwa kupata nafasi hiyo unaweza kwenda Umoja wa Mataifa na Kusimama Mbele na kusoma hotuba au mhadhara kwa Niaba ya Tanzania zaidi ya saa Moja?

Kwanza Ulipaswa uonyeshe kwa vielezo Kuwa ni kweli Polisi Dar Es Salaam wanakuchukia na wanakuchukia kwasababu gani? Lini walianza kukuchukia?

Polisi wakikukataza kisheria kufanya ziara zako ambazo zinahatarisha Usalama wako na kuleta Usumbufu Katika Jamii ndiyo wanakuchukia?

Lowassa wewe ni kiongozi wa ajabu sana na unageuka kuchekesha Mbele ya watu tunaofikiri sawa sawa.

Leo umetumia dakika nane jukwaani kuzungumza mambo ambayo siyo mapya ,jipya nililoliona ni lile la kumshukuru aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani,Fredrick Sumaye eti amefanyakazi nzuri sana ya kuwapa vidonge vyao serikali ya CCM.

Hili Mimi Ndio nimeliona jipya kutoka mdomoni mwako kwasababu umemsifia aliyekuwa hasimu wako wa kisiasa Sumaye.

Na pia nimeliona jipya pia kwa mdomo wa Sumaye kutoa maneno ya kujisafisha wewe Lowassa Kuwa ni Msafi wakati ni Sumaye huyu huyu alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanakupiga vijembe.

Sielewi kabisa ni kwanini watu wazima Mmekuwa na tabia za kinafki mna misimamo inayoyumbayumba na ya msimamimii maneno yenu?

Itoshe Kusema tu kwa nilichokiona Leo nimeitimisha kwa Kusema mkutano wa Leo wa UKAWA ulikuwa Una sura mbili.

Sura ya kwanza ni ya Uzinduzi wa Kampeni na sura ya pili ni Sumaye kutumika kurusha makombora Moja kwa Moja kwa Rais Jakaya Kikwete na serikali na CCM.

Na kweli Sumaye amefanyakazi hiyo kikamilifu ya kurusha vijembe Kwani watu walikuwa watu livu sana wakamsikiliza na kushangilia licha Lowassa Katika zile dakika zake wakati akizungumza watu baadhi ya wananchi walikuwa hawamsikilizi Kwani walikuwa wakiondoka uwanjani hapo.

Yaani mgombea Urais kabisa wa UKAWA, huyu Lowassa anasimama jukwaani anasema eti akiwa Rais Atalishughulikia Kesi ya Babu Seya,kuwaachiria huyu Masheikh wa UAMSHO Sheikh Farid na wenzake ambao wapo gerezani,elimu ya Darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu Bure. Kwa hiyo hayo yapo ndani ya Ilani ya UKAWA?

Lowassa Leo Kasema anajua tu ataibiwa kura zake .Sasa Kama unajua utabiwa kura zako kwanini unaendelea kushiriki Katika uchaguzi Mkuu?Maana hadi umediriki Kusema utaibiwa kura Ina maana utashinda.Kwanza Hao watakaokuibia ni wakinanani na kwasababu gani?Kama unajua utaibiwa kura zako kwanini unaamasisha wananchi wakupige kura?.

UKAWA simnajitapa Kuwa mmejipanga kisawasawa na kwa upande wa wanausalama mmpo vizuri.Sasa Kama mmejipanga vizuri na wanausalama wa UKAWA wapo imara kwanini uibiwe kura?Basi hamna wanausalama UKAWA?

Hivi Lowassa kwa usanii huu unaoufanya kabisa unaamini utakuwa rais wa Tanzania baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Mwaka huu? Pole sana Lowassa kwasababu huwezi kushinda urais kwa Sababu haupo Siriazi na urais ,unafanya mzaa na usanii wa wazi kabisa.

Lowassa jiulize kwanini Hilo limetokea uliopoanza kuongea wananchi walianza kuondoka Hawakutaka kuusikiliza .Jibu ni Jepesi walilokuwa wanalitajarajia kutoka kwako hawajalipata maana umewaambia wakasome Kwenye Mtandao.

Kumekuwa na Madai Kuwa Afya ya Lowassa sio nzuri ,licha yeye Mara kwa Mara amekuwa akikanusha taarifa hizo. Sasa kwa kitendo hicho cha Leo cha kushindwa kusoma hotuba kwa kisingizio cha muda kumalizika.

Je hatuoni hii ni mbinu iliyotumiwa na viongozi wa UKAWA ya kumuepusha Lowassa asisome hotuba hiyo kwasababu hawezi kusimama jukwaani muda mrefu ? Lowassa unatatizo.

Mungu ibariki Tanzania


0716 774494
Facebook: Happy Katabazi
Blogg: .
29/8/2015
 
Very good job lowassa.. umepiga ihena jangwani... Watu wakavuta viti usiku... Full surprise.

Usiache kuwakimbiza
 
Umeongea maneno meengi hayana point Sumaye hajawahi kugombea urais ila alikuwa anaomba ridhaa ya chama chake kimchague aweze kugombea urais kuhusu Lowassa umeongea meengi ila mi napenda kukwambia hanaga maneno mengi yule Mzee subirin vitendo after October 25
 
Mipasho hii
Magufuli tutapatia wapi hotuba yake ya kusalimia kwa lugha zote na pia ilani ya ccm sisi malofa tutaipata wapi?

MAANA NAYE MAGUFULI ZAIDI YA KUIMARISHA MUUNGANO KANIACHA GIZANI.
 
Aisee!!! Ccm wamepita mara ngapi wakabwabwaja na hotuba gazeti hadi leo nchi haijielewi.

Kwanza katika maisha yako ogopa sana mtu anaeongea sana, maana anakua hana muda wa kufikiri kwa kina.

Tunataka vitendo tu maneno awaachie wapaka carolight na wasutanaji mabalazani a.k.a CCM
 
Kichwa chako kinahitaji kupepewa. Umezoea kutongozwa kwa masaa Kama ulivyosema. Tunakusamehe. Nitashangaa Kama umeolewa, sio rahisi kwa mtindo huo.
 
Lowassa kanyaga twende baba, wauwe hao ccm kwa hoja, kufikia october ccm watakua wamekufa wote kwa presha.
 
Wanafikiri dola ni kitu kidogo sana kiasi kwamba kinaweza hata kufanyiwa masihara na sinema...
 
Poleni sana wanabadiliko wakweli na wanamapinduzi ya kweli,,, maana ndio watu pekee wenye akili na uwezo wa kufikiri,, taasisi ya urais haihitaji hizi sinema hata kidogo,, hili lilitarajiwa kutokea kabla..
 
Tumechoka na maneno mengi jamani, mok wakenya wanasemaga watz maneno mengi, na hiyo ujue ni dalili ya utapeli, mtu anayeongea sana si mtendaji, mara nyingi anaficha udhaifu wake kwenye kubwabwaja........UKAWA ina timu bora kabisa ya Kampeni,Mbatia, Lissu,Duni,Mbowe,Sumaye.........lowasa hata akiongea dakika tano zinatosha kabisa sisi kuelewa,mnaojilazimisha kutoelewa nendeni mkasikilize maneno mengi huko kwa Magufuli na kina Nchemba.
 
#hapa pont tu kazi hata punda anafanya.

Linganisha vipaumbele vya hawa Wagombea wetu,

LOWASSA,
1.Elimu
2.Kilimo
3.Afya
4.Mawasiliano
5.Nidhamu pamoja na Utawala bora.

Kwenye kona ya kitalaaam Lowassa yuko vizuri sana amegusa mahitaji ya jamii kwa kutumia lugha ambayo inaeleweka kwa kila mtu, intellectual pamoja na layman

VS
Ahadi za JP Magufuli;
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za wana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo
32. Reli ya Dar itajengwa

Hakuna Tafiti yoyote duniani ambayo unaweza kutekeleza kwa kuwa na Malengo (objectives 32)kwa Kipindi Cha miaka mitano utaalamu hapo umewekwa pembeni ila utamu wa lugha ndo umewekwa mbele Hakuna uhalisia (insight and realistic)
 
Happiness huna HAJA NA Lowasa.We Endelea kuchangia unayemshobokea.Ukawa hatuna haja ya Sera kwa sasa.CCM Sera zipi Miaka 53 ya Uhuru anabwabwaja ila ndo Tunazidi kudidimia.Tunasema hv na mtuelewe CCM bench kwanza.Sera tunazijua na ut azifurahia baada ya kuwekwa huru.KATABAZI habari ndo hiyo.
 
Back
Top Bottom