Lowassa: Tuzo ya amani imewaumbua CCM

Lowassa: Tuzo ya amani imewaumbua CCM

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa amesema anashangaa kuona anaambiwa mleta vurugu wakati dunia inamkubali kuwa ni mlinzi wa amani.

Kauli ya Lowassa imekuja ikiwa ni siku moja baada ya taasisi za kidini 1,200 duniani kupitisha jina lake kwa ajili ya kumpatia Tuzo ya Amani.

"Nimepokea kwa unyenyekevu na furaha tuzo ya amani duniani ninayotarajiwa kupewa na taasisi za kidini 1200 duniani," alisema Lowassa akinukuliwa na msemaji wake, Aboubakar Liongo.

Lowassa alisema tuzo hiyo ni kithibitisho cha uongo wa CCM na Serikali yake kuwa wapinzani ni watu wa vurugu.

Taasisi hizo katika kikao chake huko Bukavu DR Congo, zilitangaza kumpa tuzo hiyo Edward Lowassa kutokana na utulivu aliyouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu Kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga ilisema kiasi wajumbe 1,400 wa mkutano huo kutoka kote duniani walikubaliana kumpa tuzo hiyo Lowassa kati ya wanasiasa 1,000 waliyoshindanishwa ili kumpata kiongozi bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.

Alisema yeye ni muungwana na ana hofu ya Mungu na hata siku moja hatoweka mbele maslahi binafsi, na ndiyo maana aliwatuliza wananchi waliyokuwa wakimtaka kutoa tamko baada ya matokeo kutangazwa.

"Siko tayari kuingia Ikulu huku mikono yangu ikibubujika damu. Nashukuru taasisi hizo za kidini duniani, zimeliona hilo," alisisitiza Lowassa.

Chanzo:
Mwananchi
 
1. TUNAOMBA SANA UTUWEKEE ORODHA YA HIZO TAASISI ZA DINI ZILIZOTOA HIYO TUZO. BILA ORODHA YAKE INAONEKANA ULE USANII UNAENDELEA.

2. VIPI WALE WALIOKUFA NA MKASEMA WANAKUFA KWA SABABU WALIMTUKANA MHE.LOWASA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NDIO MAANA MUNGU KAWAUA. JE HIYO DAMU HAIHESABIKI????

3. WATUMISHI WA MUNGU WENGI WAMEPOTEZA MVUTO KWA WAUMINI KUTOKANA NA MATAMKO YENYE KUPINDUKAPINDUKA. HEBU SOMENI NENO LA MUNGU TENA MTUAMBIE NI WAPI MANABII WA KWELI WA MUNGU ALIYEHAI WALIKUWA NA KAULI ZENYE MAGUMASHI?? Nabii Eliya alisema mvua hainyeshe ila kwa neno langu na haikunyesha nk

4. HAWA WATUMISHI WALISEMA LOWASA ATAKUWA RAIS MAAANA WANA HAKIKA NA MUNGU ALICHOSEMA NAO. TENA KUNA MMOJA ALISEMA LOWASA ASIPOKUWA RAIS WAMUUE???? Hivi wameshamuongoza sala ya toba????

5. HEBU HUBIRINI INJILI JAMANI YESU KARIBU ANARUDI. DUNIA IMEJAA DHAMBI NA MAOVU. HEBU TAFAKARINI TENA UPOSO WENU???

6. HALAFU HAWA NDIO WALE WANAOTOA PHD FEKI. NATAMANI SERIKALI ITOE TAMKO LA KUFUTA HIZI PHD ZA TAASISI ZA DINI. ZINAONDOA KABISA MAANA. YAANI WACHUNGAJI MITUME NA MANABII WANAKIMBIZANA NA HIZI PHD. SASA HIVI HUO UGONJWA UMEKUJA MPAKA KWA WAUMINI.

7. HEBU ACHENI KUIRAHISISHA IMANI NA NENO LA MUNGU KWA MATUMBO YENU. Shame on you.

Queen Esther

Lowassa ametupa kijembe cha kufungia mwaka pale aliposema Ccm wanaeneza uvumi na propaganda kwamba wapinzani wana vurugu baada ya yeye kutambuliwa na taasisi za kimataifa kama mtu wa amani.

Amesema yeye asingeenda Ikulu na mikono iliyojaa damu.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa kuwa alikubali binafisi nampongeza sana lowassa ila vijembe havisaidii tena kumfanya aingie ikulu leo, tuombeana uzima 2020 sio mbali nafasi anayo ya kuingia ulingoni, kwa sasa nimtakie tu mapumziko mema!
 
Lowassa ametupa kijembe cha kufungia mwaka pale aliposema Ccm wanaeneza uvumi na propaganda kwamba wapinzani wana vurugu baada ya yeye kutambuliwa na taasisi za kimataifa kama mtu wa amani.

Amesema yeye asingeenda Ikulu na mikono iliyojaa damu.

Chanzo: Mwananchi
Lowasa tapeli kwahiyo kapewa tuzo na matapeli wenzake wanajuana wenyewe.
 
Ata ingekuwa tuzo za kili Lowassa asingepata?!! Hivi ao wanamjua huyu kiumbe au wanamsikia??? Tuzo aandae RA alafu mujifanye taasisi za kidini
 
Ninayo Hofu Kuu, Kua Ccm Wanaweza Kua Na Mkono Wao Katika Hizi Tuzo Za Amani This Time. Isije Ikawa Ccm Wanawaandaa Ukawa Kisaikolojia Ili Wakubali Yaishe Na Kuwaachia Ccm Waichukue Zanzibar Kwenye Nafasi Ya Urais Kiulaini Bila Kuwepo Kwa Vurugu Yoyote. Is Like Tuzo Za Nobel Walizopewa Wakina Yesser Arafat, Dhidi Ya Akina Shimon Perez Na Yirzak Rabin Pale Mido Isti. Hii Dunia Hua Inaendeshwa Kwa Master Plan. Kuondoa Presha Ya Cdm Kule Visiwani Na Kuiachia Cuf Alone. Itaisaidia Ccm Ku-push Interests Zake Vizuri .Kama Tuzo Hizi Zingekua After Uchaguzi Zenji Umekwisha Ningeziamini, Lets Pray N See..
 
Lowasa tapeli kwahiyo kapewa tuzo na matapeli wenzake wanajuana wenyewe.

Tatizo unaangaika na aekuzidi:-
1. Hekima
2.Busara
3.Elimu
4.Cheo na nyadhifa mbalimbali
5.Upendo na kupendwa
6.maisha mazuri
7.pesa
kwa maana hiyo ungeweza hata kumshauri Jecha kule Zanzibar kua nduguyo wa Zanzibar wanakosa haki zao kwa sababu yake.
 
Kuna watu mna wivu mpaka mnachekesha, sasa watu wameamua kumpa tuzo nyie mnabeza watu gani nyinyi! Ni kweli ukiangalia jicho la tatu utaona Lowassa kajariwa sana tena sana licha ya madhaifu yake kama yangu na wewe. Punguzeni wivu jamani siyo vizuri kumuonea mwenzio donge tumieni akili badala ya hisia na chuki zenu. TUZO yake na ataichukua kufeni au hamiani Kenya.
 
Lowassa amekosa mvuto,hiyo tuzo ni magumashi na usanii mtupu,ili impandishe chati.asubiri tu 2020

asubiri nini tena 2020? hatutaki tena kiongozi mkuu wa nchi atokane generation ya akina lowassa, kikwete, chenge, mwakyembe n.k. jpm anatosha 2020.
 
Kuna watu mna wivu mpaka mnachekesha, sasa watu wameamua kumpa tuzo nyie mnabeza watu gani nyinyi! Ni kweli ukiangalia jicho la tatu utaona Lowassa kajariwa sana tena sana licha ya madhaifu yake kama yangu na wewe. Punguzeni wivu jamani siyo vizuri kumuonea mwenzio donge tumieni akili badala ya hisia na chuki zenu. TUZO yake na ataichukua kufeni au hamiani Kenya.

Wenye nchi hii unawajua?
 
Ni CCM wanaoandaa TAMKO la Babu Duni la January????? Stay tuned.

Back
Top Bottom