Duuuhhh,kuwa mwanasiasa unahitaji kuwa na roho ngumu,labda na yeye alete tume mpya ya uchaguzi kutoka nje,kama Simba Sc inavyosisitiza mechi yake na Yanga ichezeshwe na marefa kutoka nje ya nchi.Kama tutaendelea na tume hizi ambazo zinavuruga uchaguzi makusudi ili zipewe tuzo(rejea kauli ya Rais John Pombe Magufuli akimtaka Rais wa Zanzibar ampe tuzo Jecha kwa kazi nzuri aliyoifanya "ya kuvuruga uchaguzi'),sioni ni kwa namna gani anavyoweza kushinda uchaguzi wa 2020.
Kwa tume hii tuliyonayo ambayo wakurugenzi wa halmashauri,majiji na miji ambao huteuliwa na Rais ndiyo wadimamizi wakuu wa uchaguzi katika maeneo yao,tutarajie goli jingine la mkono zaidi ya hili tuliloliona uchaguzi uliopita.
Kutegemea msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mteule wa Rais akutendee haki,huku akijuwa kuwa kitendo cha kukutangaza mshindi kinaweza kumpelekea akapoteza nafasi yake kama ilivyotokea kwa yule mama wa Morogoro,ni sawa na kudubiri embe dodo chini ya mnazi.