babu M
JF-Expert Member
- Mar 4, 2010
- 5,222
- 3,176
Inashangaza! Kama alivyokuwa anadai alishinda 2015 ni kipi kilichobadilika kinaweza kumafanya atangazwe raisi 2020!Kwahiyo uchaguzi wa 2015 Lowassa hakushinda?
Inashangaza! Kama alivyokuwa anadai alishinda 2015 ni kipi kilichobadilika kinaweza kumafanya atangazwe raisi 2020!Kwahiyo uchaguzi wa 2015 Lowassa hakushinda?
Alieshinda yuko jumba jeupe.Kwahiyo uchaguzi wa 2015 Lowassa hakushinda?
New version ya Safari ya matumaini lazima itafeli tena.JPM 2015-2025.![]()
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amesema kwa hali ilivyo na inavyoendelea nchini kuna kila dalili za chama hicho kushinda uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Lowassa alisema hayo Dar es Salaam, wakati kuna kilio kikubwa cha wananchi wanaolia kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi, huku wengi wakidhani imesababishwa na kubana matumizi kunakofanywa na Serikali.![]()
Alisema hayo wakati akifungua semina kwa wabunge, mameya na madiwani wa chama hicho wa Jiji la Dar es Salaam ikilenga kujadili kazi waliyofanya ya kutumikia wananchi kwa mwaka mmoja na namna ya kupiga hatua miaka minne ijayo.
Alifafanua: ”Nimepita maeneo mengi kufanya mikutano ya ndani, kwa hali ilivyo tunakubalika mno, tuna dalili zote za kushinda uchaguzi mkuu wa 2020, tujitahidi kuwa na umoja, bila umoja hatuwezi kushinda ni muhimu sana, CCM wanajua maana ya umoja na wanaung’ang’ania, tuangalie sana maneno ya kutugawa tusiyakubali.’’
Alisema Chadema itapita maeneo ambayo watu wako nyuma kielimu ambayo kwa kiasi kikubwa wameipigia kura CCM, ili kuwaelewesha nia njema ya kuwaletea maendeleo na kuwapa elimu.
‘’Muda uliobaki ni mchache, tunatakiwa kuamka ili chama chetu kishinde kwa kuwa tumeshakifikisha sehemu nzuri, hatuna muda tuchangamke kila mmoja aone kwamba anapaswa kueleza namna ya kukisaidia chama kivuke,’’ alisema Lowassa.
Kuhusu mikutano ya ndani ambayo aliita ‘mitamu’ zaidi, alisema vimefanya wamekuwa imara zaidi, kwani wamezungumza na wanachama wao maeneo mengi wakiwa wanaonana kwa karibu.
‘’Tumekuwa mikoani na viongozi wenzangu, tumezunguka mikoani hali ni nzuri kwa mazungumzo tuliyofanya na wanachama wetu, vikao ni vitamu zaidi kuliko vya nje, unapata nafasi ya kuongea na wananchi ana kwa ana kwa muda mrefu, kwa mapenzi na mahaba yote,’’ alisema Lowassa.
Lowassa aliwataka mameya na viongozi wengine wa Chadema jijini humo kukataa kutoa mikataba ya aina yoyote kienyeji na kushughulikia suala la maegesho, ili isifike mahali wananchi wakajuta kuichagua Chadema na kusema afadhali CCM.
Zabuni ya maegesho jijini Dar es Salaam imetolewa kwa kampuni ya Kenya ambayo imeongeza tozo ya kuegesha gari kutoka Sh 300 hadi Sh 500 kwa saa.
Alisema kero ambayo wamekuwa wakikutana nayo katika mikutano yao ni wananchi kutaka uongozi, jambo ambalo alisema kama ingepatikana Katiba mpya zingeongezwa nafasi zaidi za kuteuliwa.
New version ya Safari ya matumaini lazima itafeli tena.JPM 2015-2025.
Yeye nani aweze kukusababisha wafuasi wake walete vulugu wakati Nchi ina mifumo yake ya kuzuia vulugu na uvunjaji wa amani.Ushaona kiongozi gani wa Tanzania alisha imiza wafuasi walete fujo na yeye akafanikiwa na dhamiara yake hiyo...ebu nitajie...uenda mnajiaminisha kuwa USALAMA wa TAIFA hili uko mikononi mwa baadhi ya watu fulanifulani viongozi...thubutu yake....Wanasiasa kama Lowasa ni watu muhimu sana kwenye mataifa haya ya Afrika kwa sababu wanaepusha vurugu zinazoweza kusababishwa na wafuasi wao wenye uchu wa kushinda uchaguzi ikifika 2020 atasema tutashinda 2025 ikifika 2025 atasema tutashinda 2030 miaka inasogea na maisha yanaenda wafuasi wake wanakuwa na imani tu ya kushinda uchaguzi unaofuata kwahiyo hakuna vurugu wala matatizo yatakayotokea Mungu akubariki Edo Lowasa uishi maisha marefu ukiendelea kuwa mgombea wa kudumu wa urais wa chadema hadi 2040.
Bila Tume huru,katiba huru asahau,hakumbuki kuwa ma Rc,Ma DC,ma DEd wote makada wa ccmHapo ni lazima ssa viongozi wetu wadai katiba mpya na tume huru otherwise tutaishia kulalamika kuibiwa tena 2020.
Atakuwa amepona kale kaugonjwa unaomlazimu kujichoma sindano za miguuni?
TrueMZEE LOWASA PUMZIKA BABA UMECHOKAAA. URAIS UTAUSIKIA TU REDIONI NA KUUONA KWENYE TV.