Mimi nashangaa chain of command yetu iko wapi. Lowassa yeye ni nani kuzungumza kwa niaba ya JWTZ? Kamanda in Chief yuko wapi? Yaani Tanzania yetu imeshaparaganyika kiasi kwamba yeyote tu anaweza kuzungumza kwa niaba yake? Suala la vita au kuwa tayari kwa jeshi letu ni kamanda in chief peke yake anayeweza kulizungumzia. When was the last time you saw Lowassa inspecting a guard of honour?
Mkuu Jasusi, Lowassa ndiye M/Kiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hivyo anazo nguvu na mamlaka yote kuzungumzia hili!.
Kwa powers alizo nazo, anaweza kumsummon MFI (Membe), CDF (Mwamunyange), CIS (R.O) na IGP (Mwema).
Utakuwa umechanganya kati ya kuzungumzia uwezekano wa Tanzania kuingia vitani na powers za kutangaza vita!.
Mwenye mamlaka ya kutangaza vita ni Amiri Jeshi Mkuu pekee na hakuna ku delegate jukumu hili!, lakini kuzungumzia nia ya kuilinda mipaka yetu, any leader anaruhusiwa kusema!.
Naendelea kukumbushia posibility ya
"Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!".
Pasco.
Jamani mimi naomba kuuliza tu, hii ni kauli ya Lowasa au ni kauli ya Kamati ambayo yeye ndio Mwenyekiti na ameongea kwa niaba ya kamati nzima? i mis some point here!
mzee mwanakijiji, you might be growing too old!. Kwa kawaida as one grows older is also expected to be wiser, nikukosoma siku hizi nakuona you are either becoming less wiser au inawezekana mimi ndio nashindwa to make sense hivyo uwezo wa uelewa wangu ndio unapungua kuweza kukuelewa!.
Hivi kuna sababu nyingine yoyote ya nchi kuingia vitani ambayo ni kubwa zaidi ya nchi kutishiwa mipaka yake?.
Kuna justfied wars na unjustified wars!. Kwangu mimi kitisho cha malawi ni justified war!. El is right and he is the not only the one who can make the best president of this country but he is "the one and only best" ccm has!.
Kwa kauli kama hii, ni uthibitisho kuwa yeye tayari ndiye amiri jeshi wetu!. Who else?. Nani mwingine yoyote ameweza kujitokeza to stand firm on this national security threat?!.
Naendelea kusisitiza tuendelee kukosoa madhaifu na madudu ya serikali iliyopo kwa nguvu zetu zote, ila pia kama kuna mabaya 99 na zuri moja, hilo moja litajwe!.
Hii kauli ya el imekuja mahali pake at the right place at the right time!.
Pasco.
Vita vya kupambana na ufisadi ambao umepoteza maisha ya Watanzania wengi kuliko vita ya Kagera vimetushinda.Huhitaji mizinga wala ndege za kivita kupambana na adui huyu ufisadi kwa nini vimetushinda?Ikibidi kuwachapa hao wapori pori inabidi wachapwe. Vita si ya kufurahia ila kama haki ni yetu lazima tuipiganie.
Very good mzee, watu wanashindwa kuelewa kuwa we are building up pressure on the other side, forcing them to see our point of view.Kuwen na uelewa, lowasa ni m/kiti wa kamati ya ulinzi na mambo ya nje, in case of anything beyond agreement diplomatically, rais atatangaza vita na siyo lowasa. Hata mvua inaanza kwa rasharasha. Akina lowasa ni rasharasha kabla ya mvua kutua. Pia tambueni kuwa vijana wanavaa kombati bila nishan, acheni wakazipate hizo za malawi jamani.
Naungana mkono na wewe.Kwanza uzalendo huu wa Lowasa unatoka wapi wakati ni yeye na wenzake tayari walishaisaliti nchi hii kwa njia za kifisadi lakini mbaya zaidi ni kwamba kama vita hii itapiganwa Watanzania tutambue kwamba tunaenda vitani tukiwa tumegawanywa na hawahawa akina Lowasa na Mimi nina wasiwasi vita hii kama itatokea itajenga mianya mingine ya kufisadi raslimali za Taifa hili.Maneno ya kujifurahusha hayo! Vijana wa JWTZ hawana morali hata kidogo ! Nani anaenda kupigana vita wakati dhuluma imetapakaa kila sehemu? Hata JWTZ kwenyewe kunafukuta moshi ndani kwa ndani kwa muda mrefu sasa.. Vijana wanaonewa , wanahujumiwa nafasi za masomo, posho halali Na mengine mengi.. Kwa maoni yangu kuingia vitani kipindi hiki imekula kwetu..
Maneno ya kujifurahusha hayo! Vijana wa JWTZ hawana morali hata kidogo ! Nani anaenda kupigana vita wakati dhuluma imetapakaa kila sehemu? Hata JWTZ kwenyewe kunafukuta moshi ndani kwa ndani kwa muda mrefu sasa.. Vijana wanaonewa , wanahujumiwa nafasi za masomo, posho halali Na mengine mengi.. Kwa maoni yangu kuingia vitani kipindi hiki imekula kwetu..