Mara nyingi katika mabunge viongozi wastaafu au viongozi wa vyama vya siasa huudhuria bungeni kwa ajili ya mambo maalum,..Hotuba ya Raisi,Hotuba ya Bajeti, Hotuba ya hali ya Taifa (PM), Hotuba ya hali ya Taifa (KUB). Ukiona viongozi wa vyama vya siasa wanahudhuria kipindi cha maswali na majibu huku wakitumia fursa ya kutambulishwa kama propaganda ujue wamefika mwisho.
mara nyingi kipindi cha maswali na majibu kule kwenye sehemu ya wageni (gallery) hukaa wasaidizi wa mawaziri na wanafunzi wanaojifunza shughuli za bunge. Ninawaeleza washauri wa Lowassa na Sumaye kuwa mmechemka na mmewafanya 'maveterani' wenu kuwa wanasiasa wa rejareja.
Kama leo Lowassa,Sumaye na Ntagazwa (aliwahi kuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais) wanajifunza tena jinsi bunge linavyoendeshwa ni dhahiri wamekwisha. Cha kushangaza hadi wasomi Prof.Safari na Prof.Baregu nao wamefanya makosa makubwa ya kiufundi,tatizo ni picha? au kutokuelewa? au kupotoshwa?
Picha hii hapa chini ni dhahiri itakuonyesha kuwa wamejishusha kiwango,nini wanachojifunza ikiwa wamekaa bungeni miaka takribani 25? . Siku nyingine hudhurieni bungeni mambo makuu ya kimkakati kwa taifa kama Hotuba ya raisi,Bajeti,hotuba ya PM na hotuba ya KUB. Hili lisiachwe lipite ni lazima Mkuu wa Protokali na mambo ya Bunge Chadema, John Mrema awajibishwe...kawafanyia hujuma hawa maveterani,kawashusha,kawapa aibu, kawalinganisha na wanafunzi wa shule ya msingi wanaojifunza bunge.