Lowassa, Sumaye na Kingunge kuisuka upya CHADEMA!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Magazeti leo yanaripoti, Viongozi Wakuu wa CHADEMA wakisaidiwa na Lowassa, Sumaye na Kingunge wako kwenye mkakati wa kuisuka upya CHADEMA. Wameendelea kufanya vikao vya siri Mjini Moshi katika lengo la kuifanyia ukarabati CHADEMA.

Ikumbukwe wakati Lowassa na genge lake wanaingia CHADEMA, tuliambiwa CHADEMA itambadilisha Lowassa lakini kinachoelekea kutokea kwa sasa ni Lowassa kuibadilisha CHADEMA.
Moja ya ajenda ni kuwaondoa viongozi zaidi ya 16 ambao walikuwa karibu na Dk. Slaa kwa njia moja au nyingine na pia wamekwamisha safari ya matumaini/uhakika ya Lowassa kwenda Ikulu ya Rais wa Tanzania.

Inasemekana Lowassa na genge lake kwa sasa watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

CHADEMA inaelekea kuzaliwa upya chini ya Lowassa na genge lake!

12498584_1019627164768408_331476876_n.jpg
 
Last edited:
Hili genge ni zaid ya MAFIA....nawashangaa sana watu wanaokiamini hiki chama pasipo kuona usanii wake uliokithiri....

Bado tuna safari ndefu sana ya kujenga demokrasia ya kweli ya mfumo wa vyama vingi...
 
3.jpg


Kikao kilichojadili hatma ya wafanyakazi hao kilifanyika Moshi wikiendi iliyopita. Hawa watu 16 lazima wataondoka CHADEMA. Wakubwa(waliokutana moshi) wanasema ni katika harakati za kubana matumizi.
source: Raia Tanzania
 
Acha uzushi habari za vijiweni zinawekwa kwenye magazet ya lumumba
 
Vijana wa M4C wanahaha baada ya kuambiwa hawajui siasa na kushauriwa waongeze nguvu kwenye ulinzi wa red brigedi...hii imewakera sana Chadema-halisi Cc Mmawia et al
Kwa sasa vijana wa 4 U Movement wametawala anga la Ufipa! Naambiwa kuna tetesi ya ofisi za makao makuu kutoka Ufipa kuhamishiwa Mikocheni..Ufipa itabaki kama tawi la vijana, wanawake na usalama (red brigade)....hii itakuwa ni "final blow" kwa chadema-halisi
 
3.jpg


Kikao kilichojadili hatma ya wafanyakazi hao kilifanyika Moshi wikiendi iliyopita. Hawa watu 16 lazima wataondoka CHADEMA. Wakubwa(waliokutana moshi) wanasema ni katika harakati za kubana matumizi.
source: Raia Tanzania


Kumbe ni wafanyakazi hata magufuli ameondoa wafanyakazi wengi wa kikwete northing is wrong
 
Back
Top Bottom