Lowassa, Sumaye, Kingunge, Mbowe na Lissu wapuuzwe

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Walipanda kwenye majukwaa kutuambia Rais Magufuli hafai, leo tunashuhudia tofauti.

Walipiga kelele wakitueleza hawezi kulisukuma gari lililokwama kwenye matope wakati yuko ndani yake, anatakiwa ashuke, kama alivyofanya Lowassa, Sumaye na Kingunge. Rais Magufuli ameonyesha kwa vitendo unaweza kulisukuma gari lililokwama kwenye matope hata kama uko ndani yake iwapo utatumia akili vizuri.

Walituambia hatuwezi kumtofautisha Dk. Magufuli na CCM. Leo hata vijana wao wa ULIPO TUPO na TimuLowassa wanatuambia Rais Magufuli ni tofauti na CCM kwa sababu anatekeleza ?sera za UKAWA?.

Walituambia hawamtambui Rais Magufuli lakini cha ajabu wakaingia bungeni kumuidhinisha kwa kumpigia kura Waziri Mkuu, Majaliwa ambaye ameteuliwa na Rais wasiyemtambua.

Kwa sasa wanataka tusiitambue serikali ya Rais Magufuli.

Kwa haya machache, kwanini tusiwapuuze kisiasa kutokana na ulaghai waliotuambia na wanaendelea kutuambia?
 
Walipanda kwenye majukwaa kutuambia Rais Magufuli hafai, leo tunashuhudia tofauti.

Walipiga kelele wakitueleza hawezi kulisukuma gari lililokwama kwenye matope wakati yuko ndani yake, anatakiwa ashuke, kama alivyofanya Lowassa, Sumaye na Kingunge. Rais Magufuli ameonyesha kwa vitendo unaweza kulisukuma gari lililokwama kwenye matope hata kama uko ndani yake iwapo utatumia akili vizuri.

Walituambia hatuwezi kumtofautisha Dk. Magufuli na CCM. Leo hata vijana wao wa ULIPO TUPO na TimuLowassa wanatuambia Rais Magufuli ni tofauti na CCM kwa sababu anatekeleza ?sera za UKAWA?.

Walituambia hawamtambui Rais Magufuli lakini cha ajabu wakaingia bungeni kumuidhinisha kwa kumpigia kura Waziri Mkuu, Majaliwa ambaye ameteuliwa na Rais wasiyemtambua.

Kwa haya machache, kwanini tusiwapuuze kisiasa kutokana na ulaghai waliotuambia?

Hao ni wawakilishi wa Shetani, wanapaswa kulaaniwa.
 
Uchizi uchizi tu...hata chizi anaanzisha mada?
 
Upuuzwe wewe usiye jua mambo, tulia Magufuli atumbue majipu na bado hajayatumbua ndo kwanza anakamua usaa subiri damu itoke ndo utajua umihimu wa Lissu na Lowassa, go go go Dr .Magufuli.
 
Uchizi uchizi tu...hata chizi anaanzisha mada?
Unatoa comment kwenye mada ya chizi huoni kuwa wewe ndiyo unaonekana chizi zaidi!

Ni sawa na chizi anachukua nguo zako wakati unaoga bafuni halafu ukatoka uchi na kuanza kumkimbiza! Unadhani wananchi wenye akili timamu wakikuona watafikiria wewe una akili timamu? Ndicho ulichokifanya hapa katika mantiki yako unaposema mimi ni chizi.
 
Walipanda kwenye majukwaa kutuambia Rais Magufuli hafai, leo tunashuhudia tofauti.

Walipiga kelele wakitueleza hawezi kulisukuma gari lililokwama kwenye matope wakati yuko ndani yake, anatakiwa ashuke, kama alivyofanya Lowassa, Sumaye na Kingunge. Rais Magufuli ameonyesha kwa vitendo unaweza kulisukuma gari lililokwama kwenye matope hata kama uko ndani yake iwapo utatumia akili vizuri.

Walituambia hatuwezi kumtofautisha Dk. Magufuli na CCM. Leo hata vijana wao wa ULIPO TUPO na TimuLowassa wanatuambia Rais Magufuli ni tofauti na CCM kwa sababu anatekeleza ?sera za UKAWA?.

Walituambia hawamtambui Rais Magufuli lakini cha ajabu wakaingia bungeni kumuidhinisha kwa kumpigia kura Waziri Mkuu, Majaliwa ambaye ameteuliwa na Rais wasiyemtambua.

Kwa haya machache, kwanini tusiwapuuze kisiasa kutokana na ulaghai waliotuambia?

Kwa taarifa yako kama sio nguvu ya Lowassa kuvuruga mchakato wa kura za maoni ndani ya ccm leo hii Bernard Membe ndio angekuwa rais wa Tanzania na sio Magufuli
 
Hii ndio IQ ya mtanzania tena mtanzania typical ambae miaka 10 iliyopita aliahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania na leo keshasahau kabisa nini kimetokea katika kipindi hicho kiasi cha hata kushindwa kabisa kuweka akiba ya maneno kwa ahadi anazotoa Raisi wa sasa.

Duniani hakuna mtu rahisi kummtawala kama mtanzania.
 
Kwa taarifa yako kama sio nguvu ya Lowassa kuvuruga mchakato wa kura za maoni ndani ya ccm leo hii Bernard Membe ndio angekuwa rais wa Tanzania na sio Magufuli
Kwani huyu Benard Membe kama angepitishwa angepambana na nani kwenye kambi ya upinzani?

By the way, Nguvu ya Lowassa ilivuruga vipi mchakato wa uteuzi ndani ya vikao?
 
Mnashindwa kuwapuuza walioifilisi hii nchi mnahangaika na watu makini.
 
Nionavyo mimi.....Mh Rais anahitaji saana ushirikiano wetu uwe wa Ukawa au Ccm uchaguzi umekwisha sasa tufanye maendeleo.Tukianza kupigia vyama vyetu debe hatutatoka hapa tulipo.TUMPE SUPPORT MAGUFULI serikali iliyopita kwa hakika imetuangusha.
 
Kwa taarifa yako kama sio nguvu ya Lowassa kuvuruga mchakato wa kura za maoni ndani ya ccm leo hii Bernard Membe ndio angekuwa rais wa Tanzania na sio Magufuli

Bora hata nyumbu wa serengeti kuliko hawa binadamu wenzetu.Yaani ni kama roboti.
 
Wewe mleta mada unaonekana ni mtu mzima kabisa huenda na ndevu zipo lakini kichwani mweupeeee.Wewe unajua maana ya kampeni,ulitaka waseme Magufuli ndo anafaa wkt wa kampeni alafu wao wangekuwa wanazunguka kufanya nini kama wangekuwa wanatangaza kwamba Magufuli ndo anafaa kuwa Rais?au ulitaka wampigie kampeni?
 
Back
Top Bottom