mwekundu
JF-Expert Member
- Mar 4, 2013
- 22,477
- 21,040
Lowassa: Sina mpango wa kutangaza nia
Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kutangaza nia ya kugombea urais kwa sasa, bali anapenda kushirikiana na waumini na wananchi katika shughuli zao za kimaendeleo.
Hayo aliyasema katika uzinduzi wa helikopta maalumu ya Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dar es Salaam jana.
Lowassa alisema alipopata mwaliko huo alifurahi kwa heshima aliyopewa, lakini alikutana na swali gumu linalohusiana na urais.
"Nilipofika hapa, kuna mmoja wa rafiki zangu akaniuliza, umekuja kutangaza nia? Nikamwambia sikuja kutangaza nia hapa...Sina mpango huo kwa sasa. Nimekuja kusali na kushiriki kanisani kwa ajili ya kuinua jina la Bwana," alisema Lowassa.
Alisema taifa linahitaji viongozi wenye maono ambao ndiyo wanaoweza kulivusha na kulipeleka mbele.
Akihutubia maelfu ya waumini kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, alisema viongozi wenye maono ndiyo mfano unaotakiwa kufuatwa kwa kuwa utaleta mabadiliko chanya.
"Hatuhitaji viongozi wenye kusimamia na kutunza hesabu. Tunahitaji viongozi wenye maono na kuhakikisha maono hayo yanatimia. Kanisa lenu lina bahati kwa kuwa lina kiongozi mwenye maono na anayeweza kuyasimamia," alisema.
Akielezea ununuzi wa helikopta hiyo, alisema amefurahishwa na hatua hiyo ambayo ni ya kihistoria nchini. Awali, Askofu Gwajima alisema anaumizwa na baadhi ya wanasiasa wanaoshindwa kusimamia uamuzi wao, huku akiwaita ‘ndumilakuwili.'
"Nawajua sana wanasiasa, wapo ambao wakikwambia umepata, usipumzike, tafuta zaidi kwa kuwa hawamaanishi hivyo. Lakini Lowassa akimwambia umepata, nenda kampumzike," alisema.
Chanzo: mwananchi.co.tz