Lowassa: Njia ya Ikulu 2020 nyeupe

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amesema njia ni nyeupe kwa CHADEMA kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.

Akizungumza nyumbani kwa kada wa CHADEMA, James Lembeli katika kijiji cha Mseki, Kahama, Lowassa alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.

Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
 
Masikini Sumaye!

Ndoto zake zinaendelea kuzikwa!

Sumaye alidhani mwaka 2020 itakuwa zamu yake!

Kuna hatari ya watu kugawana fito!
2010 mliaminishwa ni mbowe cha kushangaza akletwa dk slaa na kuzoa kura mamilioni..... then
Mlijiaminisha hivi hivi kwa dk slaa kuwa atagombea 2015.....mwisho wa siku mkapewa suprise package mkabaki mnaduwaa na kma sio NEC na polisi yangekuwa mengine kabisa sahivi.
Haya nyie jiandaeni na lowassa 2020 trend ile ile iendelee muhim muweke tume huru coz atakayeletwa lazma awatingishe maana hamjajiandaa naye nyie mnakomaa na lowasa kma mlivyokomaa na slaa 2010-2015
 
8221ceecfbb5d741a65aa9a0b1adf58b.jpg
Ikulu ni yake
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amesema njia ni nyeupe kwa CHADEMA kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.

Akizungumza nyumbani kwa kada wa CHADEMA, James Lembeli katika kijiji cha Mseki, Kahama, Lowassa alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.

Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
Lowasa anaimaliza chadema, anatengeneza mtandao ndani ya chadema kama ule alioutengeneza akiwa ccm na hii ndio staili yake ya siasa. Hajiamini ndio maana anapenda kutengeneza mtandao wa kumbeba. Chama kama wana akili huu ndio wakati wa kumpiga chini lowasa na waanze upya kujenga chama chao kiwe na upinzani wa kweli kuelekea uchaguzi 2020 maana huu wa marudio wameangukia pua vibaya.
 
upinzani wajitahidi 2020 wapate wabunge wengi lakini nchi urais wa nchi
kiukweli bado sana.
 
Lowasa anaimaliza chadema, anatengeneza mtandao ndani ya chadema kama ule alioutengeneza akiwa ccm na hii ndio staili yake ya siasa. Hajiamini ndio maana anapenda kutengeneza mtandao wa kumbeba. Chama kama wana akili huu ndio wakati wa kumpiga chini lowasa na waanze upya kujenga chama chao kiwe na upinzani wa kweli kuelekea uchaguzi 2020 maana huu wa marudio wameangukia pua vibaya.

Hata mwenywe nimeona hivo,atatengeneza mtandao hatarre sana ndan ya Chadema mwisho wa cku itakuwa classes ndan ya chadema,wacha watifuane
 
Ameshajpitisha mwenyewe bila kamat kuu safi sana ichi ndyo chama tulichokuwa tunataka
 
Mhm, siasa bhana kila siku mtu anaota ushindi na ushindi haupatikani kirahisi,hata 2015 alisema atashinda na matokeo yakawa sivyo.
 
Lowassa nampenda sana anaitendea haki kabisa taaluma yake sanaa na mazingaombwe
ila anachoshindwa kuwaeleza wafuasi wake ni kuwa hatakuja kuwa rais wa nchi hii
 
Back
Top Bottom