Lowassa: Njia ya Ikulu 2020 nyeupe

Lowassa: Njia ya Ikulu 2020 nyeupe

2010 mliaminishwa ni mbowe cha kushangaza akletwa dk slaa na kuzoa kura mamilioni..... then
Mlijiaminisha hivi hivi kwa dk slaa kuwa atagombea 2015.....mwisho wa siku mkapewa suprise package mkabaki mnaduwaa na kma sio NEC na polisi yangekuwa mengine kabisa sahivi.
Haya nyie jiandaeni na lowassa 2020 trend ile ile iendelee muhim muweke tume huru coz atakayeletwa lazma awatingishe maana hamjajiandaa naye nyie mnakomaa na lowasa kma mlivyokomaa na slaa 2010-2015
Kumbe kuna "kapi" linatafutwa afu 2020 Lowassa atatoswa kiaina.
Poor Lowassa, ya Dr. Silaa yanakufuata.
 
Bila muundo wa tume ya uchaguzi kufanyiwa marekebisho ukawa msifikirie kushinda uchaguzi mkuu Tz.
 
Njia mbona nyeupe tu watu wanapita kila siku kwenda ferry na kurudi ila mwisho saa 12 jioni.
 
Kumbe kuna "kapi" linatafutwa afu 2020 Lowassa atatoswa kiaina.
Poor Lowassa, ya Dr. Silaa yanakufuata.
Lini chadema wamerudia mgombea?? Wapi chadema wamesema lowasa atagombea 2020?? Mkutano upi umempitisha??
Acheni kuspeculate 2020 analetwa msiyemtegemea na mziki wake utakuwa zaidi ya 2015 muhim tukiweka tume huru inshallah madhara mtayaona

Huyo dr slaa ndie aliemleta lowasa chadema sema kilichotokea ni mke wake alikataa akamuambia achague kati ya lowasa au ndoa.... the rest is history na ndio maana slaa hajawahi kukanusha hizo taarifa mpaka leo ssa nyie endeleeni kujidanganya eti slaa slaa kwani unafkiri hakuwa na wapiga kura million 2?? Sasa ilikuwaje hawakumfuata??? Hujiulizi?? Karatu jimbo lake lote bado likarudi chadema na meya wa pale ni chadema??? Hahaahahahaaha

Namheshim sana slaa mpaka kesho ila mnapomuingiza kwenye mijadala kma hii mnaudhi sana
 
Hizi threads za leo siwaoni BAVICHA na wale ULIPO TUPO wakichangia,wote wamelala mbele,wamemwachia Zitto Junior peke yake,naona anajibu mashambulizi kote kote.. hahaha
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na mkurugenzi wake kitaifa wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM. Kule majimboni Wakurugenzi wa maendeleo ndio mabosi wa tume na wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM. Mzee wangu Lowasa unadhani utaishindaje CCM kwa mtaji wao huo?
 
Lowasa anaimaliza chadema, anatengeneza mtandao ndani ya chadema kama ule alioutengeneza akiwa ccm na hii ndio staili yake ya siasa. Hajiamini ndio maana anapenda kutengeneza mtandao wa kumbeba. Chama kama wana akili huu ndio wakati wa kumpiga chini lowasa na waanze upya kujenga chama chao kiwe na upinzani wa kweli kuelekea uchaguzi 2020 maana huu wa marudio wameangukia pua vibaya.
Hapo Bado hajamseti mwenyekiti wake..ndio chadema II itazaliwa ikiungwa mkono na cuf na kina mtatiro..subiri uone
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amesema njia ni nyeupe kwa CHADEMA kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.

Akizungumza nyumbani kwa kada wa CHADEMA, James Lembeli katika kijiji cha Mseki, Kahama, Lowassa alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.

Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
Katika mfumo huu Lowassa asitudanganye ccm itashinda daima, hata vijana wote wakipigia kura upinzani haitasomeka hivyo. Lakini yeye pia kwa kiasi kikubwa amechangia hali hii kwasababu hakuwa mkweli na mpenda haki alipokuwa kwenye ufalme, iwe funzo kwake na kwa wengine ambao bado wapo katika ufalme kwa kuwa kama sio wao basi vizazi vyao vitakutana na hali anayokutana nayo Lowassa sasa..
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amesema njia ni nyeupe kwa CHADEMA kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.

Akizungumza nyumbani kwa kada wa CHADEMA, James Lembeli katika kijiji cha Mseki, Kahama, Lowassa alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.

Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
Siyo kila mgonjwa hupelekwa Mirembe
 
Nasikitika sana anaposema Lowassa Njia ya Ikulu 2020 Nyeupe. Tuchukue mfano mdogo tu wa huu uchaguzi mdogo uliomalizika juzi.
Wapinzani wameshinda viti vingapi- 1 kati ya 20
CCM wameshinda 19. Mh. Lowassa ametembea karibia vituo vyote vya kura akiwaombea kura wapinzani but impact yake kwa wapiga kura ameambulia kata moja kati ya 20. Bado Chadema wanaamini kuwa Lowassa anapendwa na watanzania laaa ashaa....!!! Ninavyoamini huu uchaguzi ungekuwa ni kipimo tosha kuelekea uchaguzi wa 2020.
So my thinking wapinzani wabadilishe upepo wa siasa waache longolongo na visingizio visivyokuwa vya msingi.
Mwisho Lowassa ndiye anayeua Chadema-UKAWA. Ukiuliza how nitakupa majibu....!!!
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amesema njia ni nyeupe kwa CHADEMA kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.

Akizungumza nyumbani kwa kada wa CHADEMA, James Lembeli katika kijiji cha Mseki, Kahama, Lowassa alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.

Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
Kama Lowassa angejifunza kwa Seif. Mara tano Kapa! Bora afanye biashara. Akitaka Urais akagombee wa TFF
 
Back
Top Bottom