Lowassa: Ninamuunga Mkono Kenyatta na nipo tayari kutoa msaada wakati wowote

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Wageni kutoka Jamhuri ya Kenya wakiongozwa na wabunge 13, Madiwani, Machifu na Maleigwanan kutoka Kenya mchana wa leo wamemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Ngoyai Lowassa nyumbani kwake kijijini Ngarash, jimbo la Monduli wakiongozana na vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali kutoka Wilaya mbalimbali za Mikoa ya Arusha na Manyara.

ad4201fe7625d5d7c37da96b853f43c5.jpg

Aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA na waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Edward Lowassa leo ameuambia ujumbe wa wabunge kutoka Kenya kuwa anamuunga mkono mgombea Urais ambaye pia ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

"Niseme hivi, sisi watu wa Monduli tumeamua kumuunga mkono Rais Kenyatta.

Tuko tayari kumsaidia pale wakati utakapofika, tunafanya hivyo kwa sababu tunampenda na yeye pia anatupenda. Tunaamini yeye pekee ndiye mtu sahihi ambae anaweza kuendeleza mshikamano na umoja uliopo baina ya mataifa yetu haya mawili"

Edward Lowassa
27 April 2017
Monduli, Arusha.
 
Wageni kutoka Jamhuri ya Kenya wakiongozwa na wabunge 13, Madiwani, Machifu na Maleigwanan kutoka Kenya mchana wa leo wamemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Ngoyai Lowassa nyumbani kwake kijijini Ngarash, jimbo la Monduli wakiongozana na vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali kutoka Wilaya mbalimbali za Mikoa ya Arusha na Manyara.

Lowasa aache kutapeli watu, yeye siyo Mmasai wa damu bali ni Mmeru/Machame!
 
Back
Top Bottom