OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,073
- 114,571
Katika mikutano yake mikubwa inayoendelea, aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA Ndg. Edward Lowassa amesema yeye alipigiwa kura na Maskini na Matajiri na watu wa hali zote!! Lowasa alisema watanzania ni wamoja bila kujali hali zao kwani wote wanategemeana katika maendeleo ya Tanzania!
Lowassa amesisitiza kwamba anashangaa kusikia kuna mgombea alipigiwa kura na masikini,Je wasio masikini watajisikiaje! Amenukuliwa akisema kauli hizi ni za kibaguzi na baada ya uchaguzi anayepata nafasi anakuwa kiongozi wa wote!
"Mwingine atakuja kusema, mimi nimepigiwa kura na waislam au wakristu tu, huu ubaguzi haukubaliki" anasema Lowassa.
Lowassa anaendelea na ziara za kuongea na Watanzania akijenga chama chake pamoja na kuinyoosha serikali kwa mambo yanayoenda hovyo hovyo.