Lowassa ni mateso kwa Taifa

Lowassa ni mateso kwa Taifa

Lowasa ameipasua Chadema nusu. Wanachama wengi wako Chadema Asili na waliokubali kubadili gia angani wako Chadema Mbowe na Lowasa wao. Kwa sasa hawana agenda baada ya ile mafisadi kutekwa na rais JPM.
Nyinyi CCM ajenda yenu ni IPI?? Kipaumbele chenu ni kipi ?
 
Napenda sana kiongozi anayesimamia maneno yake. Lowasa alisema atarudi kuchunga ng,ombe na mbuzi huko kwao. leo bado yupo kwenye vitaru vya mihogo Morogoro na juzi alikuwa kituo cha polisi kati. Je ataaminika huyo?

Lowassa ni mwanachama na katiba ya chadema ipo.
a
 
Mkuu, (full disclosure: Mimi ni mpenda mabadiliko na maendeleo). Mtu akilisoma atajua una-agenda ya U-CCM. Ila una hoja. Upinzani wanahitaji kukaa chini na kujitafakari. Walijipambanua kwa agenda ya Ufisadi. Leo wamebadilika. Kitu ambacho hata critics wa Magufuli watakubali (hata kimoyomoyo), Magufuli hana makando kando ya ufisadi. Sasa ukiangalia anadeal na yale yale ambayo upinzani wameyapigia kelele miaka nenda rudi (na wananchi wakawa-support). Leo Magufuli mnamuweka kundi lipi? Do you really think kweli kwa mwananchi masikini asiye na kitu...huu wimbo wa udikteta utamwingia?

Kwangu mimi Tanzania inahitaji Upinzani makini na strong. Lakini nina wasiwasi na upinzani unakoellekea. Ujikite kwenye hoja ambazo zina mashiko. Zinazoleta chakula mezani mwa mlalahoi. Ukiangalia hii kasi ya Magufuli waathirika wakubwa ni wale wale (usual suspects). Waliokuwa nacho. Kiukweli RAIS wanaomsupport wengi ni wale wanaoamini kwamba wizi ulikuwa umetamalaki na wanaolalamika kuhusu utendaaji wake ni wale wale waathirika wa sera za wizi kipindi cha Jakaya.

Nawashauri kaka na dada zangu upinzani. Kaeni chini mjitathimini tena. Mnahitaji kurudisha imani yenu kwa wananchi.
Huwa nawashangaa wanaojisemesha kuwa upinzani wameachana na agenda ya ufisadi. Hiv kama wapinzani wanazibwa midomo watawezaje kuendelea na vita na Ufisadi?

Kama wewe ni mfatiliaji wa matukio ya kisiasa, wapinzani wameanza kuzibwa mdomo pale walipoanza kuleta bungeni sakata la Lugumi na uuzwaji wa nyumba za serkal. Je uo si ufisadi au wewe unaongelea ufisadi gani? Au ufisadi unaomgusa Magu sio ufisadi?

Bila wapinzani kushadadia swala la Lugumi hata kitwanga asinge tengenezewa muvie ya kumtumbua ila kwakuwa watz wasaulfu tiyar wamesha sahau.

Leo tunadanganywa na utumbuaji hewa. Hakuna mpaka sasa hv tunayeskia kafikishwa mahkaman au kafilisiwa baada ya kutumbulia. Ila watz tulio wajing tunashangilia et ni utumbuaji wakati mijamaa bado inapokea mishahra na tunapishana nayo tu njian inaponda starehe. Wewe leo ukiiba hta kuku ni miaka sita jela. Wenzio wanaiba mabilion wanapewa misamaha au kupunguziwa hukumu. Wewe uku unapiga makofi et utumbuaji.

Ulivyo zoba utasema wanasubili mahkama ya Mafisadi.
 
Mtu akiamka tu Lowassa...akinya tu Lowassa..basi ww unayejua ni fisadi mshitaki kama hujatoa mapovu kwa aibu
 
Nitaandika kwa kifupi sana.

Swali ni hili... ajenda kubwa ya upinzani ni ipi?? Jibu ni " kupambana na udikteta chini ya John Magufuli" rais wa tanzania amekuwa dikteta ambaye anaziba watu midomo. Naendelea kujiuliza huyo dikteta ni yupi ambaye anawaacha watu wamuite dikteta... ni dikteta yupi huyo ambae ukivunja sheria anakupeleka mahakaman na bado unashinda,unapewa rufaa..yaan dikteta anakuacha utafute haki Zako katika mahakama (chombo kinachosimamia haki)?? Dikteta anaziba watu midomo au anakuzima hata hiyo sauti hutoi??

Lakini bado najiuliza hivi wananchi issue ya udikteta unaclick kichwani kwa mtu ambaye ameanza kwa kufungua mahakama ya mafisadi? Mtu ambaye anarudisha nidhamu katika offisi za uma? Mtu anaepigania kufanya kazi? Kiongozi ambaye anasafisha mifumo mibovu kama elimu??

Wapinzani chonde chonde yale maisha ya kusubiri udhaifu wa serikali ndiyo mtengeneze ajenda pengine ndiyo wakati sahihi wa kuyaacha.. kila ajenda mnayopigia kelele Magufuli anaifanyia kazi.

Mlikuwa na nguvu kabla LOWASSA hajaja upinzani.. kwa zile kura alizosema mwenyekiti wa chadema mh Mbowe kamati kuuu nanukuu " makamanda kutokana na muda hatutapiga kura za siri.. wanaokubali lowassa simameni mmkunje ngumi hivi"... najiuliza katika mazingira hayo ungeweza kumkataa?? Lakini Lowassa yupo kamati kuu na vikao vyote vya juu anashiriki.. kwa katiba ipi?? Mwenyekiti wa chadema tukisema anatumia mabavu kuongoza chama kama ilivyowahi kulalamikiwa na watu kama Zitto Kabwe nitakosea???

Ukweli ni huu ajenda ya Upinzani ilikuwa ufisadi. Sasa hivi sio ajenda yao tena ndiyo maana ile list of shame wameifuta kwenye website yao ... narudia kumchukua Lowassa was a wrong move . .

Hivi hiyo september 1.. tu assume Magufuli akawaruhusu mufanye mikutano na maandamano ajenda itakuwa ipi??? Udikteta?? Yaani upo kwenye mikutano na unahojiwa kabisa na tv unasema hii nchi rais anaziba watu midomo... nasononeka upinzani unakufa haraka tofauti na nlivyofikiri.
fimbo ya ccm ni lowasa......................
 
Tushawachoka,naombeni chance nipige hela halafu nikishaneemeka na familia yangu nijiuzulu na ninyi mmbaki kwenye mitandao mkiniimba mimi fisadi,tena hata mimi mkitaka nitakuwa najiimba Mimi fisadi!
 
Hujaelewa, Sio dikteta ila dikteta uchwara

Hata mimi nashangaa kwanini imekuwa ngumu kueleweka...Magu sio dikteta, bali ni "dikteta uchwara" kuna tofauti kubwa sana kati ya maneno hayo mawili. Kwa kudhihirisha kwamba yeye ni dikteta uchwara, bado anatawala kimabavu ilhali kuna katiba na sheria za nchi, na kila siku anapozivunja, watu majasiri kama Lissu na wengine hawaogopi kumwambia na hata kumshinda mahakamani. Dikteta halisi (sio uchwara) huwa ana tawala kwa decree (amri na maono binafsi) au kwa "katiba" ambayo haina vipengele vyovyote vya kumzuia kufanya atakayo kufanya. Sasa kama Magu ndio anataka tufike huko, basi aanze tu sasa hivi kubadili katiba na sheria nyengine, na kuwa yeye ndio mkuu wa yote. Vinginevyo, ni kuendelea kuichanganya nchi bila sababu za maana.
 
bureeeeee kabisa mijitu inaimba lowassssaaaaaa mwizi Mara fisadi mbaf* si mpeleke mahakamani? ndo maana upinzani tunamkubali kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.
 
Yan Uyo Lowassa utazan amezaa na wake zenu
 
Habari za Lowasa kwa sasa si ishu.Ishu ni habari za hali ya kiuchumi mitaani.Maisha ya mitaani hayaridhishi yanakatisha tamaa.Dili za hapa na pale zimeadimika.Haijulikani matumaini ya kupata kazi yatarejea lini.
 
Mtoa mada, maumivu ya kichwa, huanza polepoleee.....vivyohivyo Ud.....Uchw....huanza kwa dalili hizo hizo.
 
lowassa amekuwa kete ya sisiem kwa muda sasa na ''heavens only know atakuwa hivyo for a very loooongtime"mpaka mazezeta washtuke kuwa kete hiyo sio issue!
 
Habari za Lowasa kwa sasa si ishu.Ishu ni habari za hali ya kiuchumi mitaani.Maisha ya mitaani hayaridhishi yanakatisha tamaa.Dili za hapa na pale zimeadimika.Haijulikani matumaini ya kupata kazi yatarejea lini.
Kama ulizoea kipato haramu, lazima maisha yatakuwa magumu. Kama una kipato halali, maisha yako vizuri. Usipende kuishi artificial life. Maisha take ni mafupi. Ishi real life, utaishi kwa furaha muda mrefu na hutakuwa unalalamikalalamika.
 
Nitaandika kwa kifupi sana.

Swali ni hili... ajenda kubwa ya upinzani ni ipi?? Jibu ni " kupambana na udikteta chini ya John Magufuli" rais wa tanzania amekuwa dikteta ambaye anaziba watu midomo. Naendelea kujiuliza huyo dikteta ni yupi ambaye anawaacha watu wamuite dikteta... ni dikteta yupi huyo ambae ukivunja sheria anakupeleka mahakaman na bado unashinda,unapewa rufaa..yaan dikteta anakuacha utafute haki Zako katika mahakama (chombo kinachosimamia haki)?? Dikteta anaziba watu midomo au anakuzima hata hiyo sauti hutoi??

Lakini bado najiuliza hivi wananchi issue ya udikteta unaclick kichwani kwa mtu ambaye ameanza kwa kufungua mahakama ya mafisadi? Mtu ambaye anarudisha nidhamu katika offisi za uma? Mtu anaepigania kufanya kazi? Kiongozi ambaye anasafisha mifumo mibovu kama elimu??

Wapinzani chonde chonde yale maisha ya kusubiri udhaifu wa serikali ndiyo mtengeneze ajenda pengine ndiyo wakati sahihi wa kuyaacha.. kila ajenda mnayopigia kelele Magufuli anaifanyia kazi.

Mlikuwa na nguvu kabla LOWASSA hajaja upinzani.. kwa zile kura alizosema mwenyekiti wa chadema mh Mbowe kamati kuuu nanukuu " makamanda kutokana na muda hatutapiga kura za siri.. wanaokubali lowassa simameni mmkunje ngumi hivi"... najiuliza katika mazingira hayo ungeweza kumkataa?? Lakini Lowassa yupo kamati kuu na vikao vyote vya juu anashiriki.. kwa katiba ipi?? Mwenyekiti wa chadema tukisema anatumia mabavu kuongoza chama kama ilivyowahi kulalamikiwa na watu kama Zitto Kabwe nitakosea???

Ukweli ni huu ajenda ya Upinzani ilikuwa ufisadi. Sasa hivi sio ajenda yao tena ndiyo maana ile list of shame wameifuta kwenye website yao ... narudia kumchukua Lowassa was a wrong move . .

Hivi hiyo september 1.. tu assume Magufuli akawaruhusu mufanye mikutano na maandamano ajenda itakuwa ipi??? Udikteta?? Yaani upo kwenye mikutano na unahojiwa kabisa na tv unasema hii nchi rais anaziba watu midomo... nasononeka upinzani unakufa haraka tofauti na nlivyofikiri.
Naunga mkono hoja mkuu umenena mpaka bass...sasa tuwamalize kwa cjui wanawaonaje Watanzania hawa wajamaa na hii saccos yao hiii
1470758065071.jpg
 
Mitaani ndiko maisha halisi ya mtanzania yanakoakisiwa.Dili si lazima ziwe shughuli haramu tu.Pia ni kazi halali zinazompatia mtu kipato,apate mkate wa siku ale ashibe,siku ipite.
 
Back
Top Bottom