Lowassa ni kiona mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa ni kiona mbali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Mar 11, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ni kiongozi makini sana. Ana upeo mkubwa sana wa kufikiri na kutenda. Anathubutu na anawapenda watu wake. Majuzi akiwa katika kijiji cha Lolkisale Monduli Lowassa alisema yeye akiwa mbunge anakusudia kuliomba Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) ililiwaruhusu wanafunzi waliofeli kidato cha nne warudie mitihani. Kweli, Monduli wamepata kiongozi. Taifa linahitaji akina Lowassa wengi.Kama Lowassa, ninaamini kuwa ELIMU KABLA.....
   
 2. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Lowasa kama angekuwa anawapenda watu wake asingeiba na kujilimbikizia mali kiasi alicho nacho sasa. Wakati akiwa waziri mkuu watu wale (waTZ) wakiwa kwenye hali ngumu ya kuhitaji umeme na taifa huku likiwa katika hali mbaya ya kifedha aliamua kuunda "tender board" yake huku akiiacha "tender board" ya TANESCO ili kuipa Richmond mkataba wa kufua umeme ili yeye na rafiki zake wajiongezee pesa zaidi kutokana na jasho la walipa kodi wa TZ. Hakika Lowasa ni adui mkubwa wa waTZ na apaswa kuogopwa kama ukoma.
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kama ni kampeni zenu za Urais 2015, Hapa JF hamna chenu, FISADI NI FISADI, Iweje ashauri warudie Monduri, kwa nin asiwapeleke ktk moja ya shule zake za pale mikocheni? ACHENI USHABIKI UTAOTUDHURU BAADAE!
   
 4. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Hutaweza kumsafisha mzee mvi ndg KAUMZA, ngoja aendelee kuwadanganya wamasai wenzake. Mtoto wa mwalimu ambaye sasa ni bilionea kwa rushwa na umafia wa hali ya juu
   
 5. Mwanaitelejensi

  Mwanaitelejensi Senior Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amekuwa kwenye serikali kwa muda mrefu hana jipya kama angekuwa anawajali watanzania asingetuibia kodi zetu au kutuingiza kwenye mikataba feki
   
 6. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,972
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Anaweza kuwa ni kiona mbali, lakini ni mwizi. Hatuwezi kumwamini kwa kuwa siyo mwadilifu.
   
 7. p

  palehorse Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wazee wetu walilala wakati wenzao wanapigana na maisha na kuwaandalia watoto wao mazingira mazuri na kuibuka akina lowasa.walaumu wazazi wenu.mkiambiwa leteni ushahidi mnasugua meno.ongeeni kama wasomi bwana.stop gossiping.talk with facts
   
 8. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hizi jitihada za kujisafisha kwa EL hata kama ndo maandalizi ya 2015 yanakuja kwa kasi.
  Hivi tunategemewa watanzania tusahau kama digidigi?
  UVCC*, wrong approach, try again.
  kwenye nyekundu isomeke hivi " Kweli Monduli wamepata FISADI. taifa halihitaji MAFISADI kama Lowasa kimoja".
   
 9. M

  Msharika JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  SIGMA, Sina mbavu, umeuwa mchana kweupeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 10. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Lowassa ni kiona mbali lakini si kwa taifa la Tanzania bali kwa mkewe na familia yake.
   
 11. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Lini ameanza kuwa kiona mbali? Umepagawa au umelogwa? Hakika ujinga hauna mipaka. Tafadhali usituletee kejeli. Tuacheni sisi na Tanzania yetu ninyi mliolishwa limbwata la EL
   
 12. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa anayekwenda kwa jina la Lowasa mshipa wake wa aibu umeshakatika na amebakiwa na mshipa wa fedheha tuuu! Hana haya mwana izaya? Ebo.
   
 13. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kimsingi taifa linahitaji watu wenye msimamo wa kimaamuzi kama Lowassa hata hivyo taifa halihitaji watu wezi na wenye kulazimisha maamuzi ya kiuwizi dhidi ya rasilimali na kidogo walichonacho watanzania masikini kama Lowassa

  Kabla hatujafikia mahali pa kumpigia debe mtu mwenye traits zote mbili (UCHPA KAZI NA UWIZI) ni bora tukaangalia katika wanasiasa wetu tulionao kwa sasa kama hakuna mwenye trait mojawapo ya muhimu (UCHAPA KAZI BILA WIZI) na kama hakuna ndipo tuweke resolution ya pamoja kufikiri mchapakazi na mwizi kwa kuwa tutakuwa tumetafitri na kujua hakuna mchapakazi asie mwizi katika tanzania yetu (kama ikitokea hivyo)

  Hata hivyo naamini wapo wachapakazi wasio wezi, hivyo Lowasa hawezi kuwa first priority kwa taifa hili maana bado tunao wachapa kazi wasio wezi, tena wengi.
   
 14. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  SIGMA, teh! teh! Umemaliza mchezo kaka, vijifisadi vidogo havina swaga tena teh!
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Lowasa ndio jembe la CCM, Richmond mwizi alikuwa Kikwete, Lowasa alibebeshwa aibu kulinda heshima ya nchni.
   
 16. t

  talumba mkiwa Member

  #16
  Mar 11, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli mnaomtetea lowasa bado mna akili timamu najaribukuwaza na kuwazia kwani yeye kazaliwa kuwa rais ccm fukuzeni huyu mtu kama hamtaona mabadiliko uande wenu
   
 17. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #17
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  taarifa za kiintelejensia zinaonesha hili limiliki la hii thread ni likada la el na linajiandaa kukumbukwa kwenye uzima wake.
   
 18. J

  Jonas justin Member

  #18
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mafisadi msipoteze muda wenu hapa!
   
 19. mmzalendo

  mmzalendo Senior Member

  #19
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
  kwenda zako kichwa cha panzi wewe ujui kama huyo ni mwizi
   
 20. A

  ANY Member

  #20
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Chumvi ikiishaharibika utaiweka nini irudishe radha yake? HAKUNA! Ni ya kutupa. Mabaya aliyokwisha yafanya EL hata afanye mazuri mangapi kuanzia sasa mpaka kufa kwake kamwe watz hatuwezi kumwamini tena kuwa RAIS wa JMT. Apumzike atuachie nchi yetu.
   
Loading...