Lowassa ni Fisadi na atabaki kuwa fisadi

Shirika la ndege liko wapi, viwanda viko wapi, nenda ziwa victoria huko meli alizoacha nyerere ndio hizo hizo, nini alichofanya zaidi ya mambo maovu kulipuka, vuwanda kufa, meno ya tembo, wanyama kusafirishwa wazima wazima, tunataka mageuzi tuone na wao watafanya nini, tukiona hakuna walilofanya tutarudi kule kule, lakini sio kukalia huko kwa waliokutuma kuja kukashifu watu, kama fisadi ushaambiwa nenda na vielelezo mahakamani, usilalamike ka mbuzi anayetaka kujifungua

Dah upo sahihi kabsa unaweza kuchukulia mfano wa kenya na hatua waliyonayo sasa lkn sijui awa wanaotaka mfumo huo uwepo miaka yte wana mtazamo gan
 
Kiongozi haya unayo yasema umeyatoa wapi? Kama ni mawazo yako sawa ila unapo leta jambo na kulipublicly akikisha una ushaidi ili ushawishi watu na thread yako otherwise itakuwa una leta issue za kizushi na fitina ambazo jf we are not welcome them.. be serious kidogo tuache utoto..
 
kama unaona lowasa fisadi nenda mahakamani tatizo watanzania tuna mambo ya kishoga ndo mana Obama kasema tuwowane tuuu.. nenda mahakamani kalalamike aitwe mpambane na kesi mbona jk kabadilishana ges na wachina kapewa mwanae yeye katoa gesi yupi fisadi sasa
 
Lowassa anajifanya kujitetea eti yeye alitekeleza amri ya bosi wake.
Kama ni kweli kama anavyotaka kutuaminisha kwanini kwa miaka yote minane hakuweka ukweli huu hadharani.

Je, asingekatwa jina huko CCM ina maana hadi leo asingesema nani ni mhusika mkuu katika tuhuma anayokabiliwa ya Richmond?
Kama hakuhusika kwanini hakujitetea wakati ule, akakimbilia kujiuzulu?

Na kama hakuhusika kwani alijiuzulu?

Muda utatuambia, lakini tufahamu kuwa Lowasa ni fisadi, na atabaki kuwa fisadi pamoja na genge lao.
Urais ausahau, atausikilizia tu kwenye vyombo vya habari.

Sana sana alichofanikiwa kufanya sasa ni kuibomoa iliyokuwa hadi sasa ngome kubwa ya upinzani.
Hongera Mbowe na Lowasa kwa kuua CHADEMA.

Upo shallow sana tafuta points zenye masikio.
 
Nitajie maeneo au miradi au project ambayo Lowassa amekula rushwa (usiniambie mambo ya richmond ambao ni mpango wa serikali nzima )
Ukitaja mfano miaka 10 ilopita lowassa alichukua mgao wa escrow
Lowasa alichukua mgao wa mv Dar es salaam
Lowassa anachukua chenji za capacity charges
Lowasa kanufaika na nyumba za serikali
Lowasa kanufaika na miradi ya IPTL
Ukileta ushahidi au kashfa nyengine zilizo ikumba serikali miaka 10 ilopita basi ukileta ushahidi unapata M -Mpesa tshs million moja

MKuu kama hujuwi ni kwamba, Lowasa na swahiba wake Rostam Azizi ndo wazee wa majenereta, wazee wa kutengeneza migao ya umeme na kutuletea mitambo yao. Hata sasa ni mnufaika wa haya makampuni ya umeme wa dharura akishirikiana na Rostam. Lifahamu hilo kama ulikuwa hulijuwi.
 
Dah upo sahihi kabsa unaweza kuchukulia mfano wa kenya na hatua waliyonayo sasa lkn sijui awa wanaotaka mfumo huo uwepo miaka yte wana mtazamo gan

nakwambia kaka tumerogwa na kurogeka hasa, hata uwaeleze vipi wao ni huko huko tena shangwe na vigelegele
 
Muda mwingine huwa najiuliza yale majizi ya escrow yote si yalitoka ccm? Jk aliyafukuza lakini kwenye kura za maoni ya ubunge yamepita tena. Sjui wtz nani katuroga. Mimi nionavyo tuwape ukawa 10yrz mana mijambazi mingi ipo CCM.
 
Ni kweli mkuu!
Wacha nikuulize swali dogo tu!
Ni kwanini Lowasa anautafuta uraisi kwa gharama yeyote ile?

huyu alikwepo kwenye mfumo ujana wake wote na kazeekea huko, mtazamo wangu anataka urais kwa gharama yoyote kwani aliona maozo mengi lakini kutokana na mamlaka alikuwa nayo ilikuwa hawezi fanya lolote, na hakuwa na maamuzi, kama atakuwa mkubwa wa nchi anaweza akaondoa huo uozo, kwani kaka tuna rekodi mbaya sana huko china, africa kusini, kama kwa madiba au china wakiona passport za tanzania, kaka unawekwa kando si kusachiwa huko utadhani we ni gaidi, tukiona na yeye ni yale yale, then back to the roots tumalizwe kabisa kwa sababu hatuna pa kukimbilia, mie kaka yangu nimebahatika kukaa maisha ya vijijini nilikokulia na kielimu kidogo nilichonacho nimejaribu kuona baadhi ya nchi hususani africa, na nimekaa mjini nimeona tofauti, check msumbiji, wao ni wa kutuacha, pesa yao wala hatuikaribii, wanafukuzana na rand, yani zile nchi ambazo tulizisaidia kusaka uhuru zimetuacha, achana na zimbwabwe na zambia, lakini tusifike huko,
 
Hayo ni wewe umesema. Ma ccm mmechanganyikiwa toka lowasa ajiunge chadema .utackia lowasa hoooo lowasa cjui nn poleni Sana kwa kwakuchanganyikiwa mapema hila msiofu kwani ukawa awana tatizo na nyie.
 
Hivi Lowasa angekuwa mgombea wa CCM,Mbowe angeongea kwa namna hii anayoongea ya kumpamba? mbona wanasiasa wanatufanya wajinga kiasi hiki?Nakumbuka wakati mchakato wa kumpata mgombea wa CCM ukiendelea Dodoma,wana Ukawa walikuwa wanaeleza waziwazi kwamba CCM wakimsimamisha Lowasa wamekwisha,kwamba wataweka wazi ufisadi wake,kumbe ulikuwa ni unafiki mtupu
 
Huu ni ukawa ...mambo ya card ni publicity tuu.
Ukawa oyee ..
Siku ya kwanza kufungua kampeni lazima suala la kuonewa kina Ponda na wale masheikh wa 15 wa Zanzibar liwe juu kabisa. Lazima ukawa itetee haki za raia na kupinga unyanyasaji na kutumia dola kutesa wale masheikh.
Ukawa inahitaji ku win hearts and minds za waislam ambao kwa mamilioni wana sononeshwa na uonevu unaofanywa na ccm kwa masheikh wale.
Huu ndio wakati wa kuitoa ccm kabisa na bakwata yao
 
Ufisadi wa Lowassa haujaanzia kwenye Richmond ulianza siku nyingi.

  1. Ingawa hajarithi utajiri wowote, 1993/4 baada ya kufanya kazi umoja wa vijana CCM, miezi michache AICC na miezi michache ya uwaziri, aliweza kujenga jumba la zaidi ya milioni 100 pale Masaki aaliyowapangisha ubalozi wa South Africa.
  2. Wakati wa kinyang'anyiro cha uraisi1995, alikodisha ndege ya kuwapeleka Dodoma akiwa na mshikaji wake JK. Unaweza ongeza vitimbwe vyake hapa....
Kwa ujumla ni kuwa, mara tu baada ya kuondoka UVCCM, Lowassa aliaanza kuiibia serikali aliyokuwa anaifanya kazi na kujilimbikizia utajiri.

Je kwa vile tunaelewa ajira yake tokea amalize shule, yaani utumishi wa serikalini, kwa nini Lowassa asitueleze ameutoa wapi huo utajiri ili tuweze kumsifia au kumlaani?

Kama alivyosema Dr. Slaa, kumkumbatia Lowassa ni kinyume kabisa cha yale yote wanamageuzi waliyokuwa wanapigania kwa miaka yote. Hivi kuna anayenufaika na hii hatua zaidi ya hawa wala rushwa wawili Lowassa na Mbowe?

Umeonaeeeeee! Lowasa hafai kabisa
 
Yule Richmond. Huyu Escro wewe ni Epa au mwengine MV Dar es salam scam au kilwa road scandal su yule kauza nyumba za serikali kwa bei za wizi ....hawa wote ni mafisadi wa mali za umma wote hakuna msafi..lakini tunaweza kufumba macho kwani kumpata safi kabisa ni mgumu ..lakini ni vigumu kumpa kura mtu au chama ambacho kina finyanga haki za raia wake. N vigumu kumpa kura wale walotia ndani masheikh zaidi ya 15 .
Ni vigumu kukirejesha chama kinachoendesha serikali tena huku kikifunga masheikh wale bila ushahidi wa maana. Nafsi yangu inaniambia hio sio haki na dhambi kubwa sana kuwasaidia kurudi tena madarakani wanyanyasaji. Ni dhahiri kila mpenda haki anachukizwa na uonevu huu na waislam wana haki ya kusema sasa inatosha
 
Lowassa anajifanya kujitetea eti yeye alitekeleza amri ya bosi wake.
Kama ni kweli kama anavyotaka kutuaminisha kwanini kwa miaka yote minane hakuweka ukweli huu hadharani.

Je, asingekatwa jina huko CCM ina maana hadi leo asingesema nani ni mhusika mkuu katika tuhuma anayokabiliwa ya Richmond?
Kama hakuhusika kwanini hakujitetea wakati ule, akakimbilia kujiuzulu?

Na kama hakuhusika kwani alijiuzulu?

Muda utatuambia, lakini tufahamu kuwa Lowasa ni fisadi, na atabaki kuwa fisadi pamoja na genge lao.
Urais ausahau, atausikilizia tu kwenye vyombo vya habari.

Sana sana alichofanikiwa kufanya sasa ni kuibomoa iliyokuwa hadi sasa ngome kubwa ya upinzani.
Hongera Mbowe na Lowasa kwa kuua CHADEMA.

Msome vizuri mwenyekiti wa CCM akitamka juu ya Lowasa. "Lowassa si fisadi, alisingiziwa tu"...

attachment.php
 
Back
Top Bottom