Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,556
- 1,394
Harambee si sehemu ya misingi ya imani ya kikatoliki, kwa hiyo kilichofanywa huko mwanza ni njaa za watu wachache wanaotumia kanisa kujifaidisha.
Sidhani kama kuna ukweli ktk hili. na kama likitokea kuwa kweli nadhani kanisa litakuwa limekwisha kabisa. Yaani sipati picha na sina uhakika kama hizi taarifa zimemfikia Pengo na maaskofu wengine wa kanisa langu hili zuri, mweeeeeee! Lowassa kuchangia kanisa katoliki,oooopssssssss! an abomination of the century, pheeeeeeeeeeeeeeeew! Tusubiri tuone kama ni kweli!
Mkuu,Yuko mtu hapa anayeweza kusema mbele ya macho ya Mungu yeye ni bora kuliko Lowasa? Hakuna! Kidini msimamo ni huu: usihukumu ili usije kuhukumiwa!
Kuna anayetaka kusema hapa Lowasa anyimwe kushiriki katika shughuli za kiroho kama kuchangia ujenzi wa kanisa? Kama anaruhusiwa kushiriki na kama Parokia imeona ana uwezo mkubwa wa kuwasaidia, kwanini wasimwalike?
Ukitaka unaweza kumtenga Lowasa kisiasa, ila ukitaka kumtenga kiroho unafanya kosa kubwa. Unakiuka amri ya Mungu inayosema usihukumu (kiroho).
Mkuu,Mimi ni mkatoliki na ninajua kuwa Lowasa hajawahi kualikwa kwenye dhifa za namna hii kwenye majimbo mengi. Niambieni ni lini mliwahi kusikia kuwa Lowasa amealikwa kwenye kuongoza dhifa ya Kanisa Katoliki kama ambavyo ameitwa huko Mwanza. D'Salaam ndiyo makazi ya Lowasa. Mke wake Regina si tu ni mkatoliki mwenzetu bali ni mshiriki mkuu wa mambo ya Kanisa na hadi ametunga kitabu kuhusu ziara yao kule Israel. Lakini jiulizeni kwamba ni lini Edward Lowasa binafsi alipewa nafasi jimboni D'Salaam kama anayopewa huko Mwanza?
Unaweza ukaliona katika mtazamo huo, ila mimi nadhani kwa jinsi huyu Bw. Lowassa alivyotokatoka ktk utumishi wa Umma, Mwenyekiti wa Parokia hawezi kusema huyu Bw. Lowassa ana mahusiano mazuri na jamii au jamii inamkubali, jamii gani anayoizungumzia huyu Mwenyekiti???Jamii hii ni ya sisi Watanzania tulioingizwa mjini na Lowassa na Kundi lake la Wahuni?? Mi nadhani aseme yeye kwa ajili ya tamaa zake za hela ameamua kumualika huyo bwana kwakuwa anafahamiana kwa ukaribu na mafisadi hivyo mafisadi wengi watakuja kutoa fedha haramu hapo kanisani. Under normal circumstance Padri anadhani wachangiaji watatoka wapi kama wana nyakato wameshindwa???Mwenyekiti kapima kaona wananyakato hawana hela hivyo kaamua kusaka hata Fedha haramu ili mradi kanisa lijengwe.
Kanisa litakufa kwa sababu ya tamaa zake za pesa. sasa hivi kama huna pesa huwezi kuwa kiongozi wa kanisa na wala hutothaminiwa. Wenzetu ulaya kanisani hawaendi kwa wingi kama Africa, nadhan walishaona jinsi kanisa linavyopotoka. Kanisa endeleeni kutamani fedha haramu halafu muone mtapoishia. Mungu pia alikataa Sadaka ya Cain kwani alikuwa mchakachuaji. Au katika hili mlilolifanya, Biblia zenu hazina huo mstari wa Cain na Abel???? Kama kanisa mnatamaa hivi, mtashindwa kukemea wafanya maovu.Na ndivyo hali ilivyo hivi sasa. Au mwenyekiti na wewe na Fisadi??
Yupo wapi Mtikila. alikuwa anabweka sana na ufisadi, Rostam akatoa ushahid kuwa Mtikila alimfwata akamkopa hela. Hadi leo Mtikila analiapproach suala la ufisadi kwa aibu sana. Kanisa acheni njaa na tamaa za kipumbavu.
Mimi ni mkatoliki na ninajua kuwa Lowasa hajawahi kualikwa kwenye dhifa za namna hii kwenye majimbo mengi. Niambieni ni lini mliwahi kusikia kuwa Lowasa amealikwa kwenye kuongoza dhifa ya Kanisa Katoliki kama ambavyo ameitwa huko Mwanza. D'Salaam ndiyo makazi ya Lowasa. Mke wake Regina si tu ni mkatoliki mwenzetu bali ni mshiriki mkuu wa mambo ya Kanisa na hadi ametunga kitabu kuhusu ziara yao kule Israel. Lakini jiulizeni kwamba ni lini Edward Lowasa binafsi alipewa nafasi jimboni D'Salaam kama anayopewa huko Mwanza?
Kanisa Katoliki limekuwa ni linaongozakatika kuupinga ufisadi. Askofu wa Jude Thaddaeus wa Dodoma alitoa pongezi kwa wanasiasa walioufichua ufisadi. Askofu huyo alitoa pongezi hizo siku ya kumsimika Askofu Msonganzila kama askofu mpya wa Musoma. Kumbuka ilikuwa ni miezi mitatu baada ya Dr. Slaa kutamka list ya mafisadi na vilevile mwezi mmoja kabla Lowasa hajajiuzulu mwenyewe kwa kushindwa kujitete bungeni kwa tuhuma za ufisadi wa RICHMOND zilizotafitiwa na timu ya Dr. Mwakyembe.
Wakati askofu Jude Thadaesu anatoa pongezi kwa kina Slaa alikuwa askofu wa Dodoma lakini alisoma pongezi zile kama rais wa Baraza la Maaskofu wa Tanzania. Leo, askofu Jude Thaddeus hayuko Dodoma bali sasa yuko Mwanza! Bado ni rasi wa Baraza la Maaskofu!
Halafu hukohuko Mwanza ndiko Lowasa ameanza kuonyesha anakubalika ndani ya Kanisa Katoliki!
Hapa tunahitaji umakini wa hali ya juu. Kwanza nina wasiwasi kama askofu amejulishwa mapema kuhusu uchangiaji huo. Wenye kujua namba za Jimbo Kuu la Mwanza bado siku ya kesho inaweza kutumika kuulizia ofisini kwake kama kweli anajua.
Lowasa hajathibitika kuwa ni fisadi. Lakini hajawahi kukanusha kutohusika na RICHMOND inayotutesa hadi kesho. Kwa nini aliitupilia mbali nafasi ya kujitetea bungeni ambapo ilikuwa ni nafasi ya nzuri ya kujisafisha mbele ya umma kuliko kutumia njia zingine.
Kanisa Katoliki limepinga sana ufisadi. Kama mafisadi hawajaakmatwa na bado kuna wale wanatuhumiwa kwa ukaribu, leo Kanisa linaenda kujiweka karibu nao. Ukweli ni kwamba Kanisa Katoliki linajiweka katika mahala pagumu kwenye vita hii y ufisadi. Lisijilaumu pale litakapoanza kuulizwa "mbona watuhumiwa mnawaalika wanapowachangia hizo pesa zao".
Ninalifahamu hili kanisa langu kuhusu mambo ya ushoga (homosexuality). Ni moja ya maknisa machache kama si pekee ambalo linapinga kwa ukali suala la ushoga. Ninalipongeza liendelee hivyo. Lakini kama linapinga ushoga na hajakamatwa mtuhumiwa wa ushoga basi ina maana kuwa kuwa mtuhumiwa wa ushoga hakumfany mtuhumiwa asikubaliwa na kanisa kuongoza harambee.
Hivyo, Tanzania kuna watuhumiwa wengi tu wa ushoga. Baadhi yao ni matajiri. Maadam hawajatiwa hatiani basi tutarajie nao siku moja tusikie wakiitwa kwenye Parokia mojawapo ili kuongoza harambee! Tusilalamike ikifika huko.
Kanisa lingejifunza kupitia kwenye scandal ya Freemasons. Kitendo cha jamaa wa freemasons kuwa karibu na viongozi wa kanisa katoliki kunalitesa na hadi kuna watu wengi tu wtanaamini kuna uhusiano mkubwa wa Freemasons na Ukatoliki.
Haijapita miaka miwili wenzetu nadhani walutheri walikataa hela ya Rostam Azizi. Naikumbuka issue ile ambapo ilibidi viongozi wa Kanisa waingilie kati na kusema Rostam alialikwa na kikundi cha kwaya na si viongozi wa Kanisa. Kama sikosei ilibidi kile kikundi kirudishe hela zile kwa Rostam na kuomba samahanani.
Je, haya si mazingira yaleyale kama ya case ya Rostam na walutheri wale. Nimelisoma gazeti na mleta mada hajakosea hata nukta. Lakini kama mmesoma vizuri hakuna palipoandikwa kwamba Paroko amemualika Lowasa. Kwa mazingira yaleyale yaaliyopita kwa Rostam, basi inawezekana huyu mwenyekiti wa Parokia ambaye ni mlei ameandaa jambo zima na labda Paroko au padri wa pale ameshirikishwa mwishoni sana.
Kama Paroko hana taarfia basi hata askofu Jude Thadeus wa jimbo hilo inawezekana habari hii ndiyo inamtaarifu.
Habari inaeleza kuwa Lowasa anaushawishi ndicho kigezo cha kumualika hapo parokiani. Hivi lina ukweli hili? Kama ni hivyo mbona hamjasikia Kanisa Katoliki likimualika Reginald Mengi. Ukweli nikwamba kama ninavyoshangaa Lowasa kualikwa nitashangaa kusikia Kanisa Katoliki kumualika Mengi tangu siku Mengi alipotamka kwamba viongozi wa dini wahimize uvaaji wa Condom.
Hayo ndiyo yangu.
mtoto akikunyea mkono utaukata?na kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi.bravo lowasa endelea na juhidi zako. pale magogoni lazima ukae
ROMAN CATHOLIC is that beast revealed in Revelation. Fuatilieni mjue ukweli ili uwaweke huru.Hekalu langu limekuwa pango la wanyang'anyi...mie ni muumini wa katoliki ila kwa hili mauti yataliandama kanisa hili,tunajenga ama tunabomoa?
Ndugu yangu Kieleweke, nami pia ni Mkatoliki tena niliyebahatika kufika mpaka St. Peters, Basilica pale Rome. Pia nimevisoma vitabu vya mwandishi Malachi Martin kuhusu Ukatoliki, lakini kama Mkatoliki mwaminifu, hupaswi kuuzungumzia in public uhusiano huo wa Ukatoliki na Freemasons, na kudai wengi wanaamini!.. Weingi hao ni wewe na hao wengine lakini Wakatoliki wenyewe tunamuamini Mungu Mmoja katika Holly Trinity, na Kanisa ni Moja Tuu!, Takatifu Katoliki la Mitume!.Mimi ni mkatoliki
Kanisa lingejifunza kupitia kwenye scandal ya Freemasons. Kitendo cha jamaa wa freemasons kuwa karibu na viongozi wa kanisa katoliki kunalitesa na hadi kuna watu wengi tu wanaamini kuna uhusiano mkubwa wa Freemasons na Ukatoliki.
Hayo ndiyo yangu.
Kiresua, sisi Wakatoliki, kwanza, tunajutia dhambi zetu, na kujuta huko, tunajutia moyoni, pili tunatubu kwa Mungu na sii kwa mwanadamu, na mwisho tunafanya malipizi kwa kutenda yaliyo mema.Hata kama watu wanacema ELo ametubu wakati hajawahi kutamka maneno either kutoa ufafanuzi wa tuhuma dhidi yake, au kuwaomba msamaha waTZ. Na hi toba n ya Kichina.