Lowassa na safari ya matumaini

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Safari ya MATUMAINI, kwa dhana nyepesi inaweza onekana kama Slogan (MSEMO) tu, si tu kwa wasio wasomi bali hata kwa wasomi wenyewe, watu ambao jamii imewapa nafasi ama fursa kubwa kuzitambua na kuziainisha fursa katika jamii yao.

Mh. LOWASSA mzee wa safari ya MATUMAINI ndiye mwenye nguvu ya utendaji wa kauli mbiu hii,. Lakini kwa nini iwe safari ya MATUMAINI?, nini mantiki yake na je inasadifu uhalisia wa Mh. LOWASSA katika kuyaleta matumaini hayo?, Imeanza lini hii safari,? ni nani mhusika wa safari ya matumaini? Na maswali mengine mengi tu ya kujiuliza juu ya safari hii aliyoianzisha Mh. Lowassa.

MATUMAINI ni uhakika wa kufanya, kutimiza ama kukamilisha jambo kwa mipango iliyotukuka.

Safari ya Matumaini ni uhakika wa Mh. Lowassa wa kutaka kuwatimizia ndoto Watanzania wengi waliokata tamaa ya maisha ili kuwajengea matumaini ya maisha mapya yenye faraja na fanaka na kujiona wenye thamani katika taifa lao.

Msingi mkuu wa Matumaini ya Mh. Lowassa kwa Watanzania yanajikita katika mambo yafuatayo,

° Kujituma,
° Kusimamia
° Kutekeleza
Mambo hayo ndiyo sifa kuu za kiongozi na mwananchi katika kufanikisha Safari ya Matumaini (Ukombozi).

Matumaini ya afya bora, elimu bora yenye ushindani, huduma za maji safi, barabara zinazopitika, masoko ya mazao ya wakulima, kilomo cha kisasa n.k.

Matumaini ya ajira kwa Watanzania, ajira ajira ajira si tu ni bomu linalosubiri kulipuka bali Cancer ambayo inahitaji matibabu kwa uharaka zaidi.

"Nachoshwa na Umasikini, nchi yetu ina rasilimali za kutosha, hatupaswi kuwa masikini" by LOWASSA.

Mtetezi, mtekelezaji na msimamiaji, tumuunge mkono Edward LOWASSA.
 
Toa njaa zako hapa jf, Mtanzania yeyote mwenye kumbukumbu sahihi na akili TIMAMU kamwe hawezi muunga mkono Lowasa awe RAIS wa Taifa letu! nasema hivyo kwa sababu kubwa moja, Lowasa ni miongoni mwa MAFISADI MAPAPA, ni mtu ambaye kwa nchi zingine zenye utawala wa kuwajibika angeshapigwa risasi hadhalani mchana kweupe!
 
Kitakule
Kumbukumbu uliyonayo umeifanyia kazi na ukajua ukweli a ndio ulicholishwa kama kinda la ndege bila kujua kilikotoka na asili yake basi umelipuka na msimamo bandia acha hizo tumia kichwa nchi hii ni zaidi ya uionavyo amka utajiumiza.
 
Kitakule
Kumbukumbu uliyonayo umeifanyia kazi na ukajua ukweli a ndio ulicholishwa kama kinda la ndege bila kujua kilikotoka na asili yake basi umelipuka na msimamo bandia acha hizo tumia kichwa nchi hii ni zaidi ya uionavyo amka utajiumiza.

jina zuri sana kwa maana yake,lakini nakuona hulitendei haki jina lako "MLOKOZI" Lowasa hafai kuwa Rais wa Taifa hili,kama wewe miongoni mwa TEAM LOWASA ,basi huenda nawe ni KAFISADIl KADOGO ambako ni UNDERGROUND,lakini pole sana!mie siyo mtoto mdogo historia ya Lowasa na record zake chafu nazifahamu vizuri sio kama wewe mfuata upepo!lakini yote kheri tutakutana August majukwaani!
 
Toa njaa zako hapa jf, Mtanzania yeyote mwenye kumbukumbu sahihi na akili TIMAMU kamwe hawezi muunga mkono Lowasa awe RAIS wa Taifa letu! nasema hivyo kwa sababu kubwa moja, Lowasa ni miongoni mwa MAFISADI MAPAPA, ni mtu ambaye kwa nchi zingine zenye utawala wa kuwajibika angeshapigwa risasi hadhalani mchana kweupe!

Lete ushahidi hapa. Kama huna muache mzee wa watu agombee! By the way,nitajie mtu ambae siyo fisadi na mpigaji hapa Tanzania,kadri ya mtu mmoja mmoja mahali pake pa kazi. Wote ni wapigaji,tuache uongo hapa!
 
Lowassa wenu vigezo vinamtupa kwa nini hamsikii?


[h=1]Kigezo[/h] [h=1]Jaji Agustino Ramadhani[/h] [h=1]Edward Ngoyayi Lowassa[/h]
[h=1]Umri[/h] [h=1]Miaka 70[/h] [h=1]62[/h]
[h=1]Elimu[/h] [h=1]Ni ya juu ngazi ya shahada ya sheria[/h] [h=1]Elimu ya juu ngazi ya shahada[/h]
[h=1]Uzoefu wa kazi[/h] [h=1]Amebobea kwenye mhimili wa dola upande wa mahakama[/h] [h=1]Amebobea kwenye mhimili wa dola upande wa serikali na bunge[/h]
[h=1]Uadirifu[/h] [h=1]Hakuna mashaka yoyote kuhusu uadirifu wake[/h] [h=1]Kuna mashaka mengi sana kuhusu suala la uadirifu[/h]
[h=1]Kazi alizofanya[/h] [h=1]Jaji, mwanajeshi, mchungaji[/h] [h=1]Kichunga ng`ombe, katibu wa chama, mkurugenzi IACC, mbunge, waziri, waziri mkuu.[/h]
[h=1]Historia kazini[/h] [h=1]Amefanya kazi serikalini hadi amestaafu kwa mjibu wa sheria[/h] [h=1]Alijihudhuru uwaziri mkuu kwa tuhuma ya kuipa tenda ya kufua umeme na kuiuzia Tanesco kampuni ya richmond ambayo haikuwa na sifa[/h]
[h=1]Kugombea urais[/h] [h=1]Hajawahi kugombea labda hii itakuwa ni mala ya kwanza[/h] [h=1]Aligombea mwaka 1995 jina lilikatwa kwa kukosa sifa[/h]
[h=1]Hali ya kugombea urais iliyopo hivi sasa[/h] [h=1]Ameombwa agombee tena ameombwa sana[/h] [h=1]Alianza mda mrefu kuonyesha nia ya kugombea urais, kuna mashaka mengi anahonga, ananunua makundi ili yamuunge mkono[/h]
[h=1]Afya[/h] [h=1]Afya yake ni imala sana[/h] [h=1]Afya ni mgogoro mala nyingi huenda Ugermani kupima afya, mala kadhaa huwa na kitetemeshi hasa asubuhi, hana uwezo wa kuhimili mikikimikiki kwa mda mrefu[/h]


[h=1] [/h]
 
Back
Top Bottom