mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Maalim Seif na Lowassa kesho kupanda jukwaani kumnadi mgombea wa ubunge jimbo la Dimani, Zanzibar Abdulrazaq Ramadhan (CUF)
=======
Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Mh. Edward Ngoyai Lowasa, kesho ataambatana na aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi, CUF Maalim Seif Sharifu Hamad kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Dimani Zanzibar.
Makada hao kwa umoja wao, watamnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya CUF. CHADEMA pia wametoa ratiba kamili ya kampeni hizo zenye mchuano mkali hasa baada ya CCM kuzindua kampeni zao juzi jimboni humo ambapo Ndg Abdulrahiman Kinana (comred) alikuwa mgeni rasmi.
Chanzo: MWANANCHI