Lowassa na Kilimo Kwanza: Wengi Hatujamwelewa

AshaDii

Je una amini katika dhana ya kupanga ni kuchagua? Naelewa msingi wa hoja yako, na tumefkia hatua ambayo tunahitaji a 'balancing act' kwani pamoja na ukweli kwamba sekta ya kilimo bado ndio mwajiri mkubwa wa taifa letu, lakini ajira katika non-farming sector nayo inazidi kukua ingawa haya sio matokeo ya sera za makusudi za serikali kukuza ajira, bali ni ujanja ujanja tu wa wananchi kukabiliana na nguvu za Privatization, Liberalization na Marketization.

Mbaya zaidi ni kwamba, tofauti na how wenzetu experienced na maendeleo ya sekta ya kilimo (mapinduzi ya kijani), sisi hizi non-farming activities hazina linkage ya maana na sekta ya kilimo. Sasa implication yake kisera ni nini? Je, tuongeze uhudi kwenye Elimu kuongeza poductivity ya watanzania ili waweze kujiendeleza kwenye non - farming activities? Na je, tunapoongelea Elimu katika mazingira ya kilimo, tunaongelea elimu ya jumla ambayo inaweza tumika sekta yoyote au specifically for kilimo?

I remain convinced kwamba Tanzanai tuna utafiti wa kutosha wa kilimo, tena mwingi tu unaozalishwa na vyuo na taasisi zetu za kilimo zilizopo. Kwa mfano Koffi Annan na pia Rais wa EU walikuja mapema mwaka huu kutembelea research centre yetu ya Kilimo kule Mbeya n.k na kujionea mengi. So tatizo sio ukosefu wa utafiti kuhusu Kilimo bora, bali linkage baina ya utafiti uliopo na shughuli au hali halisi huko mashambani.

Naamini ndio katika dhana ya kupanga na kupangua… Naomba nikujulishe kuwa naelewa where it is coming from na kwa nini hasa unaamini kuwa kuchagua moja ama lingine itakuwa bora zaidi. Ningekubaliana moja kwa moja na hilo iwapo kama viongozi wetu wangekuwa wanyoofu katika utendaji. Kwamba unajuwa kabisa kuwa EL (ama yeyote yule) akizungumzia 'Elimu Kwanza'; kweli kutakuwa na mabadiliko chanya for the better nchini na kwa wananchi.... vivo hivo MP akiongelea na kumaanisha upande wa 'Kilimo Kwanza'. Hio inakatisha tamaa Mchambuzi kuanza kujadili kipi bora kati ya hayo mawaili...

Najitahidi nitoe hoja sio kwa msingi wa kipi bora kati ya hayo mawili, bali nitoe kwa kipi ambacho hata kikijadiliwa ndio hasa ambacho inabidi kufanikisha ili kuweza fika malengo (malengo ambayo yameegemea maendeleo kwa kudhatiti na kuboresha maeneo husika). Kwa maneno mengine naweza Kimsingi na ki depth wa kipi bora zaidi mimi na wewe twaweza kuwa pamoja ila tutapishana padogo kwa kipi zaidi; kati ya kuboresha moja ya hayo mawili (Elimu na Kilimo) AMA kuwa lolote ni sawa na tatizo ni utendaji…

Nakubaliana na wewe na hio lack ya linkage kati ya non-farming activities na kilimo. Na ndio mana naomba nikurudishe nyuma, kuwa nimesisitiza kuwa kama moja ya hayo yakipewa uzito (in this case tuseme Kilimo kwanza); hata hilo tatizo la kutokuwa na link kati ya sekta ya kilimo na mengineyo yatajisolve automatically… Mchambuzi lets say ‘Kilimo Kwanza' ikapewa kipau mbele IPASAVO…

Kwa vyovyote ina maana kuwa mengi ambayo ni weaknesses kwa sasa yataboreshwa kama vile viwanda vya Processing vitafufuliwa, Taasisi za kujitegemea zihusuzo Kilimo zitaanzishwa na kuboreshwa, Watafiti/wajuvi/wadau wa Kilimo watasimamiwa na kupewa support vilivo na mengine mengi. Can you imagine namna gani change inaweza tokea iwapo pale manifesto ya Kilimo kwanza ikawa implemented vilivo from start to the full stop inavoweza leta change katika kila Nyanja? Iwe Elimu, iwe uchumi, iwe ajira, iwe soko la ndani na la dunia… (Haya maelezo ni applicable kama pia Elimu ikasimamiwa vile ambavo kweli inatakiwa isimamiwe… Sio kama ilivo saizi ambapo inakuwa more out of obligation zaidi ya Malengo ya kuoboresha).

Umeuliza kuwa; tunapoongelea Elimu katika mazingira ya kilimo, tunaongelea elimu ya jumla ambayo inaweza tumika sekta yoyote au specifically for kilimo? Kwa hapo naomba niwe wazi kwa kusema nililenga kuzungumzia kuwa Elimu ya kilimo itapewa kipaumbele kuliko ilivo sasa.

Hio paragraph yako ya mwisho, kaka nakubaliana na kila ulilo zungumza hapo. Kwamba nimetoa impression kuwa kuna ukosefu wa utafiti kuhusu Kilimo bora? Hapo basi sijajieleza vema sababu siamini hilo. Naomba niongezee kuwa NAAMINI kuwa Tanzania tuna karibu kila kitu kwa sasa on paper kinachohusiana na sector nyingi, ikijumuisha matatizo, namna ya kuboresha, namna ya kunufaika n.k. Narudi pale pale kuwa haijalishi kipi kinaanza, what matters ni utendaji wa hao viongozi katika kile ambacho wataamua kusimamia na kuhakiki kinafanikiwa kwa kuweka kabisa timeframe ya malengo yao.
 
Mzee Mwanakijiji,

Nashukuru sana kwa mchango wako mzuri. Kwa kweli nimependa sana dhana yako ya UONGOZI BORA KWANZA, na kwamba mengine yafuate baadae. Hii ni sahihi kabisa.

Tukimrejea Lowassa kidogo, muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, aliwahi fanya interview moja nje ya nchi (ipo youtube) ambapo alielezea mikakati mingi ya maendeleo kwa taifa letu, Elimu ikiwa ni moja wapo. Lowassa alipata tamka kwamba: "An Empty Stomach Cannot Feed an Empty Head." Hii ina maana anatambua umuhimu wa sekta ya Kilimo katika Maendeleo ya taifa. To what magnitude? Hilo hajafafanua kwa ufasaha.

Ni muhimu tukajiuliza, Je, kama Taifa, tunalenga kufanikisha nini hasa na sera zetu Sekta ya Elimu? Mwalimu Nyerere aliwahi kulizungumzia hili kwenye chapisho lake la "Education for Self Reliance", pale anaposema:

"Only when we are clear about the kind of society we are trying to build can we design our educational services to serve our goals."

Je, Elimu ina mchango kiasi gani kwenye Maendeleo ya Sekta ya Kilimo? Mwalimu pia analizungumzia hili kwa mapana sana katika chapisho lake hili, kwa mfano kuna sehemu anatamka kwamba:

"However much agriculture a young person learns, he will not find a book which will give him all the answers to the detailed problems he will come across on his farm. He will have to learn the basic principles of modern knowledge in agriculture and then adopt them to solve his problems."

Umezungumzia kidogo kuhusu tatizo lililopo sasa ambapo vijana wengi wanaomaliza Elimu zao, hawana interest ya kwenda kutumikia sekta ya Kilimo. Je tatizo lipo wapi? Je ni bajeti ndogo? Kama suala ni fedha, kwa mujibu wa bajeti ya mwaka wa fedha 2012-2013, serikali imetenga shilling billioni mia moja (100 billion) kwa ajili ya kutoa mikopo sekta ya Kilimo kupitia taasisi za TIB na benki mpya ya Maendeleo ya Kilimo. Je, will it deliver? Mimi nadhani tatizo lipo kwenye maandalizi ili kusaidia sekta ya kilimo iweze ‘to take off';

I believe kwamba ili kufanikisha Kilimo Kwanza, ni muhimu serikali katika hatua ya awali kabisa ikatengeneza mazingira ya kuwezesha Maendeleo ya kilimo to ‘take off', na this should involve kuitazama upya land tenure system kwani iliyopo sasa doesn't provide the necessary incentives kwa wakulima; na pili ni kujenga positive attitudes towards change (agricultural transformation) miongoni mwa rural households, hasa vijana; ni lazima waone in black and white, what's in there for them; haya yatasaidia kuweka mazingira ya ‘take off';

Ningependa kumalizia kwa quote ya Mwalimu on ‘Education For Self Reliance'. Nadhani mengi anayoyasema hapa tunayaona leo, hasa hili la Sekta ya Elimu not to deliver kwenye masuala ya msingi ya taifa letu:

["The few who go to secondary schools are taken many miles away from their homes; they live in enclave, giving permission to go into the town for recreation, but not relating the work of either town or country to their real life – which is lived in the school compound. Later a few people go to university. If they are lucky enough to enter Dar-es-salaam University College they live in comfortable quarters, feed well, and study hard for their Degree. When they have been successful in obtaining it, they know immediately that they will receive a salary of something like £660 per annum. That is what they have been aiming for; they may also have the desire to serve the community, but the idea of service is related to status and the salary which a university education is expected to confer upon its recipient. The salary and status have become a right automatically conferred by the Degree"

"It is wrong of us to criticize the young people for these attitudes. The new university graduate has spent the larger part of his life separated and apart from the masses of Tanzania; his parents may be poor, but he has never fully shared that poverty. He does not really know what it is like to live as a poor peasant. He will be more at home in the world of the educated than he is among his own parents. Only during vacations has he spent time at home, and even he will often find that his parents and relatives support his own conception of his difference, and regard it as wrong that he should live and work as the ordinary person he really is. For the truth is that many of the people in Tanzania have come to regard education as a meaning that a man is too precious for the rough and hard life which the masses of our people still live."]

J.K. Nyerere, Education For Self Reliance (1967).
 
mambomengi

Ni kweli, mchango wa kilimo katika uchumi umepungua, kwahiyo dhana kwamba Kilimo ni uti wa mgongo imepungua uzito, lakini kusema hivyo ni tofauti na kusema kwamba umuhimu wa sekta ya kilimo umepungua, umuhimu upo pale pale kama sio kuongezeka.

Kilimo ni muhimu sana for food security, mapinduzi ya viwanda, lakini muhimu zaidi, bado ni mainstay when it comes to nguvu kazi, na ni muhimu kufanikisha mapinduzi ya kijani/kilimo ili tuweze ku - diversify uchumi wetu ili nguvu kazi katika sekta ya kilimo iwe more productive, lakini pia ianze kuhamia sekta nyingine.

Yote haya i.e. mapinduzi ya Kilimo yatafanikiwa iwapo tutafanya kilimo kuwa important sasahivi, sio baadae. Suala la elimu linaweza kuwa a complimentary good in the process...

Je ni kweli nchi yetu (ama serikali yake na viongozi wake) wametoa kipaumbele kwa kilimo? Kauli mbiu ya Kilimo kwanza na dhana ya kilimo ni uti wa mgongo hazitaleta Mapinduzi ya Kilimo. Pia tujiulize kuwa wale wahitimu wetu wa SUA wamefikisha malengo yaliyoanzisha kile chuo kikuu?
Kinachohitajika sasa hivi ni kuwezeshwa wakulima (wenyeji na sio wahamiaji) walime kwa kutumia nyenzo za kisasa waondokane na kutegemea majembe ya mkono na mvua za vuli na masika. Tuweke siasa kando tufanye mambo ya kitaalamu zaidi kwenye sekta ya kilimo ilikuleta mageuzi endelevu.
 
Mkuu Mchambuzi umezungumzia kitu cha msingi hapa
I believe kwamba ili kufanikisha Kilimo Kwanza, ni muhimu serikali katika hatua ya awali kabisa ikatengeneza mazingira ya kuwezesha Maendeleo ya kilimo to ‘take off', na this should involve kuitazama upya land tenure system kwani iliyopo sasa doesn't provide the necessary incentives kwa wakulima

Nitaendelea kubaki na msimamo wangu kuwa Kilimo Kwanza ni mpango wa watu wachache kujimilikisha ardhi (Land grabbing) kwa manufaa yao wenyewe. Kwa ushahidi ipitie hii video Sun Biofuels
Utaamini ninachomaanisha. Pasipo kupitia upya Land Tenure in Tanzania, KILIMO KWAZA Tanzania itakuwa ni kama mtu anayeota kujenga nyumba angani (Ndoto za mchana). Mifano ipo mingi sana ukienda Zimbabwe hali ni mbaya sana wananchi wa kawaida hawana ardhi (Thanks to Mugabe at least amejaribu kumilikisha ardhi kwa wazawa). Tusipokuwa makini kwenye umilikishwaji wa ardhi kwa tunaowaita wawekezaji tutakuja lia na kusaga meno.
 
Falsafa za Eddo ziko wazi,

Bila Elimu hata hicho kilimo kitafeli tu!! Angalia Zimbwabwe, wale Ma-settler waliokua na mashamba makubwa mfano wa hapa mpaka chalinze walikua na elimu ya juu sana kuhusu kilimo, hawakua wanategemea mvua ya Mungu, na walikua wakianza kilimo tu, wanakua washajua watavuna tani ngapi, +/- erro zinakua ndogo sana.

Sasa Bongo tunadanganyana na sera za kilimo kwanza wakati wakulima hawajui hata hayo mazao watauzaje,
elimu ya kilimo kando,
elimu ya kutunza mazao kando,
elimu ya kuvuna kando,
elimu ya kuhifadhi kando,
elimu ya kuuza kando,
hawajui hata bargaining,
wamakuja matapeli wa kikenya na kuwatapeli wakati wao wanaenda kutajirika.

Kilimo kwanza imekua ni mradi wa wachache kuingiza zana za kilimo bila kodi huku wakiwanyonya wakulima kwa kuwauzia kwa bei kubwa.

Vocha ghalani ni wizi, pembejeo zinatolewa kwa rushwa na kujuana, hakuna mikopo kwa wakulima, yaani wanaibiwa sana kutokana na ukosefu wa elimu.

Tanzania still bado tuna un-utilized arable land kubwa tu lakini hakuna anaefikiria kwenda kule.

Elibu kwanza, ndio Kilimo kifuate!!
 
Natumaini wanasiasa wanapoweka vipaumbele vya taifa hawasukumwi na uzalendo juu ya maeneo wanapotoka, hivyo kuweka vipaumbele kwenye sekta ambazo ni relevant zaidi na maeneo wanayotoka. Kwa mfano, sio kila jamii Tanzania inategemea Kilimo zaidi, kuna jamii nyingine hutegemea ufugaji, na kuna jamii nyingine zinahisi kwamba historia haikuwatendea haki kuhusu suala la Elimu n.k, hivyo kuwa na uwezekano wa wanasiasa kupigia debe masuala yanayonyanyua maeneo yao - iwe Elimu, Kilimo, Ufugaji n.k. Sina maana kwamba maamuzi ya wanasiasa wetu yanafuata tabia hii, bali nachofanya ni kutoa angalizo tu.
 
Mkuu wangu Mchambuzi nimefurahi kuleta hili nukuu la Nyerere ambapo anasema "“Only when we are clear about the kind of society we are trying to build can we design our educational services to serve our goals.”


Sasa utaona kuwa hapa Nyerere amesema kitu kizito sana (extremely profound). Mtu anaweza kujenga nyumba kwa kadiri anavyotaka. Lakini mtu mwenye hekima anajiuliza kwanza anataka nyumba ya namna gani na yenye kukidhi mahitaji gani ndio atatoka kujenga. Lakini pamoja na hilo atajikuta analazimika kuangalia ardhi na vitu vingine ili kuamua nyumba inajengwaje.

Ninaamini kabisa kuwa hatujui tunataka kujenga Tanzania ya namna gani. Mpango wao (CCM) wa maendeleo wa hivi karibuni una lengo kubwa la hatimaye kuifanya Tanzania kuwa ni taifa la viwanda. Kuna njozi ambayo hata baadhi ya viongozi wa upinzani wanaamini kuwa Tanzania inaweza kweli kuwa taifa la viwanda. Kwa kweli sijui ni nani alikuja na njozi hiyo. Ukifikiria sana tulipoamua kuwa taifa la Kilimo tuliwekeza na kujaribu kufanya kila tuwezalo kufanya hilo liwe kweli. Tatizo la kujaribu kufanya Tanzania kuwa taifa la viwanda ni kuwa ni njozi isiyowezekana.

Tukiamua kuwa tujenge taifa la kilimo basi elimu na sekta nyingine zote zitazunguka kwenye kilimo na kusupplement kilimo. Sijui kama hili tunalielewa ipasavyo. Ni kilimo tu ndicho kinachoweza kuinua mamiliioni ya watu wetu kutoka kwenye umaskini wa kutupwa.
 
Mchambuzi my brother

I HAVE ALWAYS BELIEVED KILIMO KWANZA MISSION IS ANOTHER AVENUE FOR A FEW GREED INDIVIDUAL TO GRAB LAND, WIN MEGA PROCUREMENT CONTRACT AND BENEFIT FROM THE WHOLE SCUM

If we really wamted kilimo kuongoza (kuwa kwanza), basi tungeanza na the whole agricultural/food industry system preparations, mapping our assets and liabilities, formalize policies, infrastructures, resources assessment nk halafu, hata kama ni kwa kusubiri 5 years, kuanza kilimo kwanza tukiwa tayari kwa kila jambo hata fomu tu za kuhifadhia mazao kuwa standardized... looks like ujamaa but nope,

KILIMO HAKIWEZI KUWA KWANZA WAKATI ADRHI INAYOTUMIKA KULIMIA HAIJAWA KWANZA KWENYE MIPANGO "FORMAL"
 
Mada nzuri hii ningependa ingejadiliwa Kama ilivyo kijamii lakini nasikitika sivyo ilivyotarajiwa pamoja na tahadhari ya kutokujadili Mtu inaonyesha inamjadili mtu mmoja zaidi kwa makusudi au Bahati mbaya kipengere cha kwanza tuu katajwa Mtu mmoja Mara nne jumla hoja nzima imemtaja Lowassa pekee Mara sita achilia mbali maoni ya wachangia pekee utaona ni lowassa zaidi hapa nahisi ni kumjadili mtu au Mtu mwenyewe kujielezea zaidi kuhusu hoja hii.

Maoni yangu kwa mada hii ni mafupi tuu Kama ni vipaumbele kwenye kilimo ni Mhimu wakati huu kuliko wakati mwingine wowote lakini kwanini hatuoni mabadiliko yeyote inaonyesha tokana na upangaji wa bajeti katika mgawanyo mipango ya utekelezaji chunguza bajeti zote za ufisadi na mafisadi zinaegemea zaidi kwenye utawala zaidi kuliko utendaji wa mradi inapunguza nguvu kazi za utendaji wa moja kwamoja na kufanya kufeli kwa utekelezaji. Ukisema kilimo kwanza hakiwezi kufanikiwa ikiwa unajenga barabara za mjini na kuacha za vijijini yanapotakiwa kutoa uzalishaji wa mazao ya kilimo unaposema kilimo kwanza huwezi panga bajeti Kubwa kwa chai ofisini ukasahau posho za mabwana shamba vijijini.

So utaona hoja hapa sio kipaumbele kibaya hoja ni aina gani ya uongozi unaosimamia vipaumbele hivyo Kama ni wa kifisadi unaowaza kuweka mazingira ya kufanikiwa kwa ujanja ujanja kupitia fedha za miradi na sio mafanikio kiutendaji ndipo miradi mingi hukwama Hapa niseme Fisadi yeyote Hana sifa ya kusimamia mradi wowote hata wa kufagia barabara ya mtaani kwenu ukategemea utakafanikiwa achilia mbali wa kitaifa.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mchambuzi nakubali mapendekezo yako
katika suala la Elimu na Klimo nini kipewe kipaumbele....

Elimu tayari imeshapewa kipaumbele kwa kuwa na sera ya Kila shule kwa kila kata.... japoa wanaofanikiwa kwenda elimu ya juu/chuo ni wachache kwa wastani ya idadi ya wanaomaliza la saba kwaiyo wengi wanaishia kati ....

kuhusu Kilimo hili suala linahitaji msukumo (empowerment) na viwezeshaji (Facilities).. pamoja na willingness ya Mkulima Mwenyewe...
 
Kimsingi Lowasa amekurupuka kwa nia ya kujitafutia umaarufu. Labda wote tuulizane, yeye yu Serikali ipi? Kilimo Kwanza kama Azimio (resolution) ina nguzo zake ambazo utekelezaji wake ndio tungejiuliza upoje. Hiyon ya ELIMU KWANZA haina mantiki kwani katika Nguzo za kILIMO KWANZA ELIUMU IPO::http://www.tzonline.org/pdf/tenpillarsofkilimokwanza.pdf
 
Mchambuzi my brother

I HAVE ALWAYS BELIEVED KILIMO KWANZA MISSION IS ANOTHER AVENUE FOR A FEW GREED INDIVIDUAL TO GRAB LAND, WIN MEGA PROCUREMENT CONTRACT AND BENEFIT FROM THE WHOLE SCUM

If we really wamted kilimo kuongoza (kuwa kwanza), basi tungeanza na the whole agricultural/food industry system preparations, mapping our assets and liabilities, formalize policies, infrastructures, resources assessment nk halafu, hata kama ni kwa kusubiri 5 years, kuanza kilimo kwanza tukiwa tayari kwa kila jambo hata fomu tu za kuhifadhia mazao kuwa standardized... looks like ujamaa but nope,

KILIMO HAKIWEZI KUWA KWANZA WAKATI ADRHI INAYOTUMIKA KULIMIA HAIJAWA KWANZA KWENYE MIPANGO "FORMAL"
Janjaweed,

Ni kweli kabisa, kwani kwa kiasi kikubwa sana, Kwanza ni kwa faida ya wanasiasa wanaojinyakulia ardhi kubwa ili kuja fanya mambo yao na wawekezaji wakubwa, na pia ni kwa faida ya wakubwa kadhaa wakishirikiana na wafadhili wao wa kisiasa (wafanyabiashara wakubwa) ambao wapo mpaka wafanyabiashara wenye hisa kwenye Jeshi letu i.e. Suma - JKT , na ndio walikuwa mstari wa mbele kuleta matrekta ya kichina.

Based on experience za wenzetu, suala la matrekta katika agricultural transformation, linakuja baadae sana; it has to begin na kilimo kinachohimiza labour - intensive methods, and cost savings, hasa to take advantage of the abundant labour in the sector, lengo lakini ikiwa kuongeza productivity of this labour over time, na vile vile growth ya Kilimo; thats how in the long run, Kilimo kitazalisha na kuwezesha taifa kupata fedha za kunyanyua sekta nyingine kama vile Mzee Mwanakijiji alivyoelezea awali; hakuna sekta itakayopiga hatua ya maana bila kwanza kilimo kunyanyuka; kunyanyuka kwa kilimo ndio kunyanyuka kwa sekta ya viwanda n.k; Mafanikio ya kukua kwa sekta ya kilimo na increase in productivity of labour yatapelekea sekta nyingine kukua, and in the long run, kufungua ajira sekta nyingine, hivyo kilimo kuanza ku release labour taratibu;

Vinginevyo kinachoendelea sasa ni Kilimo Kwanza, Wakulima Mwisho.
 
Mchambuzi nakubali mapendekezo yako

katika suala la Elimu na Klimo nini kipewe kipaumbele....

Elimu tayari imeshapewa kipaumbele kwa kuwa na sera ya Kila shule kwa kila kata.... japoa wanaofanikiwa kwenda elimu ya juu/chuo ni wachache kwa wastani ya idadi ya wanaomaliza la saba kwaiyo wengi wanaishia kati ....

kuhusu Kilimo hili suala linahitaji msukumo (empowerment) na viwezeshaji (Facilities).. pamoja na willingness ya Mkulima Mwenyewe...
Na haya ni muhimu sana kuyafanyia kazi kisera katika hatua za awali kabisa ambazo ni key for kilimo to "take off"; suala la land tenure system ni muhimu ili kujenga incentives za kutosha kuliko hali ya sasa ambapo wakulima hawana uhakika na masuala ya umiliki wa ardhi; vile vile lazima kuwe na mkakati maalum wa kujenga positive attitudes towards change huko vijijini kuhusu kilimo kwanza, ni muhimu rural households, hasa vijana waone bayana whats in there for them; haya ni mambo ya kufanya katika kipindi cha angalau miaka mitano kama janjaweed anavyohimiza; vinginevyo viongozi wetu wanafanya makosa ya makusudi kabisa kuamini kwamba the necessary per-conditions for agricultural transformation already exists; as of now, what exists ni loopholes za kula fedha za walipa kodi kupitia sera ambayo it was already a failure at its inception; tukumbuke kwamba njia pekee ya kuhalalisha wizi wa fedha za walipa kodi ni miradi miradi ya ovyo tunayoaminishwa ni kwa maslahi ya taifa; tumepoteza fedha nyingi sana kwa njia hii;
 
Janjaweed,

Ni kweli kabisa, kwani kwa kiasi kikubwa sana, Kwanza ni kwa faida ya wanasiasa wanaojinyakulia ardhi kubwa ili kuja fanya mambo yao na wawekezaji wakubwa, na pia ni kwa faida ya wakubwa kadhaa wakishirikiana na wafadhili wao wa kisiasa (wafanyabiashara wakubwa) ambao wapo mpaka wafanyabiashara wenye hisa kwenye Jeshi letu i.e. Suma - JKT , na ndio walikuwa mstari wa mbele kuleta matrekta ya kichina.

Based on experience za wenzetu, suala la matrekta katika agricultural transformation, linakuja baadae sana; it has to begin na kilimo kinachohimiza labour - intensive methods, and cost savings, hasa to take advantage of the abundant labour in the sector, lengo lakini ikiwa kuongeza productivity of this labour over time, na vile vile growth ya Kilimo; thats how in the long run, Kilimo kitazalisha na kuwezesha taifa kupata fedha za kunyanyua sekta nyingine kama vile Mzee Mwanakijiji alivyoelezea awali; hakuna sekta itakayopiga hatua ya maana bila kwanza kilimo kunyanyuka; kunyanyuka kwa kilimo ndio kunyanyuka kwa sekta ya viwanda n.k; Mafanikio ya kukua kwa sekta ya kilimo na increase in productivity of labour yatapelekea sekta nyingine kukua, and in the long run, kufungua ajira sekta nyingine, hivyo kilimo kuanza ku release labour taratibu;

Vinginevyo kinachoendelea sasa ni Kilimo Kwanza, Wakulima Mwisho.

kweli kabisa

Mimi huwa naona tunakurupuka tu kwenye kilimo (ni kama ilivyokua kwenye kwenye madini, we need to draw sheria, dira, taratibu, policies, mikakati na systems nzima bila kuangalia nani yupo wapi )

Sijawahi kusikia cha kwanza kuletwa ni power tillers wakati forecasting and quantification ya the whole system demand haijakaa sawa, wanapiga mahesabu "kwa kila wilaya" nk.

Ni kiini macho....
 
Mpango wao (CCM) wa maendeleo wa hivi karibuni una lengo kubwa la hatimaye kuifanya Tanzania kuwa ni taifa la viwanda. Kuna njozi ambayo hata baadhi ya viongozi wa upinzani wanaamini kuwa Tanzania inaweza kweli kuwa taifa la viwanda.

Well said Mzee Mwanakijiji, na tunaendelea kupoteza fedha nyingi sana kwenye sera za industrialization ambazo kamwe hazitazaa matunda. Mapinduzi ya viwanda yataletwa tu na jasho la wakulima likitumiwa ipasavyo. Juzi kwenye hotuba ya kufunga mjadala wa wizara yake ya Viwanda, Dr. Kighoda alinishangaza sana na kauli zake kuhusu jinsi gani tutafanikiwa kuwa taifa lenye viwanda; navyoelewa, Dr Kigoda ni mchumi mzuri, so ilitakiwa aelewe kwamba atakayoenda eleza bungeni sio sahihi. Yapo kwenye hansard, nikipata muda nitayaleta humu.

Tukiamua kuwa tujenge taifa la kilimo basi elimu na sekta nyingine zote zitazunguka kwenye kilimo na kusupplement kilimo. Sijui kama hili tunalielewa ipasavyo. Ni kilimo tu ndicho kinachoweza kuinua mamiliioni ya watu wetu kutoka kwenye umaskini wa kutupwa.

This is the bottom line lakini inasikitisha kwamba hakuna anayelizungumzia hivi hata huko bungeni, both from upinzani na watawala.
 
Well said Mzee Mwanakijiji, na tunaendelea kupoteza fedha nyingi sana kwenye sera za industrialization ambazo kamwe hazitazaa matunda. Mapinduzi ya viwanda yataletwa tu na jasho la wakulima likitumiwa ipasavyo. Juzi kwenye hotuba ya kufunga mjadala wa wizara yake ya Viwanda, Dr. Kighoda alinishangaza sana na kauli zake kuhusu jinsi gani tutafanikiwa kuwa taifa lenye viwanda; navyoelewa, Dr Kigoda ni mchumi mzuri, so ilitakiwa aelewe kwamba atakayoenda eleza bungeni sio sahihi. Yapo kwenye hansard, nikipata muda nitayaleta humu.



This is the bottom line lakini inasikitisha kwamba hakuna anayelizungumzia hivi hata huko bungeni, both from upinzani na watawala.

Tatizo la baadhi ya wapinzani ni kuwa wanaamini sera za CCM ni nzuri tatizo ni wana CCM!
 
Back
Top Bottom