The Khoisan
Platinum Member
- Jun 5, 2007
- 18,628
- 18,242
Mswahili eti akijua kingereza na yeye anataka aongee kwa kubana pua Kama Raia wa America, huu ulimbukeni unapaswa ukemewe kwa nguvu kwani Wenye Lugha Yao wao hawana shida kwenye matamshi na hata ukiongea kingereza kibovu wanakuelewa pasipo kukushangaa kwani wanajua kuwa wewe haukuzaliwa London.
Mkuu hatuongelei Kiingereza kama taaluma bali kama lugha ya Taifa. kwa kuwa tumechagua Kiingereza kuwa lugha Taifa na ni ya kufundishia ni lazima tuielewe na kuimaster. Failure to do that ni KUSHINDWA KWA ELIMU!! Haiwezekani tuamue kutoa elimu kwa kiingereza halafu siku kijana anahitimu hawezi hata kujieleza kwa lugha aliyofundishiwa. Kwenda kutoa hotuba UN that is something else. Kama tungekuwa hatufundishwa kwa kiingereza au kama Kiingereza kisingekuwa ni lugha ya Taifa sidhani kama tungekuwa tunabishana hapa!!
Acha ujinga,kagame anaalikwa kutoa mada kwenye vyuo vikuu ughaibuni na anaongea na wasomi wale very comfortable kiingereza,hajikakamui kama huyu mwanaume wenu wa shoka hapo kideoni,tafute video za kagame akiongea kiingereza zipo nyingi tu u tube,ya lowassa ni hii moja tu,hakurudia tena kuthubutu kuongea tena hadharani,
Lugha ya Taifa ni Kiswahili na Kama shida ni ufahamu wa lugha wapo wakalimani watafanya kazi.Hivi nani alikudanganya kuwa huko London ndiyo wanazungumza Kiingereza kizuri!!? Tatizo siyo accent bali ni ufahamu wa lugha!!
Huyo jamaa sio kingereza tu hata kiswahili hawezi kujielezea bila kusoma
Kuingereza sio lugha ya taifa. Hadhi ya kiingereza hapa Tanzania ni Lugha ya kigeni, pia ni lugha inayotumika kwa mawasiliano na kufundishia mashuleni kuanzia sekindari mpaka elimu ya juu. Ni lugha ya biashara na official.
Lugha ya Taifa ni Kiswahili na Kama shida ni ufahamu wa lugha wapo wakalimani watafanya kazi.
Samahan wadau,naombeni mnijuze,HIVI LOWASA ANA DEGREE YA NIN?
Ok, ngoja nikubaliane nawe kuwa Kiswahili ni lugha ya Taifa halafu Kiingereza ni official language!!
Point yangu ni kuwa Kiingereza kuwa ni official language Tanzania ina maana ni lazima tukifahamua na tuweze kukiongea. Haiwezekani tujifunze kwa Kiingereza, tufanyiwe interview za kazi kwa Kiingereza halafu kesho tuseme siyo lazima kikijua Kiingereza sawasawa!! What the Heck!! I repeat and I will repeat again, UKO KUTAKUWA NI KUSHINDWA KWA ELIMU YETU!! Kwa nini tusifanyiwe interview za kazi kwa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili!!
Tanzania ni nchi pekee Duniani ambao watu wake hawawezi ku-communicate kupitia their own official language!!
Tatizo liko wapi? Ameongea vizuri na zaidi alichoongea ni kizuri zaidi na kinaonesha jinsi gani alivyo makini. kamwe mtoto hawezi kusoma vema na kuelewa kile anachofundishwa kama ana njaa.
wangapi wanaongea kiingereza kama waingereza wenyewe lakini wanachofanya ni utumbo mtupu.
Walisoma na Mama yako muulize
Acha matusi ya rejareja,mi nimeuliza tu,nataka kujua kwani sijawah kusikia akijinadi kwa elimu yake kama wengne wanavofanya! Afu naogopa KUONGOZWA na MBUMBU!
rais wa china au msumbiji au urusi huwa wanaongea kiingereza?Mdau umewahi kumsikia Lowassa akizungumza kiingereza????hebu mtazame hapa rais wetu huyu mpya halafu just imagine siku yuko cnn anahojiwa na Larry King na hivi vingereza vya kuandika kwanza then kukariri