Lowassa na falsafa ya maji kwenye pakacha

Lowassa na falsafa ya maji kwenye pakacha

Watanzania wapi?
Sema wafuasi wajinga wake ndiyo wanamuita Jembe lkn Lowassa ni zero hafai kabisa kwenye uongozi. Hats siku moja hajawahi kemea ufisadi

Mbona mnahangaika sana nyie vijana wasio na maono?wasio na vision?acheni mungu aitwe MUNGU kama mnaamini hivyo,lowasa ni jembe na hilo litabakia hivyo,kikubwa fanya analysis kwa kutokuwa bias utaelewa kwanini watu wanamuita jembe,
 
1.bongo ukiiba wewe ndo mjanja 2.ukiwa unatoa sana fedha hata bila kujua umetoa wapi na zina lengo gani wewe ndo jembe 3.wanafanya comparison na mkuu anayetawala sasa hivi

Lakini hao si indo wapiga kura wenyewe, au?
 
Mtahangaika sana kumchafua Lowasa,... Lowassa ni Jembe la Ukweli aliweza kupambana UFISADI kwa vitendo! Aliweza kuitemelea mbali kampuni ya City water iliyokuwa inaitafuna Taifa kama IPTL! Aliweza kukemea UFISADI wa kujikopesha kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii na matokeo yake fedha za kujenga UDOM na shule za kata zilipatika... LOwassa aliweza sana kukomesha Ufisadi uliokithiri kwenye Halmashauri zetu.... Kazi zote nzuri alizozifanya zimegeuka kazi bure, UFISADI kwenye halmashauri imetamalaki, IKULU inapiga deals kwa kwenda mbele... Sasa hivi Watanzania si wajinga tena!!! Wanajua kuwa Lowassa aliachia Ngazi baada ya kuona Ofisi Kuu inashidaaaa... Leo hii Heshima yake iko Juu, Watanzania tunahitaji huduma yake, utendaji wake na ueledi wake wa kimaendeleo!!!

Yoote umepatia lkn Umesahau Moja ambalo kwangu Mimi ndiyo Namba Moja na kwa nini namfagilia huyu Jamaa Lowasa nalo ni Maji ya Ziwa Nyanza, nilifika Kahama nikakuta Wakazi wake wanafungua bomba la Maji nikaambiwa yanatoka Ziwa Nyanza nikashangaa sana, hilo hapo ndipo nilipomkubali, halafu la Pili ni Ujenzi wa Shule za Kata, sasa nitakubali hoja za Watu wanaompinga Lowasa kama kuna Mtu ataniambia kwamba SIYO Lowasa aliyesimamamia Maji ya Ziwa Nyanza na ujenzi wa Shule za Kata kinyume na Hapo mimi kwangu Ni chaguo Namba Moja kwa sasa Nchini hata zaidi ya Nyerere!
 
Mimi neno FISADI nimeanza kulisikia likivuma kwenye mitaa enzi za LOWASSA, ndiyo maana kila anayeandika lolote linalomkataa LOWASSA huwa naungana naye. HAFAI hutu mtu.

Umekurupuka kaka,kajipange tena upya na ujitahidi sana kusoma na kungalia habari za nchi zingine hususan majirani zetu kenya,naona uelewa wako ni mdogo sana
 
Mwanasiasa Edward N. Lowassa ni mwanaCCM mwenzangu hasa. Lakini,hanizuii kusema ukweli juu yake. Natambua nia yake ya kutaka Urais wa nchi hii.Natambua tafiti mbalimbali zinazombeba Lowassa kama Mgombea mtarajiwa wa Urais ndani na nje ya CCM. Natambua hamu na shauku aliyonayo Lowassa kuongoza Tanzania. Kama Rais.

Amekuwa akijipambanua kama mtu wa maamuzi magumu. Na kama mwenye kipaumbele cha elimu. Chapuo zake zote zimejikita huko. Lakini,Lowassa si mgombea sahihi kwa CCM na watanzania. Ni kutokana na falsafa ya maji kwenye pakacha. Hata yajae namna gani,baada ya muda huisha yote na pakacha kubaki tupu.

Tatizo lililopo nchini kwasasa ni ufisadi na uwepo wa mafisadi. Pamoja na uwepo wa rasilimali na nguvu kazi (maji), ufisadi (pakacha) hukwamisha. Lowassa hajawahi,imaneno na kivitendo,kukemea pakacha hili. Ima kwa bahati mbaya au makusudi,Lowassa amekuwa akikwepa ajenda hii. Anakwepa tatizo kuu. Hana uwezo tuutakao mwakani na kuendelea. Bado hafiti.

Tunataka Rais anayechukia ufisadi na mafisadi kwa maneno na vitendo. Kwakuwa hilo ndilo pakacha linalopoteza maji ya Tanzania yetu. Na hata sura yake ioneshe hivyo. Lowassa kwa hili bado hajajipambanua vyema. Labda tusubiri zaidi.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Bila ya kukuvunjia heshima yako sijaona mgombea yoyote wa chama chenu ambaye yuko tayari kukemea hilo pakacha linalovuja (ufisadi). Labda kama na wewe umo kwenye orodha ya wagombea ila hujaweka wazi, basi ndio utakuwa wa kwanza!
 
Tatizo lililopo nchini kwasasa ni ufisadi na uwepo wa mafisadi. Pamoja na uwepo wa rasilimali na nguvu kazi (maji), ufisadi (pakacha) hukwamisha. Lowassa hajawahi,imaneno na kivitendo,kukemea pakacha hili. Ima kwa bahati mbaya au makusudi,Lowassa amekuwa akikwepa ajenda hii. Anakwepa tatizo kuu. Hana uwezo tuutakao mwakani na kuendelea. Bado hafiti.

Tunataka Rais anayechukia ufisadi na mafisadi kwa maneno na vitendo. Kwakuwa hilo ndilo pakacha linalopoteza maji ya Tanzania yetu. Na hata sura yake ioneshe hivyo. Lowassa kwa hili bado hajajipambanua vyema. Labda tusubiri zaidi.

H
ayo ni maoni yako na una uhuru wa kusema unachoona kinafaa,but the fact is the guy is the right candidate,unachotakiwa kujua ni kwamba hayuko kwenye system kwa sasa hivi na hawezi kukemea kitu chochote yeye ni mbunge wa kawaida kabisa,so naomba hii argument yako uje nayo one year baada ya mzee kuingia IKULU then utuulize hapa tutakuwa na majibu ya kutosha,lakini kwa sasa inabaki ni nadharia tu
Haya turudi nyuma alipokuwa waziri ; ni wapi aliwahi kukemea rushwa na ufisadi ?
 
Ufisadi ni sehemu mojawapo ya kuingizia ccm mapato hasa uchaguzi unapokaribia,kuna vijana wenzangu wanamkubali sana lowasa kwamba ni mchapa kazi pia fedha anazo hivyo hatoweza kuyumbishwa na matajiri akiingia madarakani,lakini kila ninae muuliza kuhusu richmond alifanya nini kuzuia ule ufisadi? Nasikitika wanaposema lile suala ni la ccm yote!! Wanadai hapaswi kuhukumiwa kwa jambo lile,inamaanisha kuwa hata akiingia madarakani anaweza kuachia ufisadi ufanyike kwaajiri ya chama,mtazamo wangu ccm kwenye ngazi ya urais hawana sifa kama ilivyotangulia kusema kada na waziri wa zamani matteo qaresi
 
Watanzania ndiyo wanaomuita Lowasa Jembe na mchapakazi, sasa swali ni kwamba ni kwa nini? Kwa nini wasimuite Pinda hivyo au sijui Sumaye?

Ingia Mtaani popote pale Tz na waulize tu Wananchi wa kawaida kuhusu Lowasa na wengi wao watakwambia ya kwamba jamaa ni Mchapakazi na pia ni fisadi, sasa kuna sababu kwa nini Watz wanamuona hivyo Lowasa, na kama ndivyo basi mimi kwangu ni poa tu na anafaa kama anapiga kazi na nchi inakwenda mbele!

mimi simwiti jembe na ni mtanzania,huyo mzee wenu ananuka RUSHWA waacheni watanzania wachague mtu mwingine.
 
mimi simwiti jembe na ni mtanzania,huyo mzee wenu ananuka RUSHWA waacheni watanzania wachague mtu mwingine.

Kwani ni nani amewakataza hao Watz kuchagua mwingine? Si wachague tu?
 
Mwanasiasa Edward N. Lowassa ni mwanaCCM mwenzangu hasa. Lakini,hanizuii kusema ukweli juu yake. Natambua nia yake ya kutaka Urais wa nchi hii.Natambua tafiti mbalimbali zinazombeba Lowassa kama Mgombea mtarajiwa wa Urais ndani na nje ya CCM. Natambua hamu na shauku aliyonayo Lowassa kuongoza Tanzania. Kama Rais.

Amekuwa akijipambanua kama mtu wa maamuzi magumu. Na kama mwenye kipaumbele cha elimu. Chapuo zake zote zimejikita huko. Lakini,Lowassa si mgombea sahihi kwa CCM na watanzania. Ni kutokana na falsafa ya maji kwenye pakacha. Hata yajae namna gani,baada ya muda huisha yote na pakacha kubaki tupu.

Tatizo lililopo nchini kwasasa ni ufisadi na uwepo wa mafisadi. Pamoja na uwepo wa rasilimali na nguvu kazi (maji), ufisadi (pakacha) hukwamisha. Lowassa hajawahi,imaneno na kivitendo,kukemea pakacha hili. Ima kwa bahati mbaya au makusudi,Lowassa amekuwa akikwepa ajenda hii. Anakwepa tatizo kuu. Hana uwezo tuutakao mwakani na kuendelea. Bado hafiti.

Tunataka Rais anayechukia ufisadi na mafisadi kwa maneno na vitendo. Kwakuwa hilo ndilo pakacha linalopoteza maji ya Tanzania yetu. Na hata sura yake ioneshe hivyo. Lowassa kwa hili bado hajajipambanua vyema. Labda tusubiri zaidi.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Ulivyosema ni sawa kabisa kuhusu Lowasa nakuunga mkono. Lakini kuhusu kukemea ufisadi hapahitaji mtu kusema bali kutenda. Ndio yeye ni fisadi na anawajua mafisadi wenzake. Kitu cha muhimu kwa Watanzania wa sasa ni elimu. Kama Lowasa anajua umuhimu wa ELIMU basi anawafaa sana Tanzania na nitapenda Slogan yake ya kampeni iwe ELIMU KWANZA. Watanzania wakielimika inatosha kuumaliza ufisadi uliopo kwani watakuwa na nafasi ya kuchagua na kuchaguliwa kutokana na uwezo wa kila mmoja. Mwache achukue kijiti kuelekea ELIMU bora kwa wote.

Hebu nikuulize kukemea ufisadi kunatosha kuumaliza?
 
Maamuzi magumu ni kibwagizo ambacho wanaimbishwa watanzania wenye akili nyepesi,lakini kiukweli maamuzi magumu ni maneno tu ya siasa nyepesi,mtu akiwajibika kwa kadiri anavyotakiwa na katiba basi ana maamuzi magumu.
 
Yoote umepatia lkn Umesahau Moja ambalo kwangu Mimi ndiyo Namba Moja na kwa nini namfagilia huyu Jamaa Lowasa nalo ni Maji ya Ziwa Nyanza, nilifika Kahama nikakuta Wakazi wake wanafungua bomba la Maji nikaambiwa yanatoka Ziwa Nyanza nikashangaa sana, hilo hapo ndipo nilipomkubali, halafu la Pili ni Ujenzi wa Shule za Kata, sasa nitakubali hoja za Watu wanaompinga Lowasa kama kuna Mtu ataniambia kwamba SIYO Lowasa aliyesimamamia Maji ya Ziwa Nyanza na ujenzi wa Shule za Kata kinyume na Hapo mimi kwangu Ni chaguo Namba Moja kwa sasa Nchini hata zaidi ya Nyerere!
"Zuzu"
 
mnatumia nguvu nyingi sana kumchafua lowasa lakini mtashindwa kila mtu anajua el ni mchapa kazi hakuna kama yeye
 
ulivyosema ni sawa kabisa kuhusu lowasa nakuunga mkono. Lakini kuhusu kukemea ufisadi hapahitaji mtu kusema bali kutenda. Ndio yeye ni fisadi na anawajua mafisadi wenzake. Kitu cha muhimu kwa watanzania wa sasa ni elimu. Kama lowasa anajua umuhimu wa elimu basi anawafaa sana tanzania na nitapenda slogan yake ya kampeni iwe elimu kwanza. Watanzania wakielimika inatosha kuumaliza ufisadi uliopo kwani watakuwa na nafasi ya kuchagua na kuchaguliwa kutokana na uwezo wa kila mmoja. Mwache achukue kijiti kuelekea elimu bora kwa wote.

Hebu nikuulize kukemea ufisadi kunatosha kuumaliza?

amefanya nini kuhusu elimu jimboni kwake ?
 
Back
Top Bottom