VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Mwanasiasa Edward N. Lowassa ni mwanaCCM mwenzangu hasa. Lakini,hanizuii kusema ukweli juu yake. Natambua nia yake ya kutaka Urais wa nchi hii.Natambua tafiti mbalimbali zinazombeba Lowassa kama Mgombea mtarajiwa wa Urais ndani na nje ya CCM. Natambua hamu na shauku aliyonayo Lowassa kuongoza Tanzania. Kama Rais.
Amekuwa akijipambanua kama mtu wa maamuzi magumu. Na kama mwenye kipaumbele cha elimu. Chapuo zake zote zimejikita huko. Lakini,Lowassa si mgombea sahihi kwa CCM na watanzania. Ni kutokana na falsafa ya maji kwenye pakacha. Hata yajae namna gani,baada ya muda huisha yote na pakacha kubaki tupu.
Tatizo lililopo nchini kwasasa ni ufisadi na uwepo wa mafisadi. Pamoja na uwepo wa rasilimali na nguvu kazi (maji), ufisadi (pakacha) hukwamisha. Lowassa hajawahi,imaneno na kivitendo,kukemea pakacha hili. Ima kwa bahati mbaya au makusudi,Lowassa amekuwa akikwepa ajenda hii. Anakwepa tatizo kuu. Hana uwezo tuutakao mwakani na kuendelea. Bado hafiti.
Tunataka Rais anayechukia ufisadi na mafisadi kwa maneno na vitendo. Kwakuwa hilo ndilo pakacha linalopoteza maji ya Tanzania yetu. Na hata sura yake ioneshe hivyo. Lowassa kwa hili bado hajajipambanua vyema. Labda tusubiri zaidi.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam