ALU255
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 2,089
- 2,125
Wana ukawa tusikate tamaa mungu habishani na mwanadam.KIPANDE CHA UNABII HIKI HAPA 'Kisha nikaona upepo uliotokea kanda ya ziwa ukipata alama nyingi za kukubalika siku ya kwanza ya uchambuzi wa alama kiasi kwamba ilisikika kila kona upepo huu utatawala miti ile.
Ghafla siku ya pili ya uchambuzi wa alama za kukubalika, upepo unaotokea mlima Meru ukapata alama zaidi na kuishangaza miti mingi, japo nguvu yake kubwa iliongezeka kutoka kwa miti mingi ya visiwani. Miti hii ya visiwani iliokoa na kuongeza zaidi alama za upepo uvumao kutoka Mlima Meru.
Kisha nikaona malaika akiandika alama katika ubao na hesabu yake ilikuwa mikono kumi na mmoja na nyongeza ya nukta kadhaa.
Naliona utata ukitokea katika kuwekwa wazi kwa alama hizo lakini baada ya msuguano Mungu aliingilia kati, kisha nikaona miti ikishangilia sana kwa sababu ya upepo utokao mlima Meru.
Haikuwa rahisi alama hizi, mikono kumi na mmoja na nyongeza ya nukta kadhaa kuwekwa wazi lakini Mungu aliingilia kati na nikaona ubaoni andiko hili (MITHALI 16:31).